TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, January 12, 2014

NHIF & KfW yakabidhi vifaa tiba Mbeya na Tanga

1     
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyotumika katika vituo vya kutolea huduma vinavyohudumia wanufaika wa mradi wa akina mama wajawazito unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Watu wa Ujerumani (KfW) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
2 
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akikabidhi  moja  ya vifaa tiba kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.Noman Sigalla. 3   
 Naibu waziri wa Afya Dk Seif Rashid akimkabidhi moja ya mashine ya
kusaidia watoto wachanga matroni Mary Mlay aliyemwakilisha mkuu wa
mkoa wa Tanga katika hafla hiyo.
4 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee akitoa maelezo ya Mradi wa KfW unaoendeshwa kwa ushirikiano wa Benki wa Watu wa Ujerumani na NHIF.  5  
Kaimu Mkuu wa Mbeya Dk. Noman Sigalla akitoa salaam za Mkoa kwa wadau wa mradi huo mbele ya Naibu Waziri wa Afya.  6 
 Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (mbele) wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii. 7    
Sehemu ya wadau wa sekta ya afya kutoka Mbeya na Tanga waliohudhuria hafla hiyo.
………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya watu wa Ujerumani (KfW) imeunga mkono mkakati wa Kitaifa wa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano kwa kutoa vifaa tiba katika vituo vya matibabu vinavyohudumia  kundi hilo.
Msaada huo unaohusisha mikoa ya Mbeya na Tanga wenye thamani ya shilingi milioni 989.1 umekabidhiwa leo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi kwa Waganga Wakuu wa mikoa hiyo.
 Akikabidhi msaada huo, Dk. Rashid alisema kuwa msaada huo utaboresha huduma za akina mama wajawazito na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi lakini pia ni fursa ya vyanzo vya mapato kwa Halmashauri na watoa huduma.
“Sote tunafahamu kuwa matibabu sahihi yanatokana na vipimo sahihi hivyo uwekezaji unaofanywa kwa pamoja na NHIF & KfW kupitia mradi huu kwa lengo la kuviwezesha vituo vya matibabu kupata vifaa tiba utasaidia sana kupunguza tatizo la upatikanaji wa huduma ya vipimo kwa akina mama wajawazito na watoto,” alisema Dk. Rashid.
Kutokana na hali hiyo, Dk. Rashid aliwaagiza Waganga Wakuu ambao wamekabidhiwa vifaa hivyo kuhakikisha vinatumika ipasavyo na kutunzwa kwa faida ya Taifa ili vipumguze vifo vya akina mama hao na watoto.
“Ni vyema walengwa wa mradi huu wakapata huduma bora na si bora huduma, msaada huu uwe na matokeo mazuri kwa walengwa ili mradi uwe na manufaa kwa nchi yetu,” alisema.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamisi Mdee alisema Mfuko unatarajia mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo yatashawishi akina mama wengi zaidi kutumia huduma za uzazi salama katika vituo vya matibabu lakini pia wafadhili kupanua maeneo ya mradi katika mikoa wanayofadhili.
Aidha alizitaka Halmashauri kuwasilisha kwa wakati madai yao baada ya kutoa huduma kwa wanachama pamoja na maombi ya fedha za tele kwa tele ili kuboresha huduma za matibabu katika vituo vyao.
Akizungumzia mafanikio ya mradi, alisema kuwa hadi sasa umefikia walengwa 74,099 ambao ni sawa na asilimia 105 na jumla ya shilingi 644,1118,912 zimelipwa kwa vituo vya matibabu vya mikoa ya Mbeya na Tanga vilivyotoa huduma kwa akina mama hao lakini pia shilingi milioni 400.4 zimetumika kulipia familia za akina hao kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

No comments:

Post a Comment