Mkurugenzi Ufundi-Seleman Methew,(kati) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Taasisi ya Liverpool,mazungumzo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Idara Habari Maelezo leo,kushoto ni Katibu wa Liverpool, Ramadhan Kitunga, na Mwaasisi Hamiss Ahamed Gwatamu.
.............................................................................................
MASHABIKI wa klabu ya Liverpool waliopo hapa nchini wameandaa Tamasha la muziki wa taarabu litakaloitwa First Seven Morden Taarab, ambalo pia litajumuhisha michezo kama Mpira wa Miguu, ikiwa ni pamoja na kutembelea Hospital ya watu wa Moyo .
Akizungumza jijini Dar es SalaamMuda mfupi Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Selemani Methew amesema kuwa Liverpool Sports Family (LSF) ni taasisi iliyosajiliwa kisheria mnamo mwaka 2009 kwa msajili wa vyama vya Michezo kwa hati namba NSC:9168 SDDW.
na kuongeza kuwa pamoja na mambo mengine Malengo ya Liverpoool Sports Family ni kukuza Mahusiano ya Kidugu baina ya mashabiki wa klabu ya Liverpool waliopo hapa nchini sambamba na kukuza Maendeleo ya Michezo hapa kwetu Tanzania.
Aidha siku ya jumapili tasisi hii imepanga kuwa na mkutano wa wana (LSF)
uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa Meeda kuanzia saa saba mchana ambapo ametoa wito kwa Makampuni mbalimbali kujitokeza kuunga mkono ikiwa ni pamoja na kuwakaribisha wapenzi wa timu nyingine za nje waliopo kufika kwa lengo la kujfunza ili kwa pamoja waweze kuwa na mshikamano katika kukuza michezo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment