Na:- Marzuku Khamis Maelezo Pemba.
Wakulima
wa zao la Karafuu Kisiwani Pemba wametakiwa kutohifadhi Karafuu zao
Majumbani na badala yake waziopeleke katika vituo vya ununuzi vya
Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) kwa ajili ya kuziuza
badala ya kuzirundikiza Majumbani mwao kama inavyojitokeza hivi sasa
Wamesema
kufanya hivyo kutawaepushia na vitendo vya Wizi na pia kuweza kupata
uzito mkubwa wa Karafuu zao zitakazowapatia pato zuri zaidi
Wakuu
wa vituo mbali mbali vya ZSTC vya unuzi wa karafuu waliyasema hayo
wakati walipotembelewa na kamati ya kitaifa yakudhibiti zao la Karafuu
Zanzibar wakati walikpokuwa wakitembelea vituo mbali mbali vya ununuzi
wa karafuu pamoja na vikosi vya ulinzi wa zao hilo kisiwami Pemba.
Wamesema
kuwa ukweli hivi sasa Msimu wa Uchumaji wa Karafuu upo ukingoni
lakini kilichobainika kuwa bado Karafuu zimo Katika majumba mbali mbali
ya wakulima hivyo ni wajibu wa kila mkulima hivi hivi sasa kuzipeleka
kwenye vituo vya ZSTC kwa kuziuza jambo ambalo litakuwa ni faida kubwa
kwao na serikali kwa jumla.
Wakizungumzia
juu ya suala la malipo ya Wakulima wanaouza karafuu zao humo vituoni
wamesema kuwa hakuna hata Mkulima mmoja aneidai ZSTC na mtu yoyote
anaekwenda kuuza Karafuu zake mara tu baada yakuuza anapewa malipo yake
yote.
Aidha
wakuu hao wa vituo wamesema kuwa kwa ujumla kazi ya ununuzi wa Karafuu
imekwenda vizuri na mashirikiano kutoka kwa wauza karafuu pia yalikuwa
mazuri na makubwa na kutowa wito kwa Wakulima kuharakisha kuzipeleka
Karafuu zao Kuziuza hivi sasa Katika vituo vya ZSTC kwani wasije kupata
usumbufu pale ZSTC itakapoamuwa kupunguza vituo hivyo Vijijini na
kuvibakisha vituo vya Mijini.
Mkuu
wa Mkoa Kusini Unguja Mustafa Mohamed Ibrahim ambae ni mjumbe wa
kamati ya kitaifa ya kudhibiti zao la karafuu Zanzibar amesema kuwa
amefarajika sana na kazi nzuri inayoendelea kufanyika katika
utekelezaji wa kazi za ununuzi wa Karafuu na kuwataka Wakuu hao
kuendelea kutoa Mashirikiano kwa Wakulima wa zao la Karafuu kwa
kuwakumbusha kuzipeleka kuuza karafuu zao haraka kwenye vituo hivyo vya
ZSTC na kutozihifadhi majumbani.
Katika
ziara hiyo wajumbe wa kamati ya kudhibiti zao la Karafuu Zanzibar
ambayo ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kusini UngujaMustafa Mohamed Ibrahim
ilitembelea Ghala kuu la kuhifadhia karafuu lilioko Mkoani, Kituo cha
ununuzi wa Karafuu cha Kiwani,Chanjaani,Bwagamoyo,
Raha,Mgogoni,Kisiwani, Mtambile na Chumbageni Wambaa.
Pia Wajumbe wa kamati hiyo walitembelea kambi za Vikosi vya Kudhibiti Magendo vya Chaanjaani na Mkuumbuu.
No comments:
Post a Comment