TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 1, 2012

FRANCIS CHEKA NA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA

Bondia Mada Maugo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba uho leokupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprili 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari leo kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Makamu mwenyekiti wa Oganizesheni ya ngumi za Kulipwa Nchini, Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Francis Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Exim Bank Chairman Mr. Yogesh M. Manek (left) and the FMO, Director Financial Institutions Ruurd Brouwer all smiles shortly after signing a Memorandum Of Understanding (MOU) that saw Exim Bank secure a 16bn/- ($10m) from the Dutch development bank.
Exim Bank Chairman Mr. Yogesh M. Manek (left) and the FMO, Director Financial Institutions Ruurd Brouwer all smiles shortly after signing a Memorandum Of Understanding (MOU) that saw Exim Bank secure a 16bn/- ($10m) from the Dutch development bank.
Dar es Salaam. Febuary 1, 2012. EXIM Bank Tanzania has secured a $10 million (TSH 16bn) loan from FMO, a Dutch development bank, which is poised to set the stage for a revitalised fiscal environment in the banking sector in Tanzania.
The historic agreement was signed in Dar es Salaam yesterday between Mr. Yogesh M. Manek, Chairman, Exim Bank and Mr. Ruurd Brouwer, Director Financial Institutions, FMO.
The loan will be payable within a seven year tenure at an interest rate of six percent according to Exim Bank Chairman Yogesh M. Manek.
Speaking to journalists shortly after the signing ceremony, Manek said the loan will help find solution to the long term credit needs of Small and Medium Enterprises (SMEs) operating within the country.
“We are happy that FMO has expressed faith in us", he further added. Indeed, it’s another feather in the bank’s cap!
Manek said Exim bank’s plans are afoot to further shore up long term borrowings during the current year, pursuant to the continuous demand for long term credit in the economy, which is a positive indicator to a growing economy.
“Articulating such a financial strategy serves to put the weight of surplus monetary supply behind the growing long-term credit needs of the bank’s clients in Tanzania,” he added.
The FMO Director Financial Institutions, Mr. Ruurd Brouwer, said “Entrepreneurship is key in creating sustainable economic growth and improving people’s quality of life. We have chosen to partner with Exim because the institution has a reputable financial stand.”
“By supporting Exim’s growth, especially in SMEs and agriculture based enterprises, we believe that our contributions will have a long term impact on the country’s economic development,” he added.
He added that FMO has for many years been supporting sustainable private sector growth in developing and emerging markets by investing in enterprising entrepreneurship,
“A strong private sector leads to economic and social development; empowering people to employ their skills productively can enhance the quality of their lives
“This will not be the end of our relationship. W e are looking foward to working together with Exim Bank again,” he added.
He said FMO focuses on four sectors that have high development impact: financial institutions, energy, housing and agribusiness. With a commanding investment portfolio of EUR 5 billion, including EUR 1.5 billion worth of investment in Africa, coupled with an active presence in 20 African countries, encompassing Nigeria, Ghana and Mozambique.
Exim Bank has succeeded in establishing its dominion in the banking sector with an impressive territorial map dotted with 75 footprints, comprising 22 branches in Tanzania, 2 overseas subsidiaries in Djibouti and Comoros Island and 51 ATMS. A healthy asset size of T. Shs. 855 billion,as ascertained on 31stDec. 2011, confirms Exim Bank’s robust and flourishing status.
Extending its services globally, Exim Bank caters to the international needs of its customers through correspondent banking relationship with other international banks that include HSBC Bank, Banker’s Trust, U.S.A. and Deutsche Bank AG, London.

Ilifika wakati Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kutoa nasaha zake kwa wanafunzi wanaohitimu. Kwanza kabisa aliwaambia wanafunzi hao kuwa alikuwepo mahala hapo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda ambaye hakuweza kuhudhuria mahafali hayo kutokana na kukabiliwa na shughuli nyingine muhimu za kiserikali.
Katika nasaha zake hizo aliwataka Wanafunzi hao kujijengea fikra za kujiajiri pindi wamalizapo masomo yao na sio kubaki kuitegemea Serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya. "Jitahidini muokoe maisha yenu wenyewe, mnahitaji kulea maisha yenu...Askari namba moja ni wewe kuikoa familia yako" Alisema Injinia Manyanya.
Alizungumzia pia suala la mimba za mashuleni na kusema kuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya elimu mashuleni. Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaahidi wale wote watakaopata Division One na Two atahakikisha anawasaidia kupata Shule za kujiendeleza.
Katika nasaha zake hizo aliwataka wanafunzi hao kutopumbazika na kauli za baadhi ya viongozi na wananchi kuwa eti Watanzania ni masikini. Aliwataka kutumia fursa waliyonayo katika kuhakikisha jamii inaondokana na fikra hizo na kujiendeleza zaidi kielimu waweze kuikomboa jamii ya wanarukwa.
Kwa upande mwingine aliwataka wazazi wote Mkoani Rukwa kuwasaidia watoto wao kufikia malengo ya kuwa na elimu bora. Aliomba ushirikiano kutoka kwa wazazi pamoja na waalimu ili kuiweka Rukwa katika hatua nyingine kielimu. Aliwaasa wazazi kuchangia huduma za elimu ikiwepo chakula mashuleni.
Alisema kuwa Rukwa kama Mikoa mingine inakabiliwa na tatizo la uhaba wa waalimu na kuwataka waalimu wanaopangiwa Rukwa kuondokana na fikra potofu za imani za kishirikina na kwamba Rukwa ni Mkoa salama ambao mambo hayo sasa yamebaki kuwa ni historia.
Lilifuata zoezi la ugawaji wa vyeti kwa wanafunzi wanaohitimu. Hapo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akimkabidhi cheti mmoja ya wahitimu katika Shule hiyo.
Mkuu huyo wa shule akikabidhi taarifa yake hiyo kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa Mkoa alianza shughuli za mahafali hayo kwa kukagua Kikosi cha Gwaride la shule hiyo ambacho kilikuwa kimejipanga kikakamavu bila ya kutikisa hata kidole.
Burudani ya Muziki kutoka kwa wanafunzi wanaohitimu ilichukua nafasi yake kuweka mazingira sawiyya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ndiye aliyefungua Muziki ikiwa ni ratiba ya mwisho kwenye mahafli hayo. Hapo akionekana na baadhi ya wanafunzi wakivunja mifupa.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita 2012 shule ya Sekondari Usevya.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akisalimiana na Mzee Kayanza Pinda wakati alipowatembelea jana kuwajulia hali. Kushoto ni Mama Kayanza Pinda ambao ni Baba na Mama wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiwa katika picha ya pamoja na Mzee na Bibi Kayanza Pinda ambao ni wazazi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwao Kibaoni Wilayani Mpanda Mkoani Rukwa. Mkuu wa Mkoa alikuwa Wilayani hapo kumuwakilisha Waziri Mkuu kwenye mahafali ya Kidato cha sita Shule ya Sekondari Usevya.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitaniana na Mzee Kayanza Pinda alipokuwa anamuaga kuelekea kwenye mahafali ya Shule ya Sekondari Usevya ambapo alienda kumuwakilisha Waziri Mkuu aliyekuwa amealikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye mahafali hayo. Miongoni mwa utani alioutoa Mzee Pinda ni pamoja na kumuita Mkuu huyo wa Mkoa "Mnyatomato" kumaanisha kuwa ni Mtoto wa Manyanya ambapo nyanya kwa kiingereza ni Tomato.  (NA HAMZA TEMBA-AFISA HABARI RUKWA)

Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Samwel Daniel na mkewe Kaindi Taratibu wakiwa kwenye picha huku bwana harusi akiwa amembeba mke wake, baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxury jijini Dar es Salaam.
Wakiwa na nyuso za furaha Bwana harusi Samwel Daniel na mkewe Kaindi Taratibu wakiwa kwenye pozi la picha baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luuiry jijini Dar es Salaam.
Bw.harusi Samwel akiwa na mkewe Kaindi wakishuka kutoka katika mlima kilimanjaro uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kufanya utalii wa ndani.Baada ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28.
Bibi Harusi akipita juu ya migongo ya wakwe zake wakati wa kuingia ukumbini ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika familia, kabila la Wayao .
Bw. Harusi akipita juu ya migongo ya wazazi wake wakati wa kuingia ukumbini wakati wa harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxiry jijini ,Dar es Salaam.utamaduni huu hufanywa na watu wa lindi kabaila la wayao.

MAMBO MANNE YATAJWA KWENYE MKATABA WA UANZISHWAJI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 Mkurugenzi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Kayabukama Kiliba katikati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam makao makuu juu ya mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya Afrika mashariki ambao umeainisha hatua nne za mtangamano ambazo ni umoja wa forodha soko la pamoja, Umoja wa Fedha na Shirikisho la Kisiasa.kushoto Stephen Mbonde mkurugenzi msaidizi masuala ya ulinzi na usalama.kulia Mkurugenzi msaidizi masuala ya siasa Patric Mwatonoka
Mkurugenzi Msaidizi masuala ya Ulinzi na Usalama Stephen Mbonde(Kushoto)akifafanua jambo makao makuu juu ya mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya Afrika mashariki, kati ninMkurugenzi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Kayabukama Kiliba, na  Mkurugenzi msaidizi masuala ya siasa  Patric Mwatonoka
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo hayo leo.(Picha Zote na Philemon Solomon).

