Na.Ashura Mohamed -Arusha
Timu
ya mpira wa miguu ya Olduvai Kids iliyopo mkoani hapa imeibuka mshindi
katika fainali za kombe la kuhamasisha vijana kupima virusi vya ukimwi
kwa kuichapa timu ya kaloleni B Magoli 2-0 mechi iliyochezwa jana katika viwanja vya kumbukumbu vya sheikh Amri Abeid mjini arusha.
Akiongea
mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo mratibu wa tamasha hilo Samweli
Mpenzu amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwawezesha vijana kuwa
pamoja kupitia michezo pamoja na kutambua afya kwa kuwa michezo ni afya
ili kijana anapogundulika kuwa na virusi vya ukumwi basi aweze kufuata
ushauri nasaha.
Mpenzu
amesema kuwa kupitia tamasha hilo vijana wameweza kuwa pamoja kupitia
michezo hiyo pia wamepata fursa nyingine ya kupima virusi vya ukimwi ili
kujua afya zao na jinsi ya kujikinga ambapo huduma hiyo pia ilikuwa
inapatikana katika viwanja hivyo.
Pia
amewashukuru vijana wote waliojitokeza pamoja na timu zote kumi kwa
kuwa bila wao tamasha hilo lisingekuwa na ushindani ambapo amesema
tamasha hilo pia litafanyika tena mwezi wa pili ambapo safari hii
itakuwa ni upande wa wanawake.
Naye
mgeni rasmi katika tamasha hilo katibu wa chama cha mpira wa miguu
wilaya ya Arusha Zakayo Mjema amesema kuwa tamasha hilo liliandaliwa na
YES Tanzania pamoja Tackle Afrika ambapo amewataka wadhamini hao kufanya
liwe endelevu.
Mjema
amesema kupitia nafasi yake wapo tayari kushirikiana na wadau wa
michezo mkoani hapa ili kuwafanya vijana kuwa bise kuliko kukaa bila
shughuli maalum ya kufanya pamoja na kuinua soka la mkoa wa Arusha.
Mshindi
wa pili katika tamasha hilo ni timu ya Kaloleni B,mshindi wa tatu ni
timu ya Intersports na timu zilizoshiriki ni CIDT,Younglife,Caroline
Ranges,Arusha Talent, na Young Kids ambapo mshindi wa kwanza aliondoka
na kombe na timu zote zilipata hati ya ushiriki.
No comments:
Post a Comment