Na Francis Godwin Blog CHAMA Cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa mjini kimesema kimejipanga kwa nguvu zote kuhakikisha mbunge wa jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa anaachia jimbo hilo hata kama hataki ikiwa ni pamoja na wiki tatu kwa mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi kufuatilia kero mbali mbali za wananchi ikiwa ni pamoja na kujua kiasi cha Tsh milioni 15 zinazotolewa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya jimbo hilo kama zinatumika vema . Mbali ya hilo pia kufuatilia huduma zinazotolewa katika vituo vya afya Hospital na Zahanati kama zinafanyika kwa ubora ama zinafanyika kwa kuwanyanyasa wananchi. “Ushindi wa Msigwa jimbo la Iringa mjini ulitokana na CCM wenyewe ila sasa tunasema kamwe hatutarudia makosa yaliyojitokeza ni lazima turudishe jimbo na Msigwa fedha zake azitumie vema asijaribu kuingia katika ubunge tena”
katibu
wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga aliyasema hayo juzi wakati wa
mkutano wake wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa toka
alipohamishiwa wilaya ya Iringa mjini akitokea Hai mkoani Kilimanjaro
Alisema
zama za ubunge wa Mchungaji Msigwa katika jimbo la Iringa mjini
umekwisha na sasa atake ataondoka na asipotaka ataondoka. “Mwambieni mbunge Msigwa wakati wa kuwadanganya wananchi umekwisha na lazima sasa awaeleze wananchi wa jimbo la Iringa mjini wapi anapelekea fedha za mfuko wa jimbo ambazo zinatolewa kila mwezi na Rais Jakaya Kikwete” Hata hivyo alimuagiza meya kupambana ili fedha kiasi cha Tsh milioni 15 zinazotolewa na rais Kikwete kuona zinafanya kazi gani katika ofisi ya mbunge pia kutembelea Hospital na vituo vya afya ili kuona changamoto mbali mbali ndani ya wiki tatu kupeleka majibu katika ofisi yake. Kuhusu kupanda kwa gharama za umeme ni matokeo ya Dr Slaa ambae alipigia kelele suala la Richmond na Dowans ambapo baadhi ya wabunge waliunga mkono suala hilo ila leo baada ya mambo kuwa magumu tunalalamikia suala hilo ambalo waasisi wake ni Chadema kuleta kwele . Alisema kuwa tunahitaji vijana kuleta maendeleo ya mji wa Iringa na sio vijana wa kutumiwa kuvuruga maendeleo ya mji wa Iringa. ” Nawaombeni wananchi kuwa tayari tumemshika pua mbunge Msigwa na naomba wananchi tusaidiane kumnywesha panado na ninamuomba Msigwa fedha za kiinua mgogo zake asije tena katika jimbo la Iringa mjini atumie kwa kazi nyingine ….tumeanza mkakati huu kwa ajili ya kumnyoa Msigwa “ Katika mkutano huo wananchi walipewa nafasi ya kuwaweka kitimoto madiwani wao ili kujibu kero mbali mbali za katani kwani huku wananchi wa jimbo hilo la Iringa mjini wakikitaka chama hicho kusaidia kukinusuru chama na kura za chuki kutokana na shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) kuendelea kupandisha gharama za umeme. Wananchi hao walisema kuwa ili CCM jimbo hilo na Tanzania kwa ujumla kiweze kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ule wa serikali za mitaa utakaofanyika mapema mwaka huu ni lazima gharama za umeme ishuke
Kwani
walisema kuwa hatua ya TANESCO kuendelea kuongeza bei ya umeme
ni kuongeza ugumu wa maisha kwa watanzania na kuwa ushindi wa CCM
utatokana na utetezi wa chama katika kuwaondolea mzigo wa bei ya
umeme watanzania.
Mbali
ya hilo pia wananchi wa kata ya Kihesa walimbana diwani wao Bw
Mussa Wanguvu kutokana na hatua ya kushindwa kupigania wananchi
ambao wanatakiwa kuvunja nyumba zao ambazo zimejengwa katika eneo
la Semtema Majengo mapya eneo ambalo halitakiwi kisheria
Diwani
Wanguvu akijibu swali hilo alisema kuwa eneo hilo lilizuiwa baada
ya kufanyika kwa mkutano wa hadhara hasa wale ambao wamejenga
katika mlima na wapo hatarini kuangukiwa na mawe ila baadhi ya maeneo
ambayo si rasmi ni waliachiwa .
Kwa
upande wao wananchi wa kata ya Mtwivila walimtaka diwani wao Bw
Victor Mushi kueleza ni lini atatekeleza ahadi yake ya zahanati na
ubovu wa barabara katika eneo la Mkimbizi pamoja .
Kwa
upande wake diwani Mushi kuhusu suala la ujenzi wa kituo cha
afya alisema kuwa ahadi hiyo haikuwa ya kwake ila ilikuwa katika
ilani ya CCM japo alisema ujenzi wa mradi huo upo mbioni baada
ya kumaliza miradi ya zamani utaanza mradi huo wa ujenzi wa kituo
cha afya.
Kuhusu
barabara alisema kuwa kata hiyo wamejitahidi kutengeneza mifereji
na zaidi ya Tsh bilioni 1.8 zitatengeneza barabara ya lami kutoka
Mtwivila kwenda Mkwawa na tayari zoezi hilo linaendelea.
Katika
hatua nyingine Mushi alipinga madai ya wananachi kuwa uongozi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umekuwa ukifanya usafi katika
mji kutokana na kuwepo kwa ugeni ama vikao kuwa jambo hilo si kweli
na kuwa linafanyika kulingana na bajeti na ufinyu wake.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pia aliweza kueleza kazi
mbali mbali alizozifanya katika jimbo la Iringa mjini ikiwa ni pamoja na
kujenga kituo cha polisi kwa gharama zake eneo la Tumaini na kuwa
ataendelea kuchonga sana juu ya kero za wananchi wa Iringa mjini.
Kabati alisema kuwa kamwe hatarudi nyuma katika utendaji na kuwa siku
zote atawapigania wananchi wa jimbo la Iringa mjini na kuwa kuwa siku
zote kwake atahakikisha anatenda zaidi.
Mstahiki
meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi akijibu kero mbali mbali
akianza na Hospital ya wilaya ya Iringa mjini alisema kuwa Hospital
hiyo imeendelea kutoa huduma .
Huku
ujenzi wa barabara za lami katika mji huo kupitia pesa za benk ya
Dunia alisema barabara itajengwa kuanzia Samora ,Hospital ya Frelimo ,
Itamba na maeneo mengine ya mji .
|
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, January 15, 2014
CCM IRINGA MJINI CHAMVAA MBUNGE MSIGWA CHADAI AJIANDAE KUNG’OKA UBUNGE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment