Mtihani
wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Machi 29 mwaka huu saa 10
kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Kutakuwa
na jumla ya maswali 20 kwenye mtihani huo, 15 yanatoka FIFA kuhusiana
na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF
kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
Kwa
ambao wangependa kufanya mtihani huo utakaokuwa katika lugha ya
Kiingereza wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za Marekani
ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambapo mtihani huo unalenga. Muda wa
kufanya mtihani hautazidi dakika 90.
Mtihani uliopita ulifanyika Septemba 29 mwaka jana ambapo watahiniwa wanane walijitokeza na kufanya mtihano huo.
Mpaka
sasa Tanzania ina mawakala saba wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA.
Mawakala hao ni Ally Mleh wa Manyara Sports Management, Damas Ndumbaro,
John Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said
Tully.
No comments:
Post a Comment