TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, August 20, 2013

PEPSI MAYOR'S GUMZO JIJINI MWANZA- PEPSI YAPONGEZWA NA WAKAZI WA MKOA HUO

Balozi wa PEPSI TANZANIA- Juma Kaseja, Muda mfupi baada ya kuwasili jijini Mwanza kushuhudia Fainali hizo za Kwanza za Kombe la Pepsi Mayor's Cup. wengine ni wafanyakazi wa kampuni hiyo. 
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).
 Mfungaji Bora wa Michuano ya Pepsi Mayor's Cup, Godfrey Gerald, akionyesha Zawadi ya Tuzo ya Dhahabu.
 Vijana wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu(Soka) Timu zilizoshiriki michuano hiyo, wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Baadhi ya Wachezaji wa Timu katika Michuano hiyo, wakijiandikisha majina yao kabla ya kuingia uwanjani
 Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu(Soka) Timu zilizoshiriki michuano hiyo, wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Baadhi ya Timu Shiriki
 Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu(Soka) Polisi, Timu zilizoshiriki michuano hiyo, wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu(Soka) Timu zilizoshiriki michuano hiyo, wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Mayor wa Nyamagana Mwanza, Stanlaus Mabula wa Pili Kulia, akionyesha Moja ya Zawadi za Wadhamini wa Fainali hizo
  Wachezaji wa Timu za Mpira wa Miguu(Soka) Timu zilizoshiriki michuano hiyo, wakifuatilia kwa Makini Semina ya Mafunzo kutoka kwa wakufunzi wa DUME- kuhusiana na Matumizi bora ya kutumia Kinga(DUME Kondom) wakati wa Tendo la Ndoa(Ngono Salama).
 Wapenzi na Mashabiki wa Timu ya Bingwa wa Fainali hizo, ISAMILO, wakiwasili kwenye Uwanja huo

MFALME WA NYIMBO ZA ASILI TANZANIA, COSTA SIBOKA APAGAWISHA WATALII JIJINI DAR ES SALAAM.

 Mfalme Siboka akiongoza kucheza ngoma katika Hafla hiyo.
 Kundi jipya la Ngoma za asili la Mfalme Costa Siboka(MFALME GROUP)
 Costa Siboka, akijaribu kuonyesha kwa Vitendo, wakati mmoja wa Watalii wa Kigeni aliposhindwa kijizuia na kuingia kucheza ngoma ya Twisile ya kabila la wanyakyusa.
Mfalme wa nyimbo za Asili Tanzania, Costa Siboka, akipagawisha Wazungu waliofurika katika Ukumbi wa Golden Jubilee, wakati wa Onyesho la Kutafuta Warembo wa Miss Ilala Tanzania 2013
.(Picha kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Matukio katika Picha na taswira yetu kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015

