30 TWIGA STARS WAITWA KUIVAA ZAMBIA
Kocha
Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ametaja kikosi cha wachezaji 30
wanaoingia kambini kesho (Januari 15 mwaka huu) jijini Dar es Salaam
kujiandaa kwa mechi dhidi ya Zambia mwezi ujao.
Mechi
hiyo ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika
kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika baadaye mwaka huu jijini Windhoek,
Namibia itafanyika jijini Lusaka
Wachezaji
walioitwa kwenye kikosi hicho ni Amina Ally (Lord Baden Sekondari),
Amisa Athuman (Marsh Academy), Anastazia Anthony (Lord Baden Sekondari),
Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar) na Belina
Julius (Lord Baden Sekondari).
Donisia
Daniel (Lord Baden Sekondari), Esther Chabruma (Sayari Queens), Evelyn
Sekikubo (Kwimba Chuoni), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Hassan
(Mburahati Queens), Fatuma Issa (Evergreen) na Fatuma Mustapha (Sayari
Queens).
Fatuma
Omari (Sayari Queens), Happiness Hezron (Copa Coca-Cola Ilala), Maimuna
Hamisi (U20 Tanzanite), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Real
Tanzanite), Mwapewa Mtumwa (Sayari Queens), Najiat Abbas (Makongo
Sekondari) na Neema Paul (U20 Tanzanite).
Pulkeria
Charaji (Sayari Queens), Semeni Abeid (Real Tanzanite), Shelder
Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari Queens), Theresa
Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis
(Mburahati Queens).
RAMBIRAMBI MSIBA WA KANALI MMARI
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mwanzilishi wa wa timu ya Oljoro JKT, Kanali Mmari kilichotokea jana
(Januari 13 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Kanali
Mmari ambaye aliasisi timu hiyo na kuifikisha hadi kwenye Ligi Kuu ya
Vodacom amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa
amelazwa baada ya kupata ajali ya gari Chalinze mkoani Pwani, Januari
Mosi mwaka huu.
Msiba
huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani mbali kuasisi timu ya
Oljoro JKT alikuwa mhamasishaji mkubwa wa mchezo huo mkoani Arusha,
hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kanali Mmari, klabu ya Oljoro JKT,
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Arusha (ARFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
MAOFISA TFF KUKAGUA VIWANJA 19 VYA VPL, FDL
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua maofisa wanaoanza leo
(Januari 14 mwaka huu) kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Ukaguzi
huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa
marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.
Viwanja
vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza),
Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage
(Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora
(Iringa)/
Kumbukumbu
ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani),
Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui
(Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha),
Umoja (Mtwar.) na Vwawa (Mbozi).
Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.
No comments:
Post a Comment