Pambano
la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa
Februari Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh.
40,191,000.
Jumla
ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 105 kwa
kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A
walikuwa 11,860.
Baada
ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu ilipata sh. 7,023,171, uwanja sh.
2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
936,423, TFF sh. 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)
sh. 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 234,106.
Nayo
mechi namba 104 kati ya African Lyon na Polisi Dodoma iliyochezwa
Februari Mosi mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es
Salaam imeingiza sh. 45,000 kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo.
Baada
ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni sh. 6,864.41 kila timu ilipata
sh. 2,591, Uwanja sh. 514, TFF sh. 514, DRFA sh. 205, FDF sh. 257 na
BMT sh. 51.
No comments:
Post a Comment