Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza
kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko
(Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
Rais
Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na
Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi
hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati
Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa
Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio
wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa
ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili
26, 1964.
Naye
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali
Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania
Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye
Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50
ya Mapinduzi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13, 2014, itakuwa ni Siku ya
Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote kusheherekea miaka 50 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini Zanzibar ambako leo ameungana na
Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi
hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati
Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa madarakani utawala dhalimu wa
Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika historia Waafrika walio
wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa
ni Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili
26, 1964.
Naye
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali
Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa Siku ya Mapumziko Tanzania
Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
Shein alitangaza mapumziko hayo wakati alipohutubia wananchi kwenye
Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika kusherehekea miaka 50
ya Mapinduzi.
Mwisho.
Imetolewa na;
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es Salaam.
12 January, 2014
No comments:
Post a Comment