TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, January 18, 2014

SHULE ZA MSINGI JIMBONI TEMEKE KUTANUA NA MADAWATI 500 -MTEMVU

Madiwani wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kushoto)  kukata utepe  wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika Shule za msingi katika Kata 13 za jimbo hilo. Hafla hiyo imefanyika leo Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika shule zilizopo katika Kata 13 za Jimbo hilo. Madawati hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo yalikabidhiwa kwa madiwani wa Kata hizo katika hafla iliyofanyika Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam
Naibu Meya wa wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga akitoa shukurani kwa Mbunge Mtemvu kutoa madawati hayo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Zena Mgaya akimpongeza Mtemvu kwa juhudi za kuinua kiwango cha elimu wilayani Temeke.
Ofisa Elimu wa  Shule za Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba akieleze furaha ya kupata madawati hao 500 yatakayopunguza tatizo la madawati wilayani Temeke.
Mtemvu akiangalia wakati mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiandika jina lake.
Mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa shukurani kwa Mtemvu kwa  niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati hayo  
Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yalitotengenezwa VETA Chang’ombe

WITO KWA WAHESHIMIWA WABUNGE WOTE

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
images
WITO KWA WAHESHIMIWA WABUNGE WOTE
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawatangazia Waheshimiwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa wafike Jijini Dar es Salaam Jumapili tarehe 26 Januari 2014 kwa ajili ya shughuli za Kamati za Bunge zitakazoanza tarehe 27 Januari 2014 hadi tarehe 8 Februari 2014. Moja ya shughuli hizo ni pamoja na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Imetolewa na
Ofisi ya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa
Dar es Salaam
17 Januari 2014.

Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kuimarisha na Serikali ya Tanzania .

IMG_9491 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa. IMG_9566 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Tanzania itakavyonufaika na mfumo wa himaya moja ya forodha katika kuimarisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
IMG_9572
aziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya  Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) kupanua huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi, ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja ya hatua za kuimarisha usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole.
…………………………….
Na Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Nyanja za miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mh.Sitta alibainisha kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 Mawaziri wa Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana kujadili namna ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, reli, anga, anga na maji.
Mh.Sitta aliongeza kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) lipanue huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama hatua za awali za utekelezaji.
Mh. Sitta alisisitiza kuwa katika mkutano wa 8 wa Baraza la la Mawaziri la Jumuiya hiyo umeridhia mfumo wa himaya moja ya Forodha na mpangokazi unaoainisha masuala ya utekelezaji katika kipindi cha miezi sita ili kuwezesha kuanzishwa kwa himaya hiyo ifikapo Juni 2014.
Mh. Sitta akifafanua zaidi alisema mfumo wa himaya moja ya forodha unaainisha utaratibu wa mzunguko wa biashara, usimamizi wa mapato na mfumo wa kisheria.
Katika mfumo huo Sitta alisema kuwa ilikubalika kuwa nchi wanachama zitakusanya mapato yake ya kodi.
Aidha, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kuelekea nchi nyingine wanachama za Jumuiya hiyo zimekubaliana kuwa nchi husika itakusanya mapato yake na kuifahamisha mamlaka ya forodha mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa kwa ajili ya kuruhusu bidhaa kuondoshwa.
Mkutano wa 15 wa Kawida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Afrika Mashariki Uliofanyika Jijini Kampala, Uganda Novemba 30, 2013 na kuamua masula muhimu ya maendeleo ya Mkutano wa Jumuiya Afrika Mashariki.
Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kutolewa uamuzi ni pamoja na kutiwa saini kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha, kuidhinishwa uundwaji wa Himaya ya Umoja wa Forodha (Single Customs Territory).

PINDA AKAGUA ATHARI ZA MAFURIKO DODOMA

IMG_0133
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama  sehemu ya jengo  la Kituo cha Polisi cha kijiji cha Chipogoro  wilayani Mpwapwa ambayo imeporomoka kufuatia mafuriko  yaliyokikumba kijiji hicho  kufuatia mvua kubwa zianazoendelea  kunyesha mkoani Dodoma januari 17, 2014. Kulia kwake  ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0152
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko  yaliyokikumba kijiji cha  Chipogoro wilayani Mpwapwa Januari 17, 2014.  Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mpwapwa, Gregory Tewu  na kushoto kwa ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa,, Alfred Msovella. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0161
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko  yaliyokikumba kijiji cha  Chipogoro wilayani Mpwapwa Januari 17, 2014.  Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Mpwapwa, Gregory Tewu na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema Nchimbi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0174
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akikagua  daraja ambalo lilizibwa na  maporomoko ya maji yaliyoambatana na magogo , mawe na udongo na  kusababisha  mafuriko katika  kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa januari 17,20134. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0203 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua athari za mafuriko katika kijiji cha Fufu wilayani Chamwino, Dodoma, Januari 17, 2014.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema nchimbi na kulia kwake ni Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, January 17, 2014

