TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, May 1, 2015

Serikali yadhamiria kukamilisha Miradi ya Kitaifa ya Kimkakati

Na Saidi Mkabakuli
Serikali imesema kuwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha miradi ya kitaifa ya kimkakati iliyoibuliwa katika Mpango wa Kwanza wa Maendeleo unaofikia kikomo mwaka ujao wa fedha wa serikali.
Hayo yalisemwa na Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu wakati akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Nagu alisema kuwa mpaka kufikia mwezi machi mwaka huu, serikali imefanikiwa kutandika reli za uzito wa ratili 56.12 kwa yadi kwa umbali wa km 9 kati ya stesheni za Lumbe, Mto Ugalla na Katumba; kukamilisha malipo ya ununuzi wa mabehewa 274 ya mizigo ambapo mabehewa yameshaanza kupokelewa Novemba 2014; kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli iliyoharibiwa na mafuriko katika maeneo ya Ruvu – njia panda ya Mruazi.
Waziri Nagu aliongeza kuwa kwa upande wa Barabara hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa kilometa 502.6 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kilomita 560, na ukarabati wa kilomita 78.8 za barabara kuu kwa kiwango cha lami dhidi ya lengo la kukarabati kilomita 131.5. Kwa upande wa madaraja hatua iliyofikiwa ni: kuendelea na ujenzi wa madaraja ambapo daraja la Kigamboni limefikia asilimia 75, Sibiti asilimia 22, Kilombero asilimia 26, Mbutu asilimia 99, Lukuledi II asilimia 25 na Kavuu asilimia 36.
Katika sekta ya Uchukuzi, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuongezeka kwa shehena iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 14.3 Machi 2015 dhidi ya lengo la tani milioni 13.0 kwa mwaka 2014/15; kuongezeka kwa ufanisi wa bandari katika kupakua magari kwa kila shifti moja ya saa 8 kufikia magari 886 kwa shifti kufikia Machi 2015 ikilinganishwa na lengo la magari 600 kwa shifti katika mwaka 2014/15; kupungua kwa muda wa meli kupakia na kupakua mizigo bandarini kutoka lengo la wastani wa siku 5 mwaka 2013/14 hadi wastani wa siku 3.7 kufikia Machi 2015; kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa malipo kwa njia ya mtandao mwezi Julai, 2014; na kuanza  kutoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kwa masaa 24 kwa siku zote za juma. Aidha, kwa upande wa bandari ya Bagamoyo, hatua iliyofikiwa ni kusainiwa kwa makubaliano ya ujenzi wa bandari; na kutangazwa kwa zabuni kwa ajili ya kupata wawekezaji katika bandari za Mtwara na Mwambani -Tanga.
“Katika sekta ya nishati, hatua iliyofikiwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam (km 542) Machi 2015, na ujenzi wa mitambo ya kusafisha gesi Madimba (Mtwara) na Songosongo (Lindi) umefikia asilimia 86.9 ambapo unatarajiwa kukamilika Juni 2015. Kwa upande wa usambazaji wa umeme vijijini, wateja wapya 2,602 wameunganishiwa umeme katika mikoa ya Simiyu, Singida, Kagera, Tanga, Ruvuma, na Iringa,” alisema Dkt. Nagu.
Kwa mujibu wa Waziri Nagu, shughuli nyingine zilizotekelezwa nia katika sekta ya nishati, ni pamoja na kukamilika kwa usimikaji wa mitambo 4 ya kufua umeme yenye uwezo wa jumla ya MW 150, kuendelea na ujenzi  wa vituo vya kupoza na njia za kusafirisha umeme, na kuendelea na ujenzi wa  karakana, majengo ya utawala, na barabara za ndani katika mradi wa Kinyerezi I; kukamilisha ulipaji fidia kwa eneo la Makambako katika mradi wa usafirishaji umeme wa Makambako - Songea;  na kuanza ujenzi wa nguzo za njia ya umeme katika mradi wa msongo wa kV 400 wa Iringa – Shinyanga.
Akiwasilisha kazi zilizotekelezwa katika sekta  ya Maji, Dkt. Nagu alisema kuwa  ulazaji wa mabomba katika mradi wa maji Ruvu Chini kutoka Bagamoyo hadi Dar es Salaam kazi ambayo imekamilika kwa kilomita 52.43 kati ya kilomita 55.93 za mradi sawa na asilimia 93.8; kwa upande wa mradi wa maji Ruvu Juu: mkandarasi amekamilisha utafiti wa udongo na uchunguzi wa awali wa mahali yatakapojengwa matanki Kibamba na Kimara; na kwa upande wa mradi wa Bwawa la Kidunda,  wananchi wamelipwa fidia ya shilingi bilioni 7 kupisha ujenzi wa barabara na eneo litakapojengwa bwawa.
Kwa upande wa miradi ya maji vijijini, jumla ya miradi 123 ya maji ilijengwa na kukamilika. Idadi hii imenufaisha wananchi wapatao 463,750 na kuongezeka kwa ufanisi katika masuala ya ununuzi wa huduma katika mikataba kutoka siku 265 hadi siku 90. Aidha, Serikali imeendelea na ujenzi wa mabwawa ambapo bwawa la Iguluba (Iringa) na Wegero (Mara) yamekamilika. Vile vile, ujenzi wa bwawa la Kawa (Rukwa) umefikia asilimia 95, bwawa la Sasajila (Dodoma) asilimia 66.09 na Mwanjoro (Shinyanga) asilimia 45.4,” aliongeza Waziri Nagu.
Katika sekta ya kilimo, Dkt. Nagu aliyataja mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: kupatikana kwa hati za mashamba mawili ya Bagamoyo na Mkulazi; maghala 30 yamekarabatiwa na kupatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbozi na Momba.  Vile vile, skimu 30 za umwagiliaji zimepatiwa watoa huduma binafsi katika Wilaya za Mbarali, Kyela na Iringa; na mafunzo juu ya kubaini na kudhibiti visumbufu, matumizi bora ya maji, utunzaji na matengenezo ya miundombinu ya umwagiliaji na kutumia mwongozo wa uendeshaji skimu za umwagiliaji yametolewa.  Aidha, ujenzi wa maghala 2 katika Wilaya ya Mlele umekamilika.