MGOMO WA MADAKTARI HAPA NCHINI WAZIDI KULETA SURA MPYA


 Waziri wa Afya, Haji Mponda (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Mgomo wa Madaktari, mazungumzo yaliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili, kushoto ni Dkt, Laurence Museru wa Muhimbili.

 Baadhi ya wauguzi katika Hospitali ya Muhimbili wakiwajibika
 Mwenyekiti wa GOOD NEWS FOR ALL MINISTRY , Askofu  Charles Gadi(kati) akiwa na wenzake 
walipotembelea Hospitali ya Muhimbili kwa lengo la kujionea hali halisi ikiwa ni pamoja na kufanya maombezi kunusuru hali ya migomo ya Madaktari hapa nchini
 Kikosin cha Madaktari kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), Muda mfupi baada ya kuwasili katika Hospitali ya Rufaa Muhimbi, hapa walikuwa na mazungumzo na Waziri wa Afya na Waandishi wa Habari
 Baadhi ya Madaktari kutoka jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ), wakipokea wagonjwa Muhimbili
 Mgonjwa anayedaiwa kuwa wa Kichaa, akiwa katika hali ya uangalizi mkali katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili
Waziri wa Afya, Haji Mponda(kulia), akiwa na mazungumzo na baadhi ya watendaji wa Muhimbili pamoja na Madaktari kutoka jeshi la wananchi JWTZ jana.(Picha Zote na Medard Akonaay ).

MASHUJAA MUSICA YATIMUA BAADHI YA WANAMUZIKI

Aliyekuwa Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica-Jado Fidifoce(kulia), akiwa na Meneja wa Bendi hiyo, Khamisi,
Bendi ya Mashujaa Musica ya jijini Dar es Salaam, imetangaza kuwafukuza kazi baadhi ya wanamuziki wake kwa kile walichokiita Utovua wa nidhamu,
akizungmza kwa njia ya Simu Meneja wa Bendi hiyo, Khamisi Khamis, amesema leo kuwa uhamuzi wa kuwaachisha kazi wanamuziki hao umetokana na tabia zao kushindwa kuvumilika katika kundi hilo ambapo wamekuwa wakisababisha upotevu wa amani mara kwa mara.
aidha panga hilo ambalo limepita pia kwa aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo, Jado Fid Foce, ambaye hivi karibuni alijiengua katika nafasi yake ya Uongozi kwa madai ya kupisha kiti hicho kukaliwa na Mtu mwingine, 
wengine waliokumbwa na Pangua pangua hiyo ni pamoja na Pasia Budansi(Mwimbaji),Dulla Ngoma(Mpiga tumba), Jimmy Adoly(mwimbaji), Zidane Chapati(Rapa), wakati kwa upande wa wacheza shoo walioachishwa kazi ni Kevini, Mwiba, Baby White, jack pamoja na Kamodee.
Mashujaa Musica Bendi hivi sasa inakuja kwa kasi katika ulimwengu wa burudani ya miziki ya dansi kiasi cha kuziogopesha baadhi ya bendi kongwe zikiwemo za Twanga, FM Academia, Extra Bongo, Mapacha watatu na zingine nyingi, 
siku ya leo jumatano bendi hiyo inapatikana katika Ukumbi wake wa nyumbani wa Mashujaa na siku ya ijumaa bendi hiyo inakuwa katika ukumbi wa Business Complex  Victoria barabara ya kuelekea Mwenge.

TAASISI YA LIVERPOOL FAMILY YA HAPA NCHINI YAANDAA TAMASHA

Mkurugenzi Ufundi-Seleman Methew,(kati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Taasisi ya Liverpool,mazungumzo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo leo,kushoto ni Katibu wa Liverpool, Ramadhan Kitunga,  na Mwaasisi Hamiss Ahamed Gwatamu.
.............................................................................................
MASHABIKI wa klabu ya Liverpool waliopo  hapa nchini wameandaa Tamasha la muziki wa taarabu litakaloitwa First Seven Morden Taarab, ambalo pia litajumuhisha michezo kama Mpira wa Miguu, ikiwa ni pamoja na kutembelea Hospital ya watu wa Moyo .