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF


tff_LOGO1TFF YANOA MAKATIBU MABORESHO TAIFA STARS
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya siku mbili kwa makatibu wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa kuhusu maboresho ya timu ya Taifa (Taifa Stars).
Semina hiyo inafanyika ukumbi wa Singida Motel, mjini Singida kuanzia kesho (Januari 18 mwaka huu) ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kwa washiriki kuhusu maboresho hayo.
TFF imeandaa mpango wa maboresho kwa Taifa Stars ambapo pamoja na mambo mengine umepanga kusaka vipaji nchini nzima kwa lengo la kupanua wigo wa kupata wachezaji wanaoweza kuchezea timu hiyo.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiu Lager mwaka huu inakabiliwa na mechi za mchujo za Kombe la Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Morocco.
Mechi hizo za mchujo zitachezwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu ili kupata timu 16 zitakazofuzu kucheza fainali hizo.
WASOMALI KUCHEZESHA YANGA, WACOMORO
Shrikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Komorozine Sports ya Comoro.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mchujo itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu wakati ile ya marudiano itachezwa kisiwani Comoro kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Mwamuzi wa kati atakuwa Hassan Mohamed Hagi wakati wasaidizi wake ni Hamza Hagi Abdi, Bashir Abdi Suleiman na Bashir Olab Arab. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Eugene Musoke kutoka Uganda.
Timu ambazo zimeingia moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa ni Coton Sport ya Cameroon, El Ahly (Misri), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), El Hilal (Sudan), Club Sportif Sfaxien (Tunisia) na Esperance (Tunisia)
Nayo mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kati ya Azam ya Tanzania na Ferroviario Da Beira ya Msumbiji itakayofanyika Dar es Salaam kati ya Februari 7 na 9 mwaka huu itachezeshwa na waamuzi kutoka Sudan.
Waamuzi hao ni Mutaz Abdelbasit Khairalla atakayepuliza filimbi, Waleed Ahmed Ali, Aarif Hasab Elton na El Fatih Wadeed Khaleel. Kamishna wa mechi hiyo ni Hassan Mohamed Mohamed kutoka Somalia. Mechi ya marudiano itachezwa Msumbiji kati ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Timu zilizotinga moja kwa moja katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo ni Asec Mimosas ya Ivory Coast, Ismailia (Misri), Wadi Degla (Misri), Djoliba (Mali), MAS (Morocco), Bayelsa United (Nigeria), El Ahly Shandy (Sudan), E.S.S. (Tunisia), C.A.B. (Tunisia) na Zesco United (Zambia).
WATANZANIA KUCHEZESHA MECHI ZA CL, CC
Watanzania wanane wameteuliwa kuchezesha mechi mbili za marudiano za raundi ya awali za Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) na Kombe la Shirikisho (CC) zitakazochezwa wikiendi ya Februari 14 na 16 mwaka huu.
Waamuzi hao walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Israel Mujuni atakayechezesha mechi ya CL kati ya Rayon Sport ya Rwanda na AC Leopards de Dolisie ya Congo itakayofanyika jijini Kigali.
Mujuni atasaidiwa na Josephat Bulali, Samwel Mpenzu na Ramadhan Ibada, wakati Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Jean Marie Hicuburundi wa Burundi.
Naye Waziri Sheha ataongoza jopo lingine kwenye mechi ya CC kati ya FC MK ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na El Ahly Atbara ya Sudan. Mechi hiyo itachezwa jijini Kinshasa.
Sheha atasaidiwa na Ferdinand Chacha, John Kanyenye na Israel Mujuni. Kamishna wa mechi hiyo ni Chayu Kabalamula kutoka Zambia.
SEMINA YA KUPANDISHA MADARAJA WAAMUZI JAN 21
Semina kwa ajili ya kupandisha madaraja waamuzi itafanyika Januari 21 na 22 mwaka huu katika vituo vitatu vya Dodoma, Mwanza na Songea.
Waamuzi watakaoshiriki katika semina hizo ambazo pia zitahusisha mitihani ya utimamu wa mwili (physical fitness test) watajigharamia wenyewe na wanatakiwa kufika vituoni siku moja kabla. Waamuzi hao ni wa daraja la pili na tatu.
Kituo cha Dodoma kitahusisha waamuzi kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Pwani, Singida na Tanga. Wakufunzi katika kituo hicho ni Paschal Chiganga, Said Nassoro na Soud Abdi.
Wakufunzi wa kituo cha Mwanza kwa ajili ya waamuzi wa mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Tabora ni Alfred Kishongole, Kanali Issarow Chacha, Saloum Chama na Zahra Mohamed.
Kituo cha Songea ni kwa ajili ya waamuzi kutoka Iringa, Lindi, Mbeya, Mtwara, Njombe, Rukwa na Ruvuma. Wakufunzi katika kituo hicho ni Charles Ndagala, Joseph Mapunda, Riziki Majala na Victor Mwandike.
Waamuzi wote wanatakiwa kwenda katika kituo walichapangiwa. Vilevile wanatakiwa kuwa na barua kutoka kwa makatibu wa Vyama vya Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) wa mikoa yao ikiwatambulisha pamoja na kuonesha madaraja yao. 

Simba VS Mtibwa kesho kiingilio sh.5000

imagesMABINGWA wa michuano ya mtani Jembe, timu ya Simba,
kesho  inashuka katika Uwanja wa Taifa kuvaana na timu ya

Mtibwa Sugar, huku kiingilio cha chini kikiwa sh.5000.

Mchezo huo utakaoanza saa 10 jioni, ukiwa wa kirafiki,

kwa ajili ya kuziweka timu hizo sawa kabla ya kuanza kwa

Ligi Kuu tanzania Bara, inayoanza kutimua vumbi wiki

ijayo.

Simba inaingia dimbani ikiwa inatoka kwenye mashindano

ya Mapinduzi, ambapo Simba ilichukua ushindi wa pili.

Katika mchezo huo Simba iliyopo chini ya kocha Zdravko

Logarusic akisaidiana na Suleiman Matola, imepanga

kutumia wachezaji wake, wote ili kiwe kipimo tosha kabla

ya Ligi Kuu.

Timu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa

Ligi, imejipanga kuhakikisha inavuka mpaka nafasi ya

kwanza huku kocha wao Logarusic, akisema ana uhakika

kikosi chake kitaibuka na ushindi.

Logarusic, alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mtihani

wake wa kutambua kikosi chake, kabla ya kuanza kwa ligi

kuu.

Alisema ameambiwa kuwa Mtibwa Sugar, ni moja ya timu

nzuri hivyo anajua kwake ni kipimo kizuri.

“Nina amini mchezo wetu na Mtibwa Sugar, utakuwa mzuri

, kutokana na ubora wa timu hiyo, ninajua itasaidia timu

yangu kupata mazoezi mazuri”alisema Logarusic.

Nae kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, alisema ana

amini mchezo huo utakuwa mzuri kwake kutokana na

wapinzani wao kutoka katika mashindano.

Mexime alisema kuwa amepata nafasi ya kucheza na timu

kubwa, ambayo itampa mazoezi mazuri.

“Nina amini mchezo huo utakuwa mzuri kwangu kwa kuwa

nacheza na timu kubwa ambayo imetoka kwenye

mashindano”alisema Mexime.

Katika mchezo huo viingilio vitakuwa shilingi 20,000 VIP A,

shilingi 10,000 katika VIP B, wakati VIP C itakuwa shilingi

7,000 na sehemu ya viti vya orange na bluu itakuwa

shilingi 5000.

The Commonwealth Games Queen’s Baton Arrives in Dar es Salaam on 18 January

index
The Glasgow 2014 Commonwealth Games, British High Commission, Tanzania Olympic Committee and UNICEF Team up to Stop Violence Against Children in Tanzania
The Glasgow 2014 Commonwealth Games Queen’s Baton will arrive in Dar es Salaam on Saturday, 18 January. The actual run is planned for Sunday, 19 January, and will kick off from the National Stadium at 2.00 pm to State House where it will be presented to H.E. President Jakaya Kikwete. It is expected that over 300 people will be involved in the 12.4 km race.
Tanzania Olympic Committee’s Secretary General, Filbert Bayi, the British High Commissioner to Tanzania, Dianna Patricia Melrose, and the UNICEF Tanzania Representative, Dr. Jama Gulaid, will kick off the Relay, and be amongst the guests at State House.
This year, the Glasgow 2014 Commonwealth Games, the Commonwealth Games Federation and UNICEF have launched a ground-breaking partnership globally. In Tanzania, the event represents a unique opportunity for the Tanzania Olympic Committee, the British High Commission, UNICEF and other partners to harness the power of sport to help children grow up healthy, happy and safe.
The Queen’s Baton relay in Tanzania will be themed around the slogan: “Stop Violence Against Children, Let Them Play!”.
Speaking ahead of the Queen’s Baton Relay, British High Commissioner Dianna Melrose said:The Glasgow 2014 Commonwealth Games is teaming up with UNICEF to transform children’s lives across the Commonwealth. It’s the first time a charity affiliation to the Games has taken place. I am delighted the UK is supporting this excellent cause. Violence against children is a worrying issue and we must do all we can to stop it.”
The aim is to use the event as a catalyst to create awareness and better understanding of the issue of violence against children amongst a more general audience in Tanzania”, says the Tanzania Olympic Committee’s Secretary General, Filbert Bayi.
The Tanzania Violence Against Children Study, released by the Government and UNICEF in 2011 revealed that in Tanzania, violence affects a majority of children, everywhere. Some of the key findings are:
· one in three girls and one in seven boys in Tanzania experiences sexual violence before the age of eighteen; · most sexual assaults occur at home or in school – and children often know their sexual


WAZIRI MUHONGO KATIKA WARSHA YA UZINDUZI WA HIGH RESOLUTION AIRBONE GEOPHYSICAL DATA

pix1
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza
na wadau wa sekta ya madini (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa
warsha ya uzinduzi wa Mfumo wa Utafiti wa Geofizikia data leo jijini
Dar es laam.Picha zote na Benjamin Sawe – MAELEZO
pix2.
Mwakilishi wa Kampuni ya Geotech Airborne Limited Malcolm
Moreton akielezea namna kampuni yake ilivyoshirikiana na Serikali ya
Tanzania kuhakikisha mfumo wa Utafiti wa Geofizikia unafanikiwa.
pix2
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Geological Survey
Tanzania(GST) Abdulkarim H. Mruma akifafanua jambo wakati wa warsha ya
uzinduzi Mfumo wa Utafiti wa Geofizikia data leo jijini Dar es laam.

  pix3
Baadhi ya wadau wa sekta ya Jeolojia wakifuatilia mada kutoka
kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Geological Survey Tanzania(GST)
Abdulkarim Mruma (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
pix4
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo (waliokaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa

Warsha ya uzinduzi wa mfumo wa Utafiti wa Geofizikia Data iliyofanyika

leo jijini Dar es Salaam

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI NDULI ,MSIGWA AOMBA RADHI KWA KUKOSA WATU

Wananchi  na  watoto  wakiwa  katika mkutano wa kampeni za chadema kata ya Nduli jana
Mbunge Msigwa  kushoto akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Nduli Ayub Mwemba  jana wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa Chadema
Hii  ndio  hali halisi  ya  wananchi  waliofika katika mkutano  huo
Na Francis Godwin Blog
IKIWA ni  siku  mbili  toka  katibu  wa chama  cha mapinduzi (CCM) wilaya ya  Iringa Hassan Mtenga  kumwagiza  mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi  kufuatilia kero  mbili za  wananchi ikiwemo ya wagonjwa  kukosa dawa katika Hospital ya  mkoa na kujua fedha za  ruzuku ya  jimbo la Iringa mjini  ziko  wapi na zinafanya  nini ,mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna  kiasi cha Tsh milioni 30 nyingine  za mfuko wa jimbo.
 Huku mbunge Msigwa akiwaomba radhi  wananchi  wachache  waliofika katika mkutano  huo kwa kudai  kuwa haukutangazwa  vya kutosha  .
 
