Wakazi
wa Kijiji cha Ilagala mkoani hapa,wamepatwa na bumbuwazi baada ya kukuta
kaburi limefukuliwa na maiti ikiwa tupu bila sanda.
Tukio
hilo limetokea Januari 14, 2014 katika Kijiji cha Ilagala Wilaya ya
Uvinza mkoani hapa ambapo wakazi hao walistaajabu baada ya kukuta maiti
ikiwa haina sanda.
Shuhuda
wa tukio hilo Abdallah Shaban ambaye ni ndugu wa marehemu ambaye pia ni
Mwenyekiti wa SACCOS ya Mwangu kijijini hapo alisema, marehemu alizikwa
Januari 13, 2014 katika maeneo ya Malalo yaliyopo pembezoni mwa soko la
Ilagala lakini na baada ya hapo walipoenda Januari 14, 2014 kwenye eneo
hilo kwa ajili ya maziko ya marehemu mwingine walishangaa kuona kaburi
limefukuliwa huku maiti akiwa mtupu
Shabani alisema, tukio hilo ni la kwanza kijijini hapo na kwamba kufukuliwa kwa kaburi hilo kunaonyesha kulifanywa na watu.
Naye
baba mdogo wa marehemu, Issa Salum alisema, tukio hilo ni la mwaka
kijijini hapo ambapo polisi wa Kituo cha Ilagala waliamuru kufukua
kaburi lote na kukuta maiti tupu pasipo sanda na waliamua kununua sanda
nyingine na kuzika upya.
Kutokana
na tukio hilo inadaiwa kuwa mