Na Francis Godwin Blog
IKIWA ni siku
mbili toka katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
Hassan Mtenga kumwagiza mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Aman Mwamwindi kufuatilia kero mbili za wananchi ikiwemo ya
wagonjwa kukosa dawa katika Hospital ya mkoa na kujua fedha za ruzuku
ya jimbo la Iringa mjini ziko wapi na zinafanya nini ,mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa adai kuna kiasi cha Tsh
milioni 30 nyingine za mfuko wa jimbo.
Huku mbunge
Msigwa akiwaomba radhi wananchi wachache waliofika katika mkutano
huo kwa kudai kuwa haukutangazwa vya kutosha .
Hatua ya katibu
huyo kuagiza kufuatilia fedha hizo ni baada ya jimbo hilo
kukabiliwa na changamoto mbali mbali na fedha hizo zinazotolewa na
Rais zimelenga kusukuma maendeleo majimboni ila alihoji kwanini
Manispaa ya Iringa fedha zinakaa bila kazi.
Akizungumza katika
mkutano wake wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata
ya Nduli leo ,Msigwa alisema kiasi hicho cha Tsh 30m zipo hadi
sasa
“Naomba
kuwahakikishieni nitaendelea kutafuta vyanzo vingine vya mapato
ili kusaidia kero za maji hapa Nduli ….mimi nasema ukweli namba mnipe
Ayub Mwenda nitafanya nae kazi”
Pia Mbunge Msigwa
amesema kuwa katibu wa CCM Hassan Mtenga si saizi yake ila yeye
saizi yake ni akina waziri mkuu Mizengo Pinda,waziri wan chi ofisi
ya waziri mkuu sera na uratibu wa bunge na mbunge wa ISimani Wiliam
Lukuvi na katibu mkuu wa CCM Bw Kinana na sio yeye .
“Nataka
kuwahakikishia kuwa huyu mimi si saizi yangu saizi yake ni akina
Frank Nyalusi diwani wa Mvinjeni (Chadema) na katibu mwenzake wa
Chadema Iringa mjini Suazana Mgonakulima.
Wao wanasema
amekuja kwa ajili ya kunishughulikia mimi ila nasema njia aliyojia
atatitoka na njia hiyo hiyo kama walikuwepo akina Charles Charles na
wametoka zaidi ya makatibu 7 iwe yeye .
Hata hivyo katika
mkutano huo ambao idadi ya watu ilionekana ni ndogo zaidi
ukilinganisha na hali halisi ya nguvu ya Chadema iliyokuwepo
jimbo la Iringa mjini ,bado mbunge huyo alitumia mkutano huo kuwaomba
radhi wananchi kutokana na mahudhurio hayo hafifi kwa madai
haukutangazwa vya kutosha.
Kampeni za
uchaguzi mdogo wa kata hiyo ya Nduli zimeanza rasmi leo kwa
Chadema kufungua pazia hilo huku wao CCM wanataraji kuzindua
kampeni hizo katika eneo hilo la Nduli Januari 26 mwaka huu
Uchaguzi huo
mdogo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo Idd
Rashid Chonanga aliyefariki duni kwa ugonjwa mapema mwaka jana
Kwa upande wake
mgombea udiwani wa Chadema katika kata hiyo ya Nduli Ayub Mwenda
ambae alipata kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Nduli kabla ya CCM
kumsimamisha nafasi hiyo kutokana na kuwa na tuhuma za ubadhilifu wa
fedha za maendeleo ,alisema kuwa yeye ana risiti za fedha zote
ambazo alikuwa akikusanya na kuwa kusimamishwa kwake nafasi ya
uenyekiti ni uoneu uliofanywa na aliyekuwa katibu wa CCM wilaya ya
Iringa mjini Lusiana Mbosa na kuwaomba wananchi kumkubali sasa ili
awe diwani wa kata hiyo.
Wachambuzi wa
masuala ya kisiasa mjini Iringa wanadai kuwa kipimo cha kukubalika
ama kutokukubalika kwa mbunge Msigwa katika jimbo hilo kwa mwaka 2015
katika uchaguzi mkuu na mwaka huu katika chaguzi za serikali za mitaa
ni uchaguzi huo wa kata ya Nduli
|
No comments:
Post a Comment