 Halii ni hatari sana na ni chanzo cha ajali za barabarani, Baadhi ya wafanyabiashara wakitoka kufanya biashara za Mitumba katika Vijiji vya Mkoa wa Shinyanga
 Pamoja na Ahadi nyingi kutoka kwa viongozi wetu, ususani wakati wa kuomba kura wakati wa Uchaguzi, tatizo kubwa linazidi kuwa Maji  kwenye maeneo mengi ya Vijiji, Vijana wakichota maji kwa ajili ya matumizi ya kila siku katika vijiji vya mkoa wa Tabora.
 Ajali nyingi usababishwa na ukaidi ama uzembe wa Madereva, pichani baadhi ya wafanya biashara wa Vijiji vya Mkoa wa Shinyanga wakitoka katika biashara zao za Mitumba Gulioni(MNADA)
 Baada ya Kumalizika Ujenzi wa Barabara ya Mkoa Shinyanga kwenda Mwanza, Hali si shwari kwa Watumiaji wa Barabara hiyo ususani Madereva wa Magari Makubwa yakiwemo Mabasi ya Abiria, Tatizo la Uchakachuaji ni chanzo kinachosadikiwa kuifanya Barabara hiyo kutokuwa bora na ya Ufanisi.
 Wakati Mwingine Magari ya Abiria mabasi upata ajali kutokana na kwenda Safari zao kwa Mashindano, kama walivyoonekana Madereva wa Barabara itokayo Singida kwenda Tabora.
 Wakati Tanzania ikielekea Uchaguzi Mkuu wa Viongozi  2015, Vijana nwengi wameendelea kukumbwa na Tatizo la Ajira, pamoja na ahadi nyingi kutoka kwa Viongozi Maisha Bora kwa Kila Mtanzania.
 Tatizo la Vijana wengi kutoka Vijijini kukimbia mijini linazidi kuongezeka, hiyo ikitokana na uwepo wa Maisha magumu Vijijini, ambapo wameamua kwenda Mijini ili kufanya Biashara na kuwaacha sasa Watoto wadogo wakiendelea kujikongoja na aina mbali mbali za Biashara, kitendo kinachozidi kudidimiza Elimu ya Tanzania( kwa watoto kujiingiza katika soko la Biashara na kukimbia Masomo Darasani).
 Maisha ya Kina mama wakazi wa vijiji inazidi kuwa tete, ambapo sasa kina mama wamejitokeza kwa wingi kuingia katika soko la kujiajiri na hivyo kusahau hali ya kuendeleza kilimo bora, Maisha ambayo yamesababishwa na udanganyifu wa Viongozi wao wakati wa kuomba kura ili wachaguliwe.
  Maisha ya Kina mama wakazi wa vijiji inazidi kuwa tete, ambapo sasa kina mama wanazidi kuangaikia maji, Maisha ambayo yamesababishwa na udanganyifu wa Viongozi wao wakati wa kuomba kura ili wachaguliwe.
 Maslahi ya Wakulima wa Pamba katika Mkoa wa Shinyanga inazidi kulalamikiwa , ambapo serikali inatakiwa kuingilia kati na kuboresha hali hiyo.ambapo wanaofaidika ni wale wafanyabiashara kubwa ya Pamba kuliko wale wadogo.
Ajali nyingi zinazidi kutokea kutokana na Madereva wengi kutotimia ama kufuata masharti ya barabarani, huku tatizo la usafiri pia likizidi kuvikumba vijiji mbalimbali nchini Tanzania ususani kutoka katika Mikoa kwenda kwenye Vijiji. kama walivyokutwa wakazi hawa wa Mkoa wa Shinyanga.
(Picha Zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania).

Thursday, August 15, 2013

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WAFURIKA KUSIKILIZA MKUTANO WA CHADEMA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA


Huu ni mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, katika uwanja wa FURAHISHA, kirumba Mwanza, katika kuzungumzia na kukusanya maoni ya katiba Mpya zoezi linaloendelea kwenye maeneo mbalimbali ya majimbo ya Tanzania. 
(Picha zote kwa Hissani ya Miss Demokrasia Tanzania)

Monday, August 12, 2013

MATUKIO MBALI MBALI TANZANIA KUHUSU BARABARA NA MAZINGIRA .


Ajali za Madereva wa Pikipiki(Bodaboda)  Barabarani Zinaongezeka  kila kukicha kutokana na Madereva wengi wa pikipiki kuwa na mafunzo ya Muda Mrefu, Kijana Jumanne juma, ambaye hayupo pichani muda mfupi baada ya kunusurika na kuikimbia pikipiki katikati ya barabara kitendo ambacho pia ni chanzo cha ajali.


Barabara kuelekea Iringa


Hii ndiyo Tanzania yetu unayosikia kila siku kuwa ina rutuba na rasilimali nyingi kutokana na ardhi yetu, lakini kwa sasa unaweza kujiuliza imeisaidia vipi jamii yake ya watanzania, lakini wakati ardhi kwa tanzania ikionekana kuwa siyo tatizo, ongezeko la vijana kukimbilia mijini limezidi kuongezeka na hivyo kujaza zaidi maeneo ya Mijini kuliko Vijijini, pamoja na kwamba wanaishi katika mazingira ya kukabiliwa na tatizo la ajira kwa watu wake zaidi ikiwa Vijana.

Wakati Tanzania inapata Uhuru, Mapambano makubwa kwa ardhi yake katika kutafuta maendeleo ilikuwa ni kupata barabara zitakazounganisha katika ya mji, mkoa na mkoa, watawala waliotangulia waliweza kuipigania zaidi na kwa kutumia umoja wao katika kufanya vitu vya msingi ikiwa ni pamoja na kufanya barabara kati ya mikoa ya iringa na morogoro inapitika kwa urahisi, lakini changamoto kubwa waliyokutana nayo ilikuwa Milima Mikubwa. je Ingekuwa ni wakati huu ufanyike ujenzi kama huu Tanzania ? Toa Maoni!!

Pamoja na Kwamba kuna Taadhali kubwa zimewekwa Barabarani lakini bado Madereva Wetu wanashindwa kuzingatia, je wanachukuliwa hatua zipi na Tanzania ama Wamiliki wa Barabara(TANRODS) wamenufaika vipi na watu hao, ni kati ya matatizo ambayo yameikumba Tanzania na hivyo kuzidi kutumia barabara zenye wembamba usiostahili kupunguza ajali za barabarani.

Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa ambayo imevuma na kusikika muda mrefu, hivyo ulitakiwa kuwa na maendeleo makubwa kwa kutumia ardhi na rasilimali walizonazo za nguvu kazi, Mkoa wa Iringa ni kati ya Mikoa yenye Baridi muda Mwingi, lakini je wakazi wa Mkoa huo wamenufaika vipi na Mkoa wao, ni vyanzo gani vya ajira ambavyo Mkoa umejiwekea katika kuwawezesha vijana kutokimbilia miji ya Mbeya na Dar es Salaam,

Miwa ni kati ya Mazao ambayo miaka ya nyuma ilikuwa si adimu kama wakati wa sasa, kutokana na kwamba wakazi wa zamani walikuwa wakithamini Mazao kama Kinga Muhimu kwao kwa Chakula, Tofauti na sasa watu wengi kinga imekuwa ni hela mbayo kama isipotafutwa uwezi kuwa na uhakika wa kuitunza familia kwa familia.

Mwendo kasi ni hatari kwa maana ni chanzo cha ajali za barabarani, na hata pia Matumizi Mazuri ya Barabara ni chanzo kizuri cha kuhepusha ajali, kuwa na tumia uhangalifu barabarani.

Sehemu nyingi za barabara chanzo kimojawapo cha ajali ni Kona, hivyo Madereva mnapaswa kuwa waangalifu zaidi sehemu zenye kona kali.Kona hii ni katika Milima Kitonga. Sehemu ambazo wakati wote Madereva wa Magari ya Abiria(BUS) upita wakiwa na zaidi ya spidi 70, kitendo ambacho ni hatari na ni chanzo kimojawapo cha ajali.

Gari la Mizigo likiwa limekatisha safari zake na kufunga nusu ya barabara, kitu ambacho ni hatari kwa madereva wasiyokuwa waaangalifu barabarani.

Viwanja Tatizo la Soka la Tanzania ama Soka na viwango kwa wachezaji ? ni kati ya maswali ambayo watu wengi kwa Tanzania wameendelea kujiuliza, zaidi ikiwa ni vijijini ambako sasa imekuwa kimya kusikiwa wakitokea wachezaji wenye kutumainiwa na Taifa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, lakini hata hivyo ikionyesha kutokuwa na mwamko kwa kizazi cha sasa katika michezo kutokana na wengi wa vijana kuwa na mawazo ya kutafuta pesa waweze kuishi, upungufu wa kufika katika viwanja vya wazi limeendea kuikumba Tanzania na hivyo kuifanya kuzidi kuwa na upungufu wa wachezaji wenye vipaji.

Moja ya taswira ya maeneo ya Mikoa ya Tanzania. nchi ambayo inasadikika kuwa na Demokrasia kubwa kuliko nchi ingine yeyote duniani, Ardhi ambayo mpaka sasa Bado imeendelea kuyanufaisha Mataifa kutoka nje, kutokana na kukosa wataalamu wa kutambua na kufanya uchunguzi wa Uwepo wa Baadhi ya Mazingira ambayo mara nyingi yamekuwa yakiibuliwa na wageni , ambao mpaka sasa wameendelea kumiminika katika kuomba kuwekeza.

Eneo hili ni Moja ya Maeneo ambayo wakandarasi , eneo hili baada ya mradi kumalizika kitakachofuata !!!

Tukumbuke kukata miti kisha kupanda miti!!


Kitakachofuata baada ya hapo unadhani ni nini, 
(Picha Zote kwa Hisani ya Miss Demokrasia Tanzania)