ZANZIBAR, Tanzania
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu
ya taifa ya CCM, imefanya kikao cha siku, Januari 13, 2014 mjini
Zanzibar chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk. Jakaya Kikwete na kujadili mambo
kadhaa ikiwemo kumteua Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa kiti cha
Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.
Taarifa iliyotolewa leo mjini Zanzibar na Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye amesema, mgombea huyu wa CCM kesho, Jumanne, Januari
14, 2013, atachukua fomu za tume za kugombea.
Nape amesema uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014
kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa
Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed
Gharib Bilal.
“Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi”, alisema Nape na kuongeza;
“Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili na Kamati Kuu inawatakia kila lakheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu”.
Nape alisema, pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu pia imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kufanikisha sherehe zake kwa ufanisi kutokana na maandalizi mazuri.
Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

Mwenyekiti
wa CCM, Dk. Rais Jakaya Kikwete, akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM,
leo katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui mjini Zanzibar.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais wa Zanzibar, Dk.
Ali Mohamed Shein na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip
Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. (Picha na Adam Mzee)
No comments:
Post a Comment