Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akihutubia baraza kuu la
madiwani wa Wilaya ya Nkasi (Full Council) lililokua kwenye kikao cha
kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2014/2015 na kupitisha
sheria ndogondogo za halmashauri. Katika hotuba yake aliwataka madiwani
na viongozi wa halmashauri na wilaya ya Nkasi kushirikiana kwa pamoja na
kuweka pembeni itikadi zao katika kuunda vyanzo vipya vya mapato na
kuvisimamia kwa kuwekeana mikakati maalum ya makusanyo kwa kila kijiji,
kata, tarafa, halmashauri na Wilaya kwa ujumla. Alisema halmshauri hiyo
haitaweza kuendelea kwa kuendelea kuwa tegemezi kutoka Serikali kuu na
badala yake waongeze makusanyo ya ushuru na mapato yasaididie katika
mipango ya kujiendeleza. Kikao hicho kilipitisha bajeti ya Tsh Bilioni
25.4.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akizungumza katika kikao hicho ambapo
alisisitiza juu ya kuboresha na kusimamia upatikanaji wa mapato ya
halmashauri ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia katika kuboresha
miundombinu ya barabara katika Wilaya hiyo ambayo imekua ndio kilio
kikubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa
wa Rukwa Ndugu Albinus Mugonya.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Kimulika Galikunga akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya mambo katika kikao hicho. Katikati ni Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Ndugu Peter Mizinga.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment