Wananchi wakiwa katika mkutano huo leo |
Wananchi Iringa mjini wakiwa wamejipanga kwa maswali katika mkutano wa CCM Iringa mjini leo |
Diwani wa kata ya Mtwivila Bw Victor Mushi akijibu maswali ya wapiga kura wake katika mkutano huo wa CCM
Iringa mjini leo
……………………………………………………………….
Na Francis Godwin Blog Iringa
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya
ya Iringa mjini kimeanza kufufua matumaini ya wananchi wa jimbo
la Iringa mjini juu ya kero zinazowakabili kwa kuwaweka kitimoto
madiwani wake katika mkutano wa hadhara kwa kumtaka kila mwananchi
kumhoji diwani wake kama anatosha ama hatoshi kuendelea kuwaongoza.
Huku wananchi wa jimbo hilo la Iringa mjini wakikitaka chama hicho kusaidia kukinusuru chama na kura za chuki kutokana na shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kuendelea kupandisha gharama za umeme.
Wakihoji katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa leo ,wananchi hao walisema kuwa ili CCM jimbo hilo na Tanzania kwa ujumla kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ule wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu ni lazima gharama za umeme ishuke
Kwani walisema kuwa hatua ya TANESCO kuendelea kuongeza bei ya umeme ni kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania na kuwa ushindi wa CCM utatokana na utetezi wa chama katika kuwaondolea mzigo wa bei ya umeme watanzania.
Mbali ya hilo pia wananchi wa kata ya Kihesa walimbana diwani wao Bw Mussa Wanguvu kutokana na hatua ya kushindwa kupigania wananchi ambao wanatakiwa kuvunja nyumba zao ambazo zimejengwa katika eneo la Semtema Majengo mapya eneo ambalo halitakiwi kisheria
Diwani Wanguvu akijibu swali hilo alisema kuwa eneo hilo lilizuiwa baada ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara hasa wale ambao wamejenga katika mlima na wapo hatarini kuangukiwa na mawe ila baadhi ya maeneo ambayo si rasmi ni waliachiwa .
Kwa upande wao wananchi wa kata ya Mtwivila walimtaka diwani wao Bw Victor Mushi kueleza ni lini atatekeleza ahadi yake ya zahanati na ubovu wa barabara katika eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa upande wake diwani Mushi kuhusu suala la ujenzi wa kituo cha afya alisema kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake ila ilikuwa katika ilani ya CCM japo alisema ujenzi wa mradi huo upo mbioni baada ya kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo wa ujenzi wa kituo cha afya.
Kuhusu barabara alisema kuwa kata hiyo wamejitahidi kutengeneza mifereji na zaidi ya Tsh bilioni 1.8 zitatengeneza barabara ya lami kutoka Mtwivila kwenda Mkwawa na tayari zoezi hilo linaendelea.
Katika hatua nyingine Mushi alipinga madai ya wananachi kuwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umekuwa ukifanya usafi katika mji kutokana na kuwepo kwa ugeni ama vikao kuwa jambo hilo si kweli na kuwa linafanyika kulingana na bajeti na ufinyu wake.
Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Hassan Mtenga alisema kuwa lengo la kuwaweka kitimoto madiwani ni kutaka kukata mzizi wa fitina na kuanzisha utaratibu mpya wa CCM kutekeleza ilani yake pamoja na kupokea kero za wananchi.
Hata hivyo alisema utaratibu huo utaendelea kama njia ya kukiwezesha chama hicho kuweza kupata ushindi wa kimbunga katika chaguzi zijazo.
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi akijibu kero mbali mbali akianza na Hospital ya wilaya ya Iringa mjini alisema kuwa Hospital hiyo imeendelea kutoa huduma .
Huku ujenzi wa barabara za lami katika mji huo kupitia pesa za benk ya Dunia alisema barabara itajengwa kuanzia Samora ,Hospital ya Frelimo , Itamba na maeneo mengine ya mji .
Kuhusu suala la usafi alisema kuwa moja kati ya sababu zilizopelekea mji wa Iringa kutoshika nafasi ya kwanza ni kutokana na hadhi ya makaburi na ndio sababu makaburi ya makanyangio kuanza kuzungushiwa uzio ili siku moja Manispaa ya Iringa iweze kushika nafasi ya kwanza .
Alisema kuwa ni vema suala la maendeleo ya mji wa Iringa lisifanyike kwa itikadi za vyama na badala yake kufanyika kutokana na mazingira yaliyopo .
Kuhusu suala la Stendi ambalo limeendelea kuleta lugha mbali mbali kutoka serikalini na viongozi wa kisiasa alisema kuwa hashangai na kauli za upotoshwaji juu ya ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa ya mkoa itakayogharimu zaidi ya Tsh bilioni 4 fedha kutoka benki ya dunia .
Alisema kuwa mchakato wa ujenzi wa stendi hiyo umeshirikisha wadau wote nyeti hadi mshauri wa mambo ya kimazingira kimataifa na tayari ameifanya kazi hiyo na kutoa maelekezo yake ya kitaalam ambapo ameruhusu ujenzi huo.
Alisema inapojengwa stendi hiyo kutoka ukingo wa mto ni mita zaidi ya 700 wakati sheria ya ujenzi ya Rufiji na Iruwasa ni mita kati ya 50 na 60 hivyo stendi hiyo ipo mbali zaidi kuliko sheria.
Alisema kuwa fedha za ujenzi wa stendi hiyo hata kama Halmashauri ingekusanya isingeweza kupata fedha hizo ambazo hata kama ingekusanya kwa miaka zaidi ya 3 bila kupata .
Alisema kuwa wanaotumia maendeleo kwa ajili ya kutafuta umaarufu katika siasa ni kutowatendea haki wananchi ambao unawatumikia na kuwa suala la uongo halikubariki katika dini zote .
Hata hivyo Mwamwindi alisema jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali ya CCM katika manispaa ya Iringa ni kutaka kuiwezesha Halmashauri hiyo kuja kuwa jiji kama ilivyo Mbeya, Mwanza na Arusha .
Hivyo alisema tayari jitihada mbali mbali za kuwezesha mji wa Iringa kuwa jiji na tayari wamepeleka mradi wa maji Nduli mradi ambao wakati wa kuwekeana saini mbunge wa jimbo la Iringa mjini alipata kushiriki .
“Tumepeleka barabara kutoka Tumaini kwenda Kigonzile KM 6 tumepeleka mabati kwa ajili ya choo mgongo pamoja na kuweka vituo katika eneo la Kigonzile ili kupeleka huduma hiyo kwa wananchi … kwa hiyo ndugu zangu mheshimiwa Mushi amezungumzia barabara ya kutoka Mkimbizi hadi bima kiasi cha mabilioni ya fedha ambazo binafsi sijapata kusaini fedha nyingi kiasi hicho ….sasa tumeanzisha mkakati wa kugawa viwanja na kupasua njia na ninasema kuwa ujenzi wa stendi upo pale pale na suala hili lipo kwa waziri mkuu ambaye ndie mwenye TAMISEMI”

No comments:
Post a Comment