Baadhi
ya watoto yatima wa kituo cha Sifa Group Children Foundation Center
kilichopo Bunju, Dar es Salaam wakiwapokea kwa furaha wafanyakazi wa
Idara ya mauzo na Usambazaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakati
walipoenda kutoa msaada kwenye kituo hicho. Msaada huo wa chakula na
vitu mbali mbali kupitia kampeni ya pamoja na Vodacom.
……………………………………………………………………
Mkurugenzi
wa kituo cha kulelea yatima cha Sifa Group Foundation Children Center
kilichopo Bunju mkoani Dar Es Salaam ametoa wito kwa wadau mbali mbali
nchini kuwa tayari kujitolea kusaidia vituo vya watoto yatima kikiwemo
kitu chake ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili vituo vingi nchini
ikiwemo uhaba wa madarasa ya kujisomea, ubovu wa vyoo na malazi.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi huyo wakatiakipokea
misaada kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kupitia
taasisi yake ya Vodacom Fondation iliyojumuisha vitu mbali mbali ikiwemo
magodoro, vifaa vya shule, vyombo vya ndani, vyakula pamoja na ada za
shule kwa watoto wa kituo hicho.
“Tuna
tatizo la uhaba wa fedha ili kuweza kumalizia kituo chetu kipya ambacho
tumejitaidi kupata kiwanja hadi sasa lakini bado hatujapata fedha
zakuweza kujengea kituo hicho, vile vile tunahitaji tujenge madarasa
ambayo yatasaidia watoto wetu kujisomea lakini fedha hatuna zakuweza
kufanikisha mradi huo.”
“Tunapokea
watoto wengi ambao hawana uwezo wa kusoma wala kuandika tumechukua
jukuma la kuwafundisha hapa kwa uwezo mdogo tulionao na darasa hili dogo
ambali haliwatoshi na pia halina vifaa kamili vya kufundishia,
tunawaomba wadau wajitolee kutusaidia ili tuweze kutoa elimu kwa watoto
hawa amba ndio msingi pekee wa kuwapatia ili wajiendeleze katika maisha a
Yao.”
Mkurugenzi
huyo alitanabaisga kuwa, “Tumekuwa tukilalamika siku hadi siku
kuhusiana na ubovu wa vyoo tulio nao ambao mara kwa mara husababisha
maradhi mbalimbali kwa watoto kutokana na wingi wa watoto kuto kuendana
na idadi ya vyoo wanavyotumia ni vichache hivyo inakuwa vigumu kuviweka
vikiwa visafi wakati wote,”.Alisema
Kwa
upande wake Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,
Hassan Saleh wakati wa makabidhiano ya misaada hiyo ameeleza kuwa ni
jambo la busara wao kama kampuni kusaidia kutatua matatizo yaliyondani
ya jamii kwani wao ndio wanaowaunga mkono kila siku.
“Tunaamini
misaada tuliyoitoa itaweza kusaidia watoto hawa kwa namna moja au
nyingine, tunatambua changamoto wanazokumbana nazo lakini sisi kama
kampuni tuataendelea kuhakikisha tunasaidia jamii kadri tuwezavyo, hiyo
imekuwa ni jadi yetu na hatuwezi kuicha.”Alisema Saleh
Mmoja
wa watoto anaelelewa katika kituo hicho Shantala Mussa aliwashukuru
wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kutoa sehemu ya fedha zao na kuwasaidia
kwa kuwaletea misaada hiyo na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa
kujitolea na kutoa wito kwa makampuni mengine kuweka mazoea yakujitolea
ili kuweza kuwafanya watoto yatima wasahau matatizo wanayokumbana nayo
na kujihisi nao ni watoto wanaohitaji matuzo kama watoto wa kawaida.
No comments:
Post a Comment