Mamia
ya washiriki tayari wanajiandikisha kwa wingi kupitia mtandao wa
intaneti ili kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2014 zinazotarajiwa
kufanyika Moshi tarehe 2 Machi, 2014.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu
wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo amesema katika taarifa yake
kwa vyombo vya habari jana kwamba idadi kubwa ya washiriki wanaendelea
kujiandikisha kupitia tovuti yam bio hizo www.kilimanjaromarathon.com
ukilinganisha na mwaka jana ambapo wachache walijiandikisha kupitia
mtandao. Uandikishwaji huo wa mtandao ambao upo wazi mpaka tarehe 18
Februari, 2014 unawapa urahisi wa kujiandikisha hasa washiriki kutoka
nje ya nchi ambao wanatakiwa kujiandaa na safari ya kuja nchini kutokana
na mtandao huo kutoa uthibitisho wa usajili mara tu baada ya kujaza
taarifa husika.
Addison
aliongeza kuwa ongezeko kubwa la usajili kupitia mtandao ni ishara
kwamba mbio za mwaka huu zitakuwa na washiriki wengi zaidi wa kigeni
ukilinganisha na zaidi ya 400 walioshiriki mwaka jana. “Ongezeko la
ushiriki lina maana kwamba mbio inazidi kukua kwa kiasi kikubwa na hii
ni kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na Kilimanjaro Premium Lager
ambao wamewekeza kwenye mbio hizi tangu zilipoanzishwa mwaka 2003.”
Pia
Addison alisema ukuaji wa mbio hizi ni matokeo ya jitihada kubwa
zinazofanywa na waandaaji kupitia mtandao wa intaneti pamoja na mbio
hizi kuonyeshwa bara zima la Afrika kupitia SuperSport na televisheni
nyingine za kimataifa dunia nzima.
Zikiwa
zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 2 Machi, 2014, mbio za Kilimanjaro
Marathon zitakuwa na matukio manne ambayo mbio ndefu za 42km Kilimanjaro
Premium Lager Marathon, 21km Nusu Marathon, 11km GAPCO Disabled Run
(zitahusisha viti vya magurudumu na baisikeli za mikono tu), na mbio za
kujifurahisha za Vodacom 5km Fun Run ambazo hutoa fursa kwa watu wa rika
zote kushiriki.
Kwa
mara nyingine tena mbio hizi zitakuwa kivutio kutokana na ushiriki wa
timu zitakazowakilisha makampuni mbalimbali kupitia shindano la Half
Marathon Corporate Challenge.
No comments:
Post a Comment