Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya
Namibia (Brave Warriors) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya
kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco.
Stars
na Brave Warriors zitacheza mechi hiyo Machi 5 mwaka huu jijini
Windhoek, Namibia. Mechi hiyo ipo katika kalenda ya mechi za kirafiki za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
Makubaliano
ya kucheza mechi hiyo yamefikiwa kutokana na mazungumzo kati ya Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Rais wa
Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA), John Muinjo.
Benchi
la Ufundi la Brave Warriors linaongozwa na kocha mzawa Ricardo
Mannetti, na mechi hiyo itachezwa ama Uwanja wa Sam Nujoma au Uwanja wa
Uhuru jijini Windhoek.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inafundishwa na kocha
Kim Poulsen kutoka Denmark na inatarajia kuanza kucheza mechi za mchujo
za AFCON Septemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment