Kuna taarifa inayosambazwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS) kuhusiana na TMA kutoa tahadhari ya Tsunami
Taarifa hizo sio za kweli, uionapo ujumbe huu upuuzie kwa kuwa sio taarifa sahii, ni taarifa ya upotishaji
Taarifa rasmi ni kama ilivyotolewa awali kuhusiana na upepo mkali kwa Ukanda wa Bahari ya Hindi na Mvua kubwa.
Ujumbe huo unasomeka kama hivi:
TAHADHARI ya Tsunami: Kuanzia saa moja usiku
Tsunami itafika Tanzania na mawimbi yatakuwa makubwa
kuanzia muda huo. Taarifa zaidi itatolewa na Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania wakati wowote kuanzia sasa, kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi.

Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa ili kutoa taarifa sahihi ni
vizuri kuwasiliana na Ofisi zetu kwa maelezo ya kina zaidi kuepusha
mkangamanyo kwa wananchi
Asante tena kwa ushirikiano wako,
Nakutakia Sikukuu njema ya Maulid,
Monica Mutoni
Ofisi ya Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
No comments:
Post a Comment