Young
Africans imeanza vizuri katika kambi yake ya mafunzo nchini Uturuki
baada ya kuifunga timu ya Ankara Sekerspor kwa mabao 3-0 katika mchezo
wa kirafiki uliofanyika pembeni kidogo ya eneo ililofikia katika mji wa
Manavgat Antalya.
Kocha
wa Young Africans aliwatumia wachezaji 18 jumla katika mchezo huo ambao
wenyeji mara baada ya mchezo walimpongeza kwa timu yake kwa kucheza
vizuri katika mchezo huo wa kirafiki.
Dakika
ya 10 ya mchezo shuti lililopigwa na mganda Emmanuel Okwi lilishinda
mlinda mlango wa Ankara Sekerspor ambapo aliutema mpira huo na kumkuta
Didier Kavumbagu aliyeukwamisha mpira huo wavuni na kuhesabu bao la
kwanza.
Timu
zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na mpaka dakika 45 za kipindi
cha kwanza zinamalizika, Ankara Sekerspor i0 – 1 Young Africans .
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika moja Young Africans
kujipatia bao la pili la mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyeitumia
vyema pasi ya mwisho ya kiungo Mrisho Ngasa aliywatoka walinzi wa Ankara
Sekaspor na kumpasia mfungaji ambaye hakufanya makosa na kuukwamisha
mpira wavuni.
Dakika
ya 58 kocha Mkwasa alifanya mabadiliko, ambapo waliingia Hamis Kizza na
Nizar Khalfani kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na kiungo Hassan
Dilunga.
Hamis
Kizza aliipatia Young Africans bao tatu la mchezo na la ushindi dakika
ya 61 ya mchezo baada mpira aliogongewa na Domayo kuwapita walinzi wa
Ankara Sekerspor na kumkuta Kizza ambaye alipiga shuti liliomgonga
mlinzi wa Ankara Sekerspor wakati akiokoa na kujaa wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Ankara Sekerspor 0 -3 Young Africans.
Mara
baada ya mchezo kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface
Mkwasa alisema anashukuru vijana wake walicheza vizuri kwa kufuata
malekezo na ndio maana wakaweza kupata ushindi huo,makosa yapo machache
yaliyojitokeza na ataendelea kuyafanyia kazi.
“Mechi
ilikua ni nzuri ukizingatia ndo mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki
tukiwa na siku ya tatu tangu tufike hapa Uturuki, kwa mazoezi ya jana
vijana wameosha mabadiliko na leo wameweza kucheza vizuri na kuweza
kupata ushindi, kikubwa naamini kwa siku zilizobakia nitaendelea kufanya
marekebisho na kukifanya kikosi kuendelea kuwa bora pindi kitaporejea
nchini tayari kwa mzunguko wa pili wa Lig Kuu ya Vodacom” alisema
Mkwasa
Kikosi cha Young Africans kilichocheza leo ni:
1.Juma
Kaseja/Ally Mustafa “Barthez” (dkk 65), 2.Juma Abdul, 3.Oscar
Joshua/David Luhende(dkk 82), 4.Mbuyu Twite (C), 5.Kelvin Yondani,
6.Frank Domayo/Ibrahim Job(dkk 80), 7.Haruna Niyonzima/Saimon Msuva
(dkk72), 8.Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (dkk 58), 9.Didier
Kavumbagu/Hamis Kizza (dkk 58), 10.Mrisho Ngasa/Jerson Tegete (dkk 68),
11. Emmanuel Okwi/Said Bahanuzi (dkk 85)
No comments:
Post a Comment