WASANII
wa muziki wa kizazi kipya na dansi Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, Herry
Samir ‘Mr Blu’, wakiwa na kundi la Mapacha Watatu ambalo linaongozwa
na Khaleed Chuma ‘Chokoraa’, Junior Kalala ‘Kalala Junior’, na Joseph
Michael ‘Jose Mara’, na kundi la muziki wa mwambao la Super Shine,
usiku wa kuamkia leo wamefanya kufuru ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar
Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam. Wanamuziki hao walivunja
rekodi ya mashabiki wengi waliowahi kushuhudia makamuzi kama hayo
katika kituo hicho cha burudani nchini.
Shoo
hiyo pia ilisindikizwa na makundi mengine kama Wakali Dancers, na
wasaniii wengine wa Bongo Fleva wakiwemo Zuhura na Dogo Mfaume na
Hejos Band. Watoto wakiserebuka ukumbini.
No comments:
Post a Comment