Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi na watendaji wa Wizara ya
nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,katika ukumbi
wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar jana,katika utekelezaji wa kazi za
Wizra hiyo.(Picha na Ramadhan Othman Ikulu.) 02/02/2012
Watendaji wa Wizara ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Ikulu,wakiwa katika kikao cha siku moja cha
utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo, chini ya Mwenyekti wake Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,
jana Ikulu Mjini Zanzibar.(Picha na Ramadhan Othman IKulu)
Makamu
wa rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalum, kuhusu ufugaji wa Kuku wa
mayai, wakati alipotembelea na kuweka Jiwe la msingi katika kituo cha
Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa
Pwani, leo Januari 02, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa
Pwani.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akitembelea na kukagua mabanda ya kufugia kuku katika kituo
hicho cha Shamba la Kuku kilichopo Kijiji cha Mkiu Wilaya ya Mkuranga
akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani, leo Januari 02, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la mradi wa Ujenzi
wa Kituo cha mnada wa Ng’ombe katika Kijiji cha Mkiu Wilaya ya
Mkuranga, wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Pwani leo, Januari
02, 2012.
A
round of applause rings after President Jakaya Mrisho Kikwete has
officially launched the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania)
yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam. Others
from left are the High Commissioner of South Africa to Tanzania, Mr
Thanduyise Henry Chiliza, the CEO of FirstRand, Mr Sizwe Nxasana and the
Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Ms Elizabeth
Nyambibo. (Photo by State House)
NA: ASHURA MOHAMED-ARUSHA
Katika
harakati za kuhakikisha kuwa kunakuwepo na taarifa sahihi pamoja na
takwimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa
tafiti na utunzaji wa kumbukumbu serikali kupitia wizara ya maendeleo ya
jamii jinsia na watoto imewakutanisha wadau mbalimbali katika warsha
kuhusu uanzishwaji wa kituo cha kitaifa cha utafiti na kumbukumbu za
wanawake katika eneo la tengeru wilaya ya arumeru mkoani Arusha.
Akifungua warsha hiyo naibu katibu mkuu wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia
na watoto Anna .T.Maembe amesema kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho
kutaiwezesha serikali kuwa na takwimu za kitaifa juu ya unyanyasaji wa
kijinsia hivyo itarahisisha utatuzi wa changamoto hizo kwa kuwa watakuwa
bna takwimu sahihi.
Anna
amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa vituo vya kitaifa ni kushirikiana
na kituo cha kanda katika kufanya tafiti mbalimbali,kuimarisha
mahusiano,kubadilisha uzoefu ,kutunza kumbukumbu na kupashana habai
zinazohusu haki za wanawake na usawa wa kijinsia.
Aidha amesema kuwa vituo hivi vitahamasisha
wadau mbalimbali kuhusu usawa wa kijinsia,ulinzi na kuheshimu haki za
wanawake lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili waweze
kufanya tafiti wa masuala ya yanayohusiana na usawa wa kijinsia na
kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki kikamilifu na wanachangia kuleta
maendeleo endelevu katika nchi wananchama hasa ziliathirika na vita.
Pia
amefafanua kuwamadhumuni ya warsha hiyo ni kuwapatia taarifa juu ya
uwepo wa kituo cha kanda kilichopo katika chuo cha ustawi wa jamii
Tengeru kuwa ndicho kilichochaguliwa hapa nchini,kubadilishana uzoefu na
kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kakufanikisha shughuli zitazofanywa
nakituo cha utafitina kumbukumbu za wanawake.
Naye
mwakilishi kutoka shirika la UNESCO Modester Munira amesema kuwa kwa
kutambua umuhimu wa kutunza nyaraka tume ya taifa unesco iliona ni vyema
kikaanzishwa kwa kituo hicho kwa kushirikiana na wizara ya maendeleo ya
jamii jinsia na watoto hivyo amatakataarifa zitolewe kwa uwazi zaidi.
Na Lydia Churi, MAELEZO, Dodoma
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali inakubali kuwa wastaafu kupewa mkataba wa kuendelea kufanya kazi si sahihi na kuahidi kuwa suala hilo litafanyiwa kazi.
Akifanya
majumuisho wakati wa mjadala wa Azimio la kuridhia mkataba wa vijana wa
Afrika (The African Youth Charter) waziri Nchimbi alisema hatua ya
wastaafu kupewa mikataba ya kuendelea na kazi inawanyima vijana haki ya
kupata ajira katika taasisi mbalimbali.
Akizungumzia
suala la maadili kwa vijana Mheshimiwa Nchimbi alisema hivi sasa vijana
wakiwemo baadhi ya viongozi wanaotoa michango yao juu ya mambo
mbalimbali katika mitandao kama vile facebook na twitter wanatumia lugha
zisizojenga na badala yake aliwataka kutoa michango isiyokuwa na
madhara kwa vijana wa taifa hili hasa ile inayotumia lugha zinazojenga
ili kulinda maadili ya Mtanzania.
Aliwataka
viongozi kuwa wa kwanza kupiga vita matumizi mabaya ya mitandao na
kuacha tabia za kulipiza visasi pale wanapokosana na wenzao kwani hizo
si sifa za kiongozi bora. “kiongozi bora na imara ni yule mwenye tabia
ya kusamehe, alisema”.
Kuhusu
mchakato wa kutafuta vazi la taifa waziri huyo alisema wizara yake
inatekeleza maagizo yaliyotolewa na bunge na kuwaomba wabunge kuwa wa
kwanza kuunga mkono wizara ya habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
inapotekeleza maagizo hayo. Aliongeza kuwa kamati iliyoteuliwa kutafuta
vazi la taifa ni makini kwa kuwa imeundwa na watu makini waliotoka
kwenye kada mbalimbali.
Awali
akichangia mjadala huo, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM) Peter Serukamba
alisema suala la wastaafu kupewa mkataba wa kuendelea na kazi halifai
kwa kuwa linawanyima vijana haki yao ya kupata ajira. Alitoa mfano kuwa
hivi sasa wenyeviti wa bodi wengi ni wastaafu ambapo ilipaswa nafasi
hizo kuchukuliwa na vijana.
Alisema
suala la uzoefu kuwa miongoni mwa sifa za kupata ajira si haki kwa kuwa
linawanyima vijana nafasi ya kupata ajira hizo. Alisema vijana wawapo
vyuoni hupatiwa muda wa kufanya mazoezi ya kazi na hivyo kuwa na uzoefu
wa kutosha.
Bunge
limeridhia mkataba wa kimataifa wa vijana isipokuwa limeridhia kwa
stara ibara mbili zinazohusu sera ya taifa ya vijana na suala la vijana
wa kike wanaopata ujauzito au kuolewa kabla ya kumaliza elimu zao kupewa
fursa ya kuendelea na masomo.
Bunge
limeridhia kwa stara ibara hizo kwa kuwa Sera ya Taifa ya Vijana kwa
taratibu za nchi yetu hupitishwa na baraza la mawaziri na sheria
hutungwa na bunge wakati mkataba unasema Sera itapitishwa na kukubaliwa
na bunge na kufanywa sheria.
No comments:
Post a Comment