WANACHUO
wa Chuo kikuu cha St,Joseph tawi la Songea wamegoma kuingia madarasani
na kutoka kufanya shughuli za aina yeyote ndani ya chuo hicho huku
wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa jumbe mbalimbali zikiwemo
zilizoandikwa wamechoka kunyanyaswa na wakufunzi ambao wengi wao raia
wa India baada ya uongozi wa serikali ya wanachuo kutimuliwa nyadhifa
zao na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita.
Kundi la waandishi wa habari wa mjini Songea mara tuu baada ya kupata
taarifa ya tukio hilo walifika kwenye eneo la chuo kikuu cha St,Joseph
kilichopo eneo la Luhuwiko mjini Songea ambako walishuhudia maandamano
makubwa ya wanafunzi wakiwa wamebeba mabango yaliyo ujumbe
mbalimbali ikiwemo ya wamechoka kunyanyashwa na wakufunzi ambao ni
wahindi.
Pia wanachuo hao walishuhudiwa wakiimba nyimbo mbalimbali zenye ujumbe
wamechoka kunyanyashwa kwani wao ni watu wazima hapaswi kulinganishwa
na wanafunzi wa shule za msingi au sekondari huku wimbo mwingine ukiwa
na ujumbe kama siyo mwalimu Nyerere kuleta amani wahindi msingefika
kwetu kufanya biashara.
Kufuatia
mgomo huo ililazimika askari polisi kufika kwenye eneo hilo huku
wakiwa wamebeba silaha kwa lengo la kutuliza gasia ambao walitawanywa
katika maeneo mbalimbali ya chuo lakini wanachuo waliendelea na
maandamano yao huku wakiimba nyimbo za kushinikiza uongozi wa chuo
uwarejeshe viongozi wa serikali ya wanachuo kwa sababu ya kutetea haki
za wanachuo ambazo walizodai wahidi hao wamekuwa wakizikiuka.
Wanachuo hao ambao walidai kuwa malalamiko yao walishayafikisha kwa
mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Saidi Mwambungu wakidai kuwa hali ya mazingira ya
chuo hicho siyo manzuri lakini bado wahindi hao wameendelea na vitendo
viovu licha ya mkuu wa mkoa kuwaangiza kuwa waache kuunyanyasa uongozi
wa serikali ya chuo na wayaweke vizuri mazingira ya chuo hicho ikiwa
ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo ambavyo vimesababisha baadhi
ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu na wayaweke vizuri
mazingira ya chuo hicho ikiwa ni pamoja na kufanyia matengezo ya vyoo
ambavyo vimesababisha baadhi ya wanachuo kwenda kujisaidia polini.
Walisema kuwa chuo hicho kinavyoo vyenye matundu 14 ambapo kati ya
matundu hayo saba ya wanawake na saba ni wanaume wakati chuo hicho
kinawachuo zaidi ya 1,200 na kufanya kusababisha tundu moja kutumiwa na wanachuo 64 badala ya kati 20 au 25.
Kwa upande wa viongozi wa serikali ya wanachuo waliyotimuliwa Aristides
Munjwahuzi
na waziri mkuu wake Deogratius Sanga waliwaambia waandishi wa habari
kuwa matatizo makubwa yaliyopo ndani ya chuo hicho ni mengi ambayo
wanachuo wakijaribu kulalamika kupitia uongozi wa serikali ya wanachuo
badala yake uongozi wa chuo umefikia kuufukuza uongozi wa serikali ya
chuo na kuwasimamisha masomo kwa muda wa miezi sita jambo lilionekana
kuwa ni uonevu mtupu.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa chuo hicho mtawa Antonia Emmanuel
alisema kuwa suala la viongozi wa serikali ya wanafunzi la kuvuliwa
madaraka
na kusimamishwa masomo walishapewa maelekezo kuwa malalamiko yao
walete kwa maandishi ili yajadiliwe lakini hawakufanya hivyo jambo
ambalo aliliita kuwa ni dharau na badala yake ameshangazwa kuona
wanachuo wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali lakini amesema
tatizo hilo linahitaji kuwepo mazungumzo ya pande zote mbili yakiwa na
lengo la kumaliza tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment