Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein
akiwapungia mkono wasanii wa asili na vikundi vya ngoma wakati Fensi
katika barabara ya Kibandamaiti Wilaya ya Mjini jana,katika shamra
shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,wengine waliokaa Makamo wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Wasanii
wa fensi ambao hujipaka mafuta machafu (mobile) wakiwa na mishale
wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein pamoja na Viongozi mbali mbnali na
wananchi waliohudhuria kuangalia fensi hiyo iliyoshirikisha kazi za
taasisi za Serikali na Binafsi,katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini
Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Wasanii
wakionesha namna ya tiba za asili kwa njia ya kupandisha mizuka ikiwemo
ngoma za pungwa, wakati wa Fensi iliyopita katika barabara ya
Kibandamaiti,Wilaya ya Mjini jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar,[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Baadhi
ya Wananchi wa Mji wa Unguja na Vitongoji vyake wakiangalia Fensi
iliyopita katika Barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni
shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na
Ramadhan Othman,Ikulu.]
Ngoma ya Beni (Mbwa kachoka) ikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, katika barabara ya Kibandamaiti Mjini Unguja jana,ikiwa ni shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
No comments:
Post a Comment