Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohammed Jiddawi na Dk. Peter McGovern wakitia
saini makubaliano ya kuanzisha huduma za Aya ya magonjwa ya akili
katika Hospitali ya Makunduchi. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dk.
Sira Ubwa Mamboya akishuhudia utiaji saini katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
………………………………………………………………………………….
RAMADHANI ALI/MAELEZO ZANZIBAR
Wizara ya Afya
ya Zanzibar imetiliana saini mkataba wa makubaliano wa kuanzishwa kwa
majaribio kutolewa huduma za maradhi ya afya ya akili katika Hospitali
ya Makunduchi iliyoko Mkoa wa kusini Unguja.
Uwamuzi wa
kuifanya Hospitali ya Makunduchi kuanzisha huduma hiyo inatokana na
mapendekezo ya Wizara ya Afya ya mwaka 2008 na taarifa ya Afya ya
akili Zanzibar ya Jumuia ya Ulaya.
Wadau watatu
wanashirikiana katika mpango huo ambao ni Hospitali ya Chuo Kikuu cha
Haukeland cha Norway, Hospitali ya Afya ya akili ya Kidongochekundu na
Mradi wa kuimarisha Afya Zanzibar.
Katika sherehe
za utiaji saini zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja, Wizara
iliwakilishwa na Katibu Mkuu Dk. Mohammed Jiddawi, Chuo Kikuu cha
Haukeland kiliwakilishwa na Dk. Ingavr Bjelland, Dk. Peter McGovern
alitia saini kwa upande wa Mradi wa kuimarisha Afya kijiji cha
Makunduchi na Dk. Khamis Othman alitia saini kwa upande Hospitali ya
Kidongo Chekundu.
Wadau hao watatu
watashirikiana katika kuimarisha kujenga uwezo huduma za maradhi ya
Afya ya akili kwa visiwa vya Unguja na Pemba, kuanzisha mtaala wa
kufundisha masomo ya afya ya akili wafanyakazi wa Hospitali ya
Makunduchi kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani (WHO) na kuunga mkono
maendeleo ya mafunzo yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya
Makunduchi na Hospitali ya Kidongo chekundu.
Katika hatua za
awali zitakazoanzia mwaka huu, kliniki ya afya ya magonjwa ya akili ya
Hospitali ya Mkunduchi itasimamiwa kwa kiasi kikubwa na Hospitali ya
Kidongo chekundu na mafunzo yatatolewa katika mwaka wa kwanza wa
kuanzishwa huduma katika Hospitali hiyo.
Hatua ya pili
ya mpango huo itakayoanza mwezi Januari mwakani ambapo kliniki hiyo
itakuwa imeimarika na Hospitali mama ya Kidongo chekundu kuridhika na
hatua iliyofikia, Hospitali hiyo itaruhusiwa kujiendesha yenyewe katika
masuala mbali mbali ya uongozi na tiba.
Kwa mujibu wa
makubaliano hayo Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland itasimamia na
kuimarisha mitaala ya elimu ya magonjwa ya Afya ya akili kwa wafanyakazi
wa Hospitali ya Makunduchi ikiwemo kusimamia mafunzo hayo.
Wadau wote kwa
pamoja wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha huduma za magonjwa ya
afya ya akili katika kliniki ya Makunduchi kwa mujibu wa misingi ya
Shirika la Afya Duniani.
Hospitali ya
Makunduchi itakuwa ni ya pili kutoa huduma za magonjwa ya Afya ya
akili kwa kisiwa cha Unguja na kwa Kisiwa cha Pemba huduma hiyo bado
inaendelea kutolewa katika Hospitali ya Chake Chake tu.
No comments:
Post a Comment