Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha
siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika
leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka
50 ya Mapinduzi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
wa mjini Zanzibar kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashuri Kuu ya CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud
Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi
ya uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara
baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea
wa nafasi uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM.
Picha na Adam H. Mzee
No comments:
Post a Comment