Rais wa Chama
cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) Injinia Peter
Chisawillo akizindua rasmi utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni
kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS Mobile System) kuhusu madhara
yatokanayo na urejeshwaji wa ada za biashara kila mwaka kwa lengo la
kuishawishi serikali kuweka sera, sheria na taratibu rafiki kwa
mazingira ya ufanyaji biashara nchini leo jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………………………………
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.Dar es salaam.
Chama
cha Wafanyabiashara,Wenyeviwanda na Kilimo (TCCIA) kimezindua rasmi
utafiti utakaohusisha ukusanyaji wa maoni kupitia ujumbe mfupi wa simu
(SMS Mobile System) kuhusu madhara yatokanayo na urejeshwaji wa ada za
biashara kila mwaka kwa lengo la kuishawishi serikali kuweka sera,
sheria na taratibu rafiki kwa mazingira ya ufanyaji biashara nchini.
Akizungumzia
utafiti huo leo jijini Dar es salaam Rais wa cha hicho Injinia Peter
Chisawillo amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka wa fedha wa 2013/2014
serikali ilitangaza urejeshwaji wa ada ya leseni za biashara nchi nzima
na kuongeza kuwa utaratibu huo unaomlazimu mfanyabiashara kukata leseni
na kuilipia kila mwaka unakwenda kinyume na sheria ya leseni ya mwaka
1972.
Amesema
kuwa sheria hiyo na hasa marekebisho yake ya mwaka 2004 yaliwezesha
leseni za biashara kutolewa bure na mara moja tu kwa kipindi cha maisha
yote ya biashara jambo ambalo linakiukwa.
“Tayari
kuna malalamiko mengi kwa jumuiya ya wafanyabiashara yanayotufikia
kutoka kuanzia ngazi za wilaya na mikoa juu ya urejeshwaji wa ada hiyo,
sekta binafsi inailalamikia serikali kwa kutoishirikisha katika
urejeshaji wa utaratibu huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja”
amesema Injinia Chisawillo.
Ameeleza
kuwa sekta binafsi inaamini kuwa serikali imeamua kuongeza mapato bila
kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta isiyo rasmi kwa lengo la
kuharakisha uchumi kwa ujumla na kuongeza kuwa hakuna mwongozo maalum
uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi ya leseni
yatakavyoshughulikiwa.
Amesema
sekta binafsi inaamini kuwa ili kuondoa urasimu na usumbufu kwa
wafanyabiashara pindi wanapoomba leseni kila mwaka , serikali itumie
kumbukumbu zilezile kila mwaka bila kulazimu mfanyabiashara kufuata
mlolongo wa taratibu za kuomba leseni kila mwaka kwa lengo la kuokoa
muda na kupunguza kupanda kwa gharama za uendeshaji wa biashara.
Aidha
Injinia Chisawillo amesema kuwa utafiti huo unaofanywa na TCCIA)
utafanyika kwa muda wa wiki 4 ukiwahusisha wanachama wote takribani
22,000 (Elfu Ishirini na mbili) na wale wasio wanachama na unafadhiriwa
na Shirika lisilokuwa la kiserikali la BEST –AC ili kuwawezesha
wafanyabiashara hao kutuma ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu zao
kwenda namba 15539 na kutoa maoni kuhusu urejeshwaji wa ada hiyo.
No comments:
Post a Comment