Wateja kupiga simu kwa robo shilingi. Kutuma SMS kwa 25/-
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza promosheni ya aina yake
ya punguzo la gharama za simu kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa maneno-
SMS itakayowahusisha wateja wa kampuni hiyo ambao sasa watapiga simu
kwa gharama ya ROBO SHILINGI kwa sekunde.
Promosheni hiyo ya siku saba kuanzia Jumatatu Januari 30, 2012
inahusu kupiga simu za ndani ya mtandao wa Vodacom yaani kupiga Vodacom
kwenda Vodacom kati ya Saa nne usiku na saa moja asubuhi kila siku kwa
wateja wote wa malipo ya kabla
Aidha sanjari na ofa hiyo kamambe Vodacom imetoa pia punguzo la gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno hadi shilingi 25/-
kwa ujumbe wakati wote wa siku kwenda mtandao wowote wa simu ya mkononi
nchini kwa kipindi cha siku saba nayo pia kuanzia leo Jumatau Januari
30, 2012.
Akitangaza
promosheni hizo mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza
amesema ni imani yake kwamba katika kipindi chote cha siku saba cha
promosheni hiyo wateja watafurahia kwa kufanikishiwa mawasiliano ya
biashara, familia, kazi na mengineyo kwa gharama nafuu zaidi.
“Wateja
wa Vodacom wakati wote wanafurahia huduma bora, nzuri na zenye kukidhi
mahitaji halisi, ni wazi kipindi hiki cha siku saba cha promosheni hii
ya punguzo la gharama za upigaji wa simu na utumaji SMS kitawapatia
wakati mwengine bora wa kufurahia kuwa wateja wa kampuni inayoongoza
soko”Alisema Bw. Rene.
Promosoheni hii inakwenda sawa na azma ya Vodacom ya kutoa fursa ya watanzania kuunganishwa kimawasiliano na kubadili maisha.
Ili mteja wa Vodacom aweze kufurahia promoheni hii ya punguzo la gharama za mawasiliano anapaswa kwanza kujiunga kwa kupiga *100# na kuanzia hapo atakuwa na uwezo wa kufurahia mawasiliano nafuu zaidi nchini miongoni mwa mitandaso ya simu za mkononi.
“Ni
fursa nzuri kwa wateja wetu, tunawaomba waitumie ikiwa ya kiwango cha
chini zaidi kuwahi kutokea katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi
nchini na Vodacom itaendeleza utamaduni wa kuwa kinara wa kubuni na
kuleta sokoni promosheni pamoja na huduma zenye thamani na mantiki
halisi ya wateja wetu na jamii nzima nchini.” Aliongeza Bw. Rene
Rene
aliongeza kwa kusema “Tunapoangalia katika utaratibu wetu wa kawaida wa
mfumo wa maisha tanagundua kuwa muda wa kati ya saa nne usiku na saa
moja asubuhi ndio wanafamilia hukaa pamoja na kufanya mawasiliano yenye
lengo la kupashana habari za familia na hata kazi na biashara baada ya
majukumu ya kutwa nzima au kabla ya kuanza siku mpya, hivyo ni imani
yetu tumewapa wateja kitu chenye thamani na kinachoweza kutumika vema na kumnufaisha kila mteja.”Aliongeza
Vodacom
ikiwa na wateja zadi ya milioni kumi nchini ni wazi promosheni ya aina
hii itatoa faida kubwa kwa jamii kwa kuwawezesha kutumia sehemu ya
punguzo la gharama ambazo wangengia kupiga na kutuma ujumbe mfupi wa
maneno kuelekeza sasa fungu hilo katika matumizi ya mahitaji mengine
No comments:
Post a Comment