Vile vile katika sekta ya viwanda, Waziri Nagu alizitaja kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilika kwa ukarabati wa barabara ya Itoni - Mkiu - Liganga na Mchuchuma kwa kiwango cha changarawe ili kuwezesha mitambo kufika maeneo ya Mchuchuma na Liganga; na kuanza uthamini wa mali za wananchi watakaohama eneo la Mchuchuma. Vile vile, fidia shilingi bilioni 53 imelipwa katika eneo la kujenga kituo cha Biashara na Huduma Kurasini; na fidia ya shilingi bilioni 7 imelipwa katika eneo la uwekezaji Bagamoyo na Serikali imesaini mkataba na kampuni ya China Mechants Holding International kwa ajili ya kujenga bandari na eneo la viwanda. Aidha, katika kiwanda cha kuzalisha dawa ya kuua viluwiluwi wa mbu, Kibaha, kazi ya ufungaji wa mitambo na ujenzi wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika kabla ya Julai, 2015.
Akizungumzia upande wa maendeleo ya rasilimali watu, Dkt. Nagu alisema kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na kuendelea kugharamia wanafunzi 159 wanaoendelea na mafunzo katika fani za mafuta na gesi kwa ngazi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya nchi ambapo wanafunzi 124 wanagharamiwa na Serikali na wanafunzi 35 wanagharamiwa na nchi wahisani; na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika vyuo vikuu na vyuo vya ualimu, ufundi na ustawi wa jamii.
Kwa upande wa utafutaji wa rasilimali fedha, Waziri Nagu alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania inatumia kanzidata bora inayohifadhi taarifa inayoweza kuthaminisha bidhaa na hivyo kutoa makadirio bora zaidi ya viwango vya kodi. Vilevile, alisema kuwa tozo kwa ajili ya uwekezaji katika elimu umeanza Julai 2013 ikiwa asilimia 2.5 ya mapato ghafi ya kampuni za simu.
“Katika sekta ya fedha, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuongezea Benki ya Maendeleo ya Kilimo mtaji wa shilingi bilioni 60; kuendelea kuongeza mtaji wa Benki ya Rasilimali kufikia shilingi bilioni 212 ambapo mtaji kutoka Serikalini ni shilingi bilioni 152.2 na shilingi bilioni 59.8 zimetokana na malimbikizo ya faida; na  mali za Benki ya Maendeleo ya Wanawake Tanzania ziliongezeka kutoka shilingi bilioni 26.5 mwaka 2013 hadi shilingi bilioni 34.8 mwaka 2014,” alisema Dk. Nagu.
Kuhusu eneo la huduma za utalii, Dkt. Nagu aliongeza kuwa kazi zilizofanyika ni pamoja na usanifu wa ujenzi wa Utalii House awamu ya pili na kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji mapato (utalii, uwindaji na upigaji picha). Aidha, idadi ya watalii kutoka nje iliongezeka kutoka watalii 1,090,905 mwaka 2013 hadi watalii 1,102,026 mwaka 2014. Vile vile mapato yatokanayo na utalii yaliongezeka kutoka dola za Marekani bilioni 1.81 mwaka 2013 hadi dola za Marekani bilioni 1.98 mwaka 2014.
Kwa upande wa Biashara, hatua iliyofikiwa ni kurekebisha sheria ya mfumo wa stakabadhi ghalani na kutoa  elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu mfumo huo; kuanzishwa kwa kampuni ijulikanayo kama Tanzania Mechantile Exchange plc kusimamia na kuendesha soko la mazao ya bidhaa na kuhamasisha matumizi ya fursa za masoko ya mipakani, Kikanda na Kimataifa,” aliongeza.
Kwa mujibu wa Dkt. Nagu maandalizi ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2015/16 yamezingatia maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16). Aidha, Mpango huu umezingatia Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini – MKUKUTA II (2010/11 – 2014/15), Malengo ya Milenia, Mwongozo wa Mpango na Bajeti  kwa mwaka 2014/15; Mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo 2014/15 yaliyojadiliwa na Bunge Novemba, 2014; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2010 – 2015); na sera na mikakati ya kisekta.
====================================================
 Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu
 akiwasilisha Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya
 Mpango ya Bunge Zima kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Sehemu ya Wabunge waliohudhuria uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima wakimsikiliza Waziri wa nchi 
(Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu kwenye Ukumbi wa Mikutano
 wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia kwa makini hotuba ya  uwasilishaji wa Mpango wa 
Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
Baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) 
akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. 
Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa 
Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy (Kulia) akimpongeza Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu,
 Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kushoto) mara baada ya kuwasilisha Mpango wa Maendeleo wa 
Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akiongea na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashilila (Kulia) mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima. Anayewasikiliza ni Naibu Katibu Mtendaji (Sekta za Uzalishaji) kutoka  Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy.
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kushoto) akiongea na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mara baada ya uwasilishaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 Katika Kamati ya Mpango ya Bunge Zima.
viongozi waandamizi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia uwasilishaji wa
 Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2015/16 uliokuwa ukifanywa na Waziri wa 
nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu katika Kamati ya Mpango
 ya Bunge Zima.

