MRENO
Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka wa
FIFA kwa mara ya pili katika historia yake, akimuangusha mshindani wake
mkuu, Lionel Messi.
Nyota
huyo babu kubwa wa Real Madrid alikuwa anakabiliwa na ushindani wa
mbali kidogo kwa nyota wa Barcelona, Messi na wa Bayern Munich, Franck
Ribery katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or.
Akiwa
mwenye hisia kali, Ronaldo aliyekwenda jukwaani kuchukua tuzo yake
akiwa ameambatana na mtoto wake wa kiume, Cristiano alishindwa kujizuia
na kumwaga machozi wakati anapokea taji hilo.
Mshindi: Pele akiwa amemshika mtoto wa Ronaldo, Cristiano wakati Mreno huyo anapokea tuzo yake
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 amepewa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao
66 katika mechi 56 za klabu na nchi yake, Ureno mwaka 2013 hatimaye
kuirejesha tuzo yake aliyoitwaa awali mwaka 2008.
Pamoja
na kwamba Ronaldo hakutwaa taji kubwa mwaka 2013, alifunga mabao yote
manne Ureno ikiitoa Sweden katika kinyang’anyiro cha tiketi ya kombe la
Dunia baadaye mwaka huu.
“Hakuna
maneno ya kusema wakati huu,” Ronaldo alisema, huku akifuta
machozi. ”Nataka kuwashukuru wenzangu wote na washirika pale Real
Madrid, katika timu ya Ureno na familia yangu, ambako wako nami,”.
“Wale
ambao wananifahamu mimi, wanafahamu kwamba watu wengi wananisaidia:
kocha wangu, rais wetu, na sitaki kusahau kumtaja Eusebio. Mpenzi wangu
na mwanangu pia. Nasonga zaidi,”.
No comments:
Post a Comment