Kwa upande mwingine
Chama Cha Mapinduzi kinapenda kurudia wito kilioutoa juu ya swala la
posho za wabunge. CCM iliwaomba na kuwasihi wabunge na mamlaka
zinazohusika na mchakato wa swala hili kuliangalia upya na kutumia
busara, ikiwezekana kuachana nalo kwasasa.
CCM inaupongeza na kuunga mkono msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kama ulivyonukuliwa na taarifa ya
Ikulu kwa vyombo vya habari, kuwa ni vizuri wabunge wakalitafakari upya
swala hili kwa masilahi mapana ya wale waliowapa dhamana ya
kuwawakilisha bungeni.
CCM inaendelea kuwasihi waheshimiwa wabunge walitafakari upya swala hili
na busara itumike katika kuliamua huku wakifungua masikio kusikiliza
sauti za Watanzania kwani huko bungeni wana wawakilisha hawa
Watanzania, ni vizuri kusikiliza hiki kilio chao! Si busara kupuuza
kilio cha waliokupa dhamana ya kuwawakilisha.
Msimamo wa Rais Kikwete kama sehemu moja ya mamlaka inayohusika na
mchakato huo ni uthibitisho wa usikivu wake kwa wananchi anaowaoongoza,
yeye katimiza wajibu wake, tunawasihi waheshimiwa wabunge wetu nao
walitafakari hili na kuona busara ya kuachana nalo kwasasa.
Kwa
muda sasa nchi yetu imepitia kwenye tatizo kubwa la mgomo wa madaktari
katika hospitali nyingi hasa za umma ambao kwa kiasi kikubwa mgomo huo
umekuwa na madhara makubwa kwa watanzania masikini ambao ni wengi,
kiasi cha kugharimu hata maisha yao.
Chama Cha Mapinduzi kinachukua nafasi
hii kuwapa pole sana wale wote walioathiriwa kwa namna moja ama
nyingine na mgomo huu. Na kwakweli tunasikitishwa sana na hali
inayoendelea! Chama Cha
Mapinduzi kinawapongeza na kuwashukuru madakitari walioonyesha
ubinadamu na uzalendo kwa kuamua kurudi kazini na ambao hawakugoma
kabisa.
Tunawashukuru na kuwapongeza kwani hakuna masilahi yanayovuka thamani
ya uhai wa binadamu mwenzako!
Tunachukua fursa hii pia kuwashukuru sana na kuwapongeza askari wetu wa
jeshi la wananchi wa Tanzania kwa uamuzi wao wa kizalendo wa kuamua
kuitikia wito wa serikali kwenda kwenye baadhi ya hospitali kusadia
kuwatibu watanzania wenzao. Moyo huu ni wa kizalendo na wa mfano.
Tunajivunia uzalendo wa jeshi letu!
Tunachukua nafasi hii kuwaomba
madaktari wanaoendelea na mgomo kurudi kazini huku wakiendelea na
mazungumzo na serikali. Tunaamini madai yao yanawezekana kushughulikiwa
ikiwa pande zote mbili zitaamua kukaa chini kwa dhati na kuzungumza.
Serikali kwa upande mmoja watafute kwa makini chanzo cha mgogoro huu na
kutafuta majibu, na madakitari nao kwa upande wa pili, wawe tayari
kukaa mezani na kuzungumza.
Tunasisitiza thamani ya maisha ya binadamu ni kubwa kuliko masilahi na
madai wanayoyaomba!
Serikali ni vizuri ikajenga utamaduni wa kushughulikia matatizo haya
ambayo yanaathiri wananchi wengi kwa uharaka na udharura unaostahili
badala ya kusubiri hali inapokuwa mbaya zaidi.
ACP Kashai akikagua kikosi cha kupambana na majambazi kwa kutumia piki piki
Na Pardon Mbwate Mwandishi wa Jeshi la Polisi- kigoma
Askari wa mapokezi katika vituo vya Polisi hapa nchini, wametakiwa kuwa
kioo cha Jeshi hilo kwa kuonyesha ukarimu na kauri nzuri
wanapowahudumia wananchi wanaofika kwenye vituo hivyo ama wanapoombwa
msaada mahala popote wanapoombwa kufanya hivyo.
ACP
Frasser Kashai amesema hatua hiyo italiwezesha Jeshi hilo kuendelea
kujenga heshma mbele ya Jamii wanayoihudumia na taifa kwa ujumla.
Akizungukia
na Askari polisi, wakuu wa idala mbali mbali za polisi posti,
Kamanda Kashai amesema dhamira ya Jeshi hilo ni kutaka kila askari
kubadilika na kutoa huduma bora kwa wananchi. na kuwa makini katika
utendaji wao wa kazi za kila siku kutoa huduma kwa mteja iliyo bora
Kamanda
Kashai amesema hayo akiwa anakagua paledi ukaguzi huo uliofanyika na
maafisa wake Kihenya Kihenya SSP na RCO Josephu Konyo SSP OCD Wilaya
kigoma Jafeti Kibona D/SSGT Silvanusi Mazengo D/SSGT Deusidedith Magogo
D/SGT Menas Temba ukaguzi huo uliowahusisha askari wa vikosi vyote pia
ukaguzi huo ni pamoja na kesi wanazo peleleza na kutaka kujua wapi zimefikia na kuona hatua walizo chukua mazingila
utabadili mwelekeo wa kiutendaji wakimazoea bali kuboresha huduma kwa
jamii.kumarisha wawapo vituoni mwao na kuwafanya wananchi kuona kuwa
vituo vya Polsi ni kimbilio la watafuta haki.
Amesema
Kamanda Kashai jukumu la kuwafundisha askari ni la kila Afisa wa
polisi, il askari wawe waadifu katika utendaji kazi wao na kuwaudumia
wananchi wanapokwenda katika kituo cha Polisi anatarajiwa kupata huduma
anayoitegemea na kwamba kama atakuwa na tatizo anaamini atapata
mapokezi mazuri na kutatuliwa tatizo lake.
Kamanda
Kashai amesema kutokana na mabadiliko ya mifumo ya Majeshi ya Polisi
Duniani Kote, Polisi anatakiwa kumuona Raia kama sehemu ya Polisi kwani
ni Raia huyo huyo atalazimika kutoa taarifa za wahalifu Polisi na hivyo
kurahisisha utendaji wa Jeshi zima.sambamba na hilo ataendelea
kufundisha askari kila juma tano ili kuwa na askari wazuri katika Mkoa
wa Kigoma amewataka askari wote kunza siri za watoa taarifa ili
kulifanya Taifa letu kuwa na amani iliyopo iendelee
Kamanda alisema kuwa washiiriki hao watalisaidia Jeshi la Polisi
katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi katika maeneo mbalimbali
hasa katika kila kata hadi tarafa kuendelea kufundisha polisi jamii
katika kila maeneo waoyopangiwa.
Mafunzo hayo yanayo tolewa mala moja kwa kila wiki moja yanawashirikisha Wakuu wa Vituo vya Polisi 18 na Askari 132 wa Vyumba vya Mashtaka kutoka vituo mbalimbali vya Polisi katika Wilaya zote tatu Kigoma mjini Kasulu,na Kibondo.
No comments:
Post a Comment