Saturday, April 25, 2015

MWALIMU NYERERE, BANDARI WATOSHANA NGUVU -NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIPS-KIGAMBONI.


-DACICO MWENDO MDUDO
-USTAWI WA JAMII YATUMIA VYEMA UWANJA WA NYUMBANI.

 Na: Mwandishi Wetu,

Michuano ya NACTE INTER COLLEGE CHAMPIONSHIPS TANZANIA-DAR ES SALAAM 2015, Leo imeendelea tena kwenye Viwanja vya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambako Timu za kundi A zimecheza na mchezo uliokuwa gumzo ni baina ya Chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere dhidi ya Chuo cha Bandari, ambapo hadi Mwisho wa Mchezo Timu hizo zimeweza kufungana 3-3.
Timu ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ndiyo waliokuwa wa kwanza kupachika mabao 2 kipindi cha kwanza, ambapo hadi timu hizo zinakwenda Mapumziko Mwalimu Nyerere ilikuwa mbele kwa 2-0.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa NACTE, Mheshimiwa Alex Nkondola wa kwanza kushoto, akipokea Kombe la Michuano ya NACTE INTER COLLEGE CHAPIONSHIPS TANZANIA 2015. wengine ni Mwanasheria Mkuu wa NACTE Exemarry Mize wa pili kushoto na wawakilishi wa Mawaziri wa Michezo wa Serikali za Vyuo Tanzana, Ladislaus Thumbu wa kwanza kulia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Samweli Gukwi kutoka chuo cha Taasisi ya Elimu ya Watu wazima. Michuano hiyoinatazamiwa kufikia kilele May 30.
kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote zilifanya mabadiliko ya hapa na pale lakini ni ya Mwalimu nyerere tena iliyoweza kupata bao la tatu kabla ya Timu ya Bandari Kusawazisha mbao yote kwenye dakika za Mwisho za mchezo huo  ambao hakika ndiyo uliokuwa gumzo katika siku ya leo.
Mchezo mwingine ilikuwa ni kati ya IFM dhidi ya chuo cha Taasisi ya  Elimu ya Watu wazima, ambapo mchezo huo timu hizo zimekubali kugawana pointi moja moja sambamba na wenzao wa chuo cha Kilimanjaro kwa mama ngoma waliogawana pointi na chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT).
Matokeo ya kundi la Uwanja wa Ustawi wa Jamii timu ya Chuo cha Biashara CBE, wamefanikiwa kujipatia Pointi zao 3 na magoli mawili baada ya timu ya chuo cha Uhasibu kushindwa kutokea Uwanjani katika kipindi kilichopangwa.
mchezo mwingine ilikuwa ni baina ya timu ya Chuo cha kodi ambao wamecheza na timu ya kitivo cha engeneering ya chuo Kikuu cha Dar es Salaam zimeweza kugawana Pointi baada ya timu zote kushindwa kufika Uwanjani.

wakati mchezo wa Mwisho wenyeji timu ya chuo cha ustawi wa jamii imeweza kujipatia Ushindi mnono wa Mabao mawili na hivyo kujizolea pointi zote tatu dhidi ya timu ya chuo cha Wauguzi wa Muhimbili, ambapo michezo hiyo awali ilipangwa kufanyika kwenye Viwanja vya chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini imelazimu kubadili Uwanja kutokana na Viwanja vya Chuo Kikuu kuwa na ratiba katika kipindi hiki hivyo michezo yote sasa itafanyika kwenye viwanja vya Ustawi wa jamii katika hatua hii ya makundi.
Kundi B ambao michezo yake inafanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha, mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu za chuo cha St.Joseph, ambapo katika mchezo timu ya St. JOSEPH ilifanikiwa kuibua na ushindi wa mabao mawili kwa bila (2-0) dhidi ya timu ya chuo cha Njuweni Insititute.
mchezo mwingine Timu ya chuo cha Wauguzi Tumbi ikafanikiwa kupata Point 3 baada ya kujipatia mabao mawili dhidi ya kitivo cha UDBS ambao walishindwa kutokea uwanjani kabla ya DACICO kidedea dhidi ya timu ya chuo cha taifa cha Teckinolojia (D.I.T) .
Washindi wawili katika kila kundi ndiyo watakaoingia hatua ya Robo fainali itakayoshirikisha jumla ya timu nane huku timu mbili zikipewa nafasi ya kuingia kwa njia ya upendeleo(Best Looser).
Michezo hii inaratibiwa na Kampuni ya Miss Demokrasia Tanzania & Enter tainment C.o Ltd, ya jijini Dar es Salaam kwa Udhamini wa NACTE, SBC TANZANIA, Vodacom, CXC Tours, Zinduka, Mlimani Radio & Mlimani Tv, Clouds Media, Michuzi Media, Tanzania Daima, Free Media, Global Publishers, Gazeti la Champion, Njuweni Institute Kibaha na Mpaluleblog:

Mawasiliano Tupigie: +255-713-86-91-33 au +255-767-8691-33

Friday, April 24, 2015

PEPSI YANG'ARISHA MAONYESHO YA SYRIAN YAFUNGULIWA LEO DIANOND JUBILEE HALL- JIJINI DAR ES SALAAM.

 Baadhi ya wanafunzi jijini Dar es Salaam, ndani ya maonyesho ya hayo
 Baadhi ya wanafunzi jijini Dar es Salaam, ndani ya maonyesho.
 Baadhi ya wanafunzi jijini Dar es Salaam, ndani ya maonyesho.
 Baadhi ya wakazi wa jiji wakiwa kwenye Mapumziko kwenye mabanda ya Pepsi
 wakazi wa jiji wakipumzika kwenye mabanda ya Pepsi
 wakazi wa jiji baada ya kufurahia maonyesho hayo
 Baadhi ya wafanyabiashara jijini wakiwa kwenye maonyesho ndani ya Viwanja vya Diamond jubilee
 Baadhi ya wafanyabiashara jijini wakiwa kwenye maonyesho ndani ya Viwanja vya Diamond jubilee
Fuatilia Maonyesho hayo kupitia hapa hapa kila siku, au piga simu +255-713-869133

Wednesday, March 25, 2015

Amazing Talent ! Haya sasa wanao muweza He Kills The Dance !