Akizungumza jijini Dar es SalaamMuda mfupi Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Selemani Methew amesema kuwa Liverpool Sports Family (LSF) ni taasisi iliyosajiliwa kisheria mnamo mwaka 2009 kwa msajili wa vyama vya Michezo kwa hati namba NSC:9168 SDDW.
na kuongeza kuwa pamoja na mambo mengine Malengo ya Liverpoool Sports Family ni kukuza Mahusiano ya Kidugu baina ya mashabiki wa klabu ya Liverpool waliopo hapa nchini sambamba na kukuza Maendeleo ya Michezo hapa kwetu Tanzania.
Aidha siku ya jumapili tasisi hii imepanga kuwa na mkutano wa wana (LSF) 
uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa Meeda kuanzia saa saba mchana ambapo ametoa wito kwa Makampuni mbalimbali kujitokeza kuunga mkono ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha wapenzi wa timu nyingine za nje waliopo kufika kwa lengo la kujfunza ili kwa pamoja waweze kuwa na mshikamano katika kukuza michezo hapa nchini.

Tuesday, January 31, 2012

TWIGA STARS , NAMIBIA ZAINGIZA MIL 38/-


Mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia (Brave Gladiators) imeingiza sh. 38,220,000.
Kiasi hicho ni kutokana na watazamaji 16,334 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa juzi (Januari 29 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Twiga Stars kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 1,000 (watoto), sh. 2,000 (viti vya kijani na bluu), sh. 3,000 (viti vya rangi ya chungwa), sh. 5,000 (VIP C na B) na sh. 10,000 kwa VIP A.
Watoto waliokata tiketi kuingia uwanja ni 634, viti vya rangi ya kijani na bluu 13,238, viti vya rangi ya chungwa 1,040, VIP B na C 1,246 na VIP A watazamaji 176.
Vilevile Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawashukuru washabiki na wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine kufanikisha mechi hiyo kati ya Twiga Stars na Namibia.

KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA BAADA YA KUFANYIWA MATIBABU

KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA BAADA YA KUFANYIWA MATIBABU YA MGUU WAKE HUKO CHENNAI INDIA ,KAAMA ANAVYOONEKANA PICHANI AKIWA NA WAUGUZI WALIOKUWA WAKIMPATIA HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA MIOT INDIA.
KATIBU WA ORGANAIZESHENI WA CCM TAIFA BI ASHA ABDALLA JUMA AKIWA NA PROF MOHANDAS MKUU WA HOSPITALI HIYO YA MIOT NCHINI INDIA.

BASATA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI SASA KUDHIBITI UHARAMIA KWENYE SANAA


Na Mwandishi Wetu
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Jeshi la Polisi nchini wameunda kikosikazi maalum kitakachokuwa kikifuatilia uharamia na maovu mbalimbali katika shughuli za Sanaa na Burudani. 
Kikosikazi hicho kimeundwa baada ya Jeshi la Polisi nchini kutumia Sanaa shirikishi katika kutoa elimu kwa wadau wa Sanaa kuhusu dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya BASATA Ilala Sharif Shamba.
Akizungumza kuhusu kikosikazi hicho, Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa, BASATA Bi. Vivian Shalua alisema kuwa, kazi kubwa ya kikosi hiki itakuwa ni kufuatilia maonesho yasiyokuwa na vibali, uharamia kwenye kazi za wasanii na wasanii kutoka nje wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
Aliyataja majukumu mengine ya kikosikazi hicho kuwa ni pamoja na kudhibiti maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania, kusimamia utoaji vibali kwa wasanii wa kitanzania wanaoenda kufanya maonesho nje ya nchi na majukumu mengine yatakayojitokeza.
“Kikosikazi hiki kitakuwa tayari kufuatilia taarifa yoyote ya uharamia kwenye kazi za wasanii, maonesho yanayodhalilisha utu na maadili ya mtanzania na wasanii wanaoingia ndani ya nchi na kufanya maonesho bila vibali” alisisitiza Shalua. 
Kikosikazi hicho kinaundwa na Shani Kitogo (Afisa Utamaduni Ilala), Tatia Ramadhan (Polisi, TAZARA), Afande Jeremiah (Polisi Kati), Koplo Juma Mashauri (Polisi Airport), Michael Kagondela (Idara ya Utamaduni), Afande Deus Matoro (Reli) na Afande Swai (Traffic),
Wengine ni Vivian Shalua (BASATA), Jonathan Abel na Tatu Burhan (Uhamiaji), Deus Kessy (Polisi Reli), Koplo Josephat Syllively (Polisi – Maji), Masanja Nyalali (Polisi – Airport) na PC Mwakajaby (Polisi – TAZARA)
Akizungumza kwenye Jukwaa hilo la Sanaa, Asp Edson Kasekwa kutoka Polisi Makao Makuu Kitengo maalum cha Operesheni uzuiaji uhalifu,alisema kuwa, Jeshi la Polisi linawategemea wadau wa Sanaa wakiwemo wasanii katika kutoa taarifa juu ya matukio ya uharamia na uhalifu kwa ajili ya ufuatiliaji na udhibiti.
“Ni vema Wasanii na wadau wa Sanaa kwa ujumla wakaonesha ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa na kudhibiti uharamia na maovu kupitia sekta ya Sanaa. Hii ndiyo maana ya dhana hii ya polisi jamii na ulinzi shirikishi ya polisi kushirikiana na jamii” alisema Afande Kasekwa.
Kikosikazi hiki kimeundwa huku kukiwa na taarifa za uwepo wa vikundi mbalimbali vinavyofanya maonesho yenye kudhalilisha utu na maadili ya mtanzania huku uharamia kwenye kazi za Sanaa ukizidi kushika kasi.

