Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania(TWIGA STARS) Jana imefanikiwa kuifunga Timu ya Namibia kwa jumla ya magoli 5-2 katika mchezo wa Kimataifa Kufuvu fainali za Afrika uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao
ya Twiga yalifungwa na Mwanahamisi Omar katika dakika 21, Asha Rashid
'Mwalala', bao la pili dakika 46, bao la tatu Etoe Mlenzi, dakika ya
84, Asha Rashid,bao la nne dakika ya 88, na bao la tano, likifungwa tena
na Mwanahamis, dakika ya 90. Mabao ya Namibia mawili ya yamefungwa na
Beki wa Twiga, Etoe, aliyejifunga dakika ya 29 na bao la pili
likifungwa na Juliana Skrywer, dakika 73.
Kwa
matokeo hayo sasa Twiga Stars inatarajia kukutana na mshindi kati ya
Misri au Ethiopia ambapo Misri ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-2 dhidi ya
Ethiopia.
Twiga
iliwakilishwa na Fatuma Omary, Fatuma Bashiri, Pulkaria Charaji, Fatuma
Khatibu, Sophia Mwasikili, Mwapewa Mtumwa, Mwanahamisi Omari, Etoo
Mlezi, Fatuma Mstafa, Asha Rashid,Fadhila Hamad, na wachezaji wa Akiba
walikuwa ni Maimuna Saidi, Mwajuma Abdallah, Siajabu Hassan, Aziza
Mwadini, Zena Khamis, Semen Abeid, Rukia Khamisi na Mwanaidi Khamis.
Namibia
iliwakilishwa na Susanna Eises, Uerikondjera Kasaona, Lovisa Mulunga,
Esther Amukwaya, Stacey Naris, Alberta Dakies, Shirley Cloete, Lethicia
Manga, Thomalina Adams, Elmarie Fredericks, Lydia Eixas na wachezaji wa
Akiba ni Novata Paulus, Veweziwd Kotjipati, Mangulukeni Hamata, Mariana
Gaebusi, Lena Noreses, Lonaine Jossob na Juliana Skrywer.
Mchezaji
wa timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Twiga Stars Asha Rashid
akimtoka beki wa timu ya taifa ya Namibia ya wanawakeLovisa Mulunga,
katika mchezo wa kuwania fainali za kombe la dunia kwa wanawake
unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,
Wachezaji
wa Twiga Stars wakishagilia mara baada ya mchezaji wa timu hiyo Asha
Rashid kufunga goli la pili katika kipindi cha pili.
Mchezaji
Mwanahamisi Omari a.k.a Gaucho akihojiwa na mwandishi wa habari wa BBC
Eric David Nampesya baada ya kumalizika kwa mpira kati ya Twiga Stars na
Namibia , Mwanahamis
Omari 'Gaucho' ni mfungaji pekee wa mabao 2 kati ya 5 ya Twiga,
katika mchezo wa kutafuta kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake,
zinazotarajia kufanyika mwezi Juni mwaka huu. (Na: Mwandishi Wetu).
No comments:
Post a Comment