TUKIO LA KUSIKITISHA LILILOWAHI KUTOKEA




MAREKANI YAZIDI KUWA GUMZO



MICHEZO YA HATARI DUNIANI WATANZANIA WATAKA KUINGIA KWENYE MAPAMBANO WWE



angalia maajabu ya huyu kijana Msanii wa wasanii duniani




BULEMBO AGEUKWA NA WAJUMBE WAKE SAKATA LA KWENDA KWA LOWASSA
















Life of Pageant Planet Episode 10



Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ameibuka na kupinga tuhuma zilizotolewa na baadhi ya watu kwamba amekusanya makundi ya kumuuga mkono huku akidai hana sababu ya kufanya hivyo na hana uwezo wa kuwagharamia watu hao wanao muunga mkono.




Monday, March 23, 2015

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAWEKEZAJI WA NCHI 5 ZA AFRIKA MASHARIKI.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
23/3/2015. Dar es salaam.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na Marais wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu. 

Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki  amesema kuwa Marais hao Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na  jumla ya wawekezaji 350.

Amesema Tanzania kwa mara nyingine imepata heshima ya kuandaa mkutano huo na kufafanua  kuwa wawekezaji hao wamekwisha anza  kuwasili jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 22 , Machi huku marais nchi hizo wakitarajiwa kuwasili jijini humo kuanzia Machi 24,2015.

Amesema wakiwa nchini Tanzania Marais hao watashiriki kwenye mkutano wa wawekezaji utakaofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Mwalimu J.K.Nyerere kuanzia Machi 23 hadi 26, watatembelea bandari ya Dar es salaam ili kuona namna nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki zinavyoshirikiana katika masuala ya ushuru wa forodha na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali.

Amebainisha kuwa kabla ya kuaondoka nchini  Tanzania Machi 26, 2015 Marais hao pia watatembelea miundombinu ya reli inayotumika kusafirisha mizigo nchi za maziwa makuu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali baina ya nchi zao.

KUHUSU  MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM.

Aidha, kuhusu mvua zinzoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam  na kusababisha madhara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amewataka wananchi kuzingatia agizo la kuhama mabondeni na maeneo mengine hatarishi ili waepuka maafa kufuatia watu 7 kupoteza maisha kutokana na kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha.

Akifafanua kuhusu matukio hayo Mhe. Sadiki amesema maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo  na kupata maafa hayo ni bonde la Mto Msimbazi na eneo la Buguruni kwa Myamani.

Amesema kuwa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo yameonekana kuwa  na wingi wa takataka ngumu na wingi wa mifuko ya plastiki  iliyotupwa na wakazi hao hali iliyochangia kuziba mifereji inayopeleka maji katika bonde la mto Msimbazi na maji hayo kuhamia kwenye makazi ya watu.

Ameeleza kuwa kazi ya uokoaji , kumwaga dawa kwenye maji yaliyotuama ili kuzuia athari ya magonjwa ya milipuko, kuzibua mifereji na kukusanya taka katika maeneo hayo inaendelea ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi  na kuwataka wakazi hao kuepuka kutupa taka ngumu zinazoziba mifereji ya maji.

Amesema Serikali inasubiri taarifa kutoka kwa viongozi wa Serikali za Mitaa kwa maeneo ambayo wakazi wake wanaishi kihalali ili waweze kupatiwa misaada ya kibinadamu.

Kwa upande wake Kamishina wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amethibitisha vifo vya watu hao 7 waliopoteza maisha kutokana na maeneo yao kukumbwa na mafuriko pamoja na athari ya Umeme.

Akitoa ufafanuzi wa vifo hivyo amesema kuwa watu 5 wamepoteza maisha kwa kusombwa na maji na wengine 2 wamepoteza maisha kutokana na ajali iliyosababishwa na Lori moja kugonga Transfoma ya umeme eneo la Buguruni Mnyamani.

Kamishna Kova amesema tayari Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO) wameunda kikosi kazi cha uokoaji.

Ametoa wito kwa madereva wa magari ya mizigo, mgari binafsi na yale ya abiria kuepuka kupita katika maeneo yaliyojaa maji ili kuepuka ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoa taarifa ya mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na wakuu wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.
Kamishina wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Dar es salaam na vifo vya watu  7 waliopoteza maisha  kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam.

The fallout reached a fever pitch at at New Galilean Baptist Church this Sunday.


NINI MTAZAMO WAKO KUHUSU BUNGE LETU NA SERA ZA VIONGOZI WETU?


ANGALIA TECKNOLOJIA ILIPOFIKIA KATIKA UPIKAJI WA MANDAZI