Hatua ya  katibu  huyo kuagiza  kufuatilia  fedha  hizo ni baada ya  jimbo  hilo kukabiliwa na changamoto mbali mbali na  fedha  hizo  zinazotolewa na Rais zimelenga  kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini Manispaa ya Iringa fedha  zinakaa bila kazi.
Akizungumza katika mkutano  wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Nduli  leo ,Msigwa alisema  kiasi  hicho  cha Tsh 30m zipo hadi  sasa 
“Naomba  kuwahakikishieni nitaendelea  kutafuta  vyanzo  vingine  vya  mapato  ili  kusaidia kero za maji  hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe Ayub Mwenda nitafanya  nae kazi”
Pia  Mbunge Msigwa amesema  kuwa  katibu  wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake  ila  yeye  saizi yake ni akina  waziri  mkuu Mizengo  Pinda,waziri wan chi  ofisi ya  waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani Wiliam Lukuvi na katibu mkuu  wa CCM Bw Kinana na  sio  yeye .
“Nataka  kuwahakikishia kuwa  huyu mimi  si  saizi yangu  saizi  yake ni akina Frank Nyalusi  diwani  wa Mvinjeni  (Chadema) na katibu  mwenzake wa Chadema Iringa mjini  Suazana Mgonakulima.
Wao  wanasema amekuja  kwa ajili ya  kunishughulikia mimi ila nasema njia  aliyojia atatitoka na njia  hiyo hiyo kama  walikuwepo akina Charles Charles na  wametoka zaidi ya makatibu  7  iwe  yeye .
Hata  hivyo katika mkutano  huo ambao idadi ya  watu  ilionekana ni ndogo  zaidi  ukilinganisha na hali halisi  ya  nguvu  ya  Chadema   iliyokuwepo  jimbo la Iringa mjini ,bado  mbunge huyo  alitumia mkutano huo kuwaomba radhi  wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi kwa madai  haukutangazwa vya  kutosha.
Kampeni  za  uchaguzi  mdogo  wa kata  hiyo ya  Nduli  zimeanza  rasmi leo kwa Chadema  kufungua  pazia  hilo huku wao CCM wanataraji  kuzindua kampeni  hizo katika  eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu
Uchaguzi  huo mdogo umekuja  kufuatia kifo cha aliyekuwa  diwani wa kata   hiyo Idd Rashid  Chonanga  aliyefariki  duni kwa ugonjwa mapema mwaka  jana
Kwa  upande wake  mgombea  udiwani wa Chadema  katika kata  hiyo ya  Nduli Ayub Mwenda  ambae  alipata  kuwa mwenyekiti wa kijiji  cha Nduli kabla ya  CCM kumsimamisha nafasi  hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za ubadhilifu  wa fedha  za maendeleo ,alisema  kuwa yeye ana  risiti  za fedha  zote ambazo alikuwa akikusanya na  kuwa kusimamishwa kwake nafasi ya uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya  ya Iringa mjini Lusiana Mbosa na  kuwaomba  wananchi  kumkubali  sasa ili awe  diwani wa kata  hiyo.
Wachambuzi  wa masuala ya  kisiasa mjini Iringa  wanadai  kuwa kipimo cha  kukubalika ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo  hilo kwa mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi  za  serikali za mitaa ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli 

WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO LA MAAFA MAUAJI YA WAKULIMA KITETO

IMG_0017
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kiteto baada ya kuwasili wilayani humo  Januari 16, 2014  kufuatilia suala la mauaji ya wakulima. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
  IMG_0021
Eneo la Mtanzania  wilayani Kiteto  ambalo ni moja kati ya maeneo ya  makazi  yaliyovamiwa na watu wanaodaiwa kuwa wafugaji  ambapo watu watatu waliuawa na nyumba kuchomwa moto. Mlheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alitembelea eneo hilo Januari  16, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0030
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanakijiji wa  Mtanzania Januari 16, 2013 wakati alipokwenda kuwapa pole  kufuatia uvamizi waliofanyiwa  na watu wanaosadikiwa kuwa wafugaji ambao waliua watu watatu  na kuchoma nyumba . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Erasto Mbwilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0042
Baadhi ya wananchi wa Kiteto  wakimsikiliza  Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia  Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo  ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na  watu wanaosadikiwa kuwa  ni wafugaji. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0050
Baadhi ya wananchi wa Kiteto  wakimsikiliza  Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakati alipowahutubia  Januari 16, 2014 katika mji wa Kibaya alipokwenda kuwapa pole wakulima wa wilaya hiyo  ambao walishambuliwa, kuuwawa na nyumba zao kuchomwa moto na  watu wanaosadikiwa kuwa  ni wafugaji. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0059
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na wazee  wa Kiteto wakati alipoteta nao baada ya kuhutubia  mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kibaya Janauari 16, 2014. Alikwenda Kiteto kuwapa pole wakulima  ambao walishambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji ambao waliua na  kuchoma moto nyumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