MKUTANO WA CHADEMA WA KUZINDUA OPERATION HAMSHAPOPO KATA YA SINZA -

 Kamanda wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kata ya Sinza, Patodi Gwakisa (kushoto), akifuatilia kwa makini tukio hilo
Mkazi wa Dar es Salaam, akiinua juu Kadi yake ya Uanachama muda mfupi baada ya kujiunga juzi

SHULE YA MSINGI MGABE YAPATIWA MSAADA WA MADAWATI NA BENKI YA KCB WENYE THAMANI YA MILIONI 6 NA LAKI 5



Benki  ya KCB Tanzania imetoa ime kabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya shule kwa shule ya Msingi Mugabe,Sinza Maalum na Shule ya Uhuru mchanganyiko wenye thamani ya zaidi ya  sh. Milioni 18.4.
Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Dokta Edmund Mndolwa alitaja miongoni mwa vifaa hivyo ni madawati,vywakula ,vifaa vya michezo na vinginevyo.

Dkt.Mndolwa allisema  nsaada huo unaonesha ni kwa jinsi gani benki yake inazingatia wajibu wake wa kusaidia jamii inayoizunguka kupitia sekta ya elimu,afya ,mazingira na maafa mbalimbali ili kupunguza umasikini nchini.
Amewataka kutunza vifaa hivyo ili viweze kudumu kwani ni vya gharama na viweze kutumika na wanafunzi wengine kwa manufaa ya jamii nzima.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwafahamnisha kwamba Benki ya KCB inatoa huduma mbalimbali kwa wananchi 

wanoizunguka,tunaamini kuwa jamii inayotuzunguka nayo itatuunga mkono kwa kuchangamkia huduma zetu ambazo ni pamoja na kufungua akaunti,kuchukua mikopo ya nyumba na biashara”alisema .
Akizungumza kwa niaba ya wanajumuiya ya Mugabe shule ya Msingi, Mwalimu Mkuu  wa Shule hiyo ya Sinza Maalum Bw.Asafu Mahelele alisema  pamoja na msaada huo bado wanakabiliwa na changamoto ya vifaa vya kufundishia ikiwemo Vitabu vya Kiada, Uchakavu wa
Mapaa ya Majengo ya Shule na ubovu wa Miundombinu ya vyoo vya Walimu na Wanafunzi na kudai kuwa watayatunza ili yaweze kutumiwa kwa muda mrefu.
"Tunashukuru kwa msaada huu mdogo kutoka benki hii ya KCB,bado tuna changamoto nyingi zinazotukabili ikiwemo  ukosefu mkubwa wa vitabu vya kiada ,uchakavu wa mapaa ya majengo ya shule  yetu na ubovu wa miundombinu ya vyoo vya walimu na wanafunzi"alisema Bw.Mkiramwene.
KCB Tanzania ndiyo benki kongwe kuliko zote Afrika Mashariki ikiwa iliyoanza kuanzishwa Zanzibar mwaka 1896 na badae kusambaa Mombasa ,Nairobi, na kurudi nchini mwaka 1997.
Baadhi ya Walimu wa Mugabe, Wanafunzi pamoja na Wafanyakazi wa KCB Benki wakiwa kwenye Moja ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali, wanafunzi wa shule ya Mugabe na Maafisa wa Benki ya KCB katika picha ya pamoja.