NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA
IMEELEZWA
kuwa pamoja na nchi kukabiliwa na majanga na changamoto mbalimbali
hasa kwa mwaka 2011 wakristo hawapaswi kukata tamaa juu ya changamoto
hizo bali wanatakiwa kuangalia imani na mahitaji ya Mungu Kwa mwanadamu
ili aweze kupunguza na kuondoa changamoto hizo.
Hayo yameelezwa mjini hapa na mchungaji Simion Vomo wakati akiongea na waumini wa kanisa la T.A.G Christian All Nation Church lilopo katika manispaa ya mji wa arusha mapema wiki hii.
Aidha
mchungaji Vomo alisema kuwa katika mwaka 2011 mambo mengi sana
yalijitokeza hali ambayo iliwapelekea baadhi ya waumini kukata tamaa
lakini katika mwaka huu mpya wa 2012 wanapaswa kumuangalia mungu zaidi
kuliko matatizo yao binasi.
Alibainisha
kuwa hata katika matatizo mungu yupo na kwa hali hiyo kila mwanadamu
anapaswa kuangalia mpango na mikakati mbalimbali ya mungu na kuachana na
tabia ya kuona wameshindwa mbele ya Macho ya wanadamu
Awali
alisema kuwa nao waliofanikiwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatangaza
zaidi utukufu wa mungu kuliko mafanikio yao kwa kuwa ndicho chanzo
pekee cha kufanikiwa katika maitaji mbalimbali ambayo yanamzunguka
mwanadamu wa leo.
Alibainisha
kuwa endapo kama wataweza kufanya hivyo ni wazi kuwa mafanikio
yatakuwa ni makubwa sana ukilinganisha na mafanikio ambayo hayana
utukufu wowote hapa duniani.
Alimalizia
kwa kusema kuwa kwa wale ambao hawajafanikiwa kwa msimu wa mwaka
uliopita wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaongeza kiwango cha imani katika
maisha yao kwa kuwa Pia Mungu anapenda na kuthamini zaidi Mtu mwenye
Imani.
No comments:
Post a Comment