SHIRIKA LA NYUMBA NHC LATOA MAFUNZO KWA VIKUNDI VYA VIJANA,LENGO NI KUBADILI MAISHA YAO

1
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akizungumza wakati wa maadalizi ya ufungaji wa mafunzo ya vijana wawakilishi wa vikundi  kutoka mikoa mbalimbali kuhusu utengenezaji wa matofali ya ya udongo yenye teknolojia ya Interlocking Blocks yaliyoanza Januari 6 mpaka 17 mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufungwa wiki ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, Mkurugenzi huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada wa sabuni na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti limeamua kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo  na kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali  zipatazo 640 katika wilaya 160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa  kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja. 2Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akizungumza akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari  3 
Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) akifafanua masuala ya kitaalamu kuhusu teknolojia hiyo ya matofali kwa waandishi wa habari. 4 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. 5 
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. 7 
Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.

PINDA CHANA Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu


indexWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Uteuzi huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha 13(i) cha Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013.
Aidha Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema ,Dr. Vicensia Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam  na Bishop Hiluka kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Wajumbe wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ntobi Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo ambaye ni Katibu wa Bodi ya Filamu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI(MAELEZO)-16.1.201

MKUU WA MKOA WA RUKWA AONANA NA TIMU MAALUUM YA KUHAKIKI MAENEO MAPYA YA UTAWALA KUTOKA TAMISEMI, AISHAURI MAMLAKA HUSIKA KUANGALIA UPYA VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUGAWA MAENEO MAPYA YA UTAWALA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na timu maalum inayohakiki maeneo mapya ya utawala kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Pichani kulia na timu yake ya Mkoa iliyokuwa ikiratibu maeneo hayo ofisini kwake leo tarehe 17 Januari 2014. Timu hiyo kutoka TAMISEMI inaongozwa na Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale (watatu kulia).
 
 Katika kikao hicho kifupi Mkuu huyo wa Mkoa ameiomba mamlaka husika kupitia timu hiyo kuangalia upya vigezo vinavyotumika katika kugawa maeneo mapya ya utawala na upandishaji wa madaraja kutoka kijiji, kata, Tarafa, Halmashauri, Miji na Manispaa. 
 
Alisema kuwa kuna maeneo mengine ambayo yakiangaliwa kwa kigezo kimoja cha wingi wa watu bila kuangalia umbali wa huduma na giografia ya eneo husika unakuta wananchi wanakosa huduma zao za msingi na kupata tabu kubwa katika kuzipata.
 
 Alitolea mfano vijiji vikubwa vya mwambao ambavyo kupata huduma katika kata zao ni lazma wavuke upande mmoja wa Ziwa kwenda upande mwingine jambo ambalo ni hatarishi kama ilivyotokea kwa wananchi wa Kijiji cha Kipwa Mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambao hivi karibuni walipoteza watu 15 katika ajali ya boti walipokwenda kupata huduma ya afya. Wengi ya waliofariki katika ajali hiyo mbaya walikuwa ni watoto chini ya umri wa miaka 5.  
Kikao kikiwa kinaendelea ambapo kwa upande wake Mwanasheria wa TAMISEMI Ndugu Eustard Ngatale alisema kuwa kubariki na kuhalalisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya Utawala vipo vitu mbalimbali vya kuzingatia ambavyo ni pamoja na kuwepo kwa makubaliano ya wananchi na viongozi wa maeneo husika kupitia mihutasari ya vikao maalumu vya kisheria vya WDC, Halmashauri, DCC na RCC katika ngazi ya Mkoa.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

BALOZI WA NORWAY ATEMEBELEA WIZARA YA MAJI

IMG_0605 
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Baloziwa Norway (kushoto), Bi. Ingunn Klepsvik pamoja na maafisa wake na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad Mutalemwa. IMG_0631 
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik.
Balozi wa Norway, Bi. Ingunn Klepsvik, jana alitembelea Wizara ya Maji na kuonana na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe.Balozi huyo alipata fursa ya kuzungumza na Prof. Maghembe kuhusu hali halisi ya sekta ya maji nchini na miradi mbalimbali ambayo Serikali ya Norway inafadhili.Bi. Klepsvik aliambatana na maafisa mbalimbali kutoka ubalozi wa Norway, huku Wizara ya Maji ikiwakilishwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maji Mijini, Inj. Amani Mafuru na Mkurugenzi Mtendaji wa DAWASA, Archad Mutalemwa.


KIWANJA KIPYA CHA MARAHA AIRPORT JIJINI DAR ES SALAAM

1a 2 3 4 5 6 7 8 9 10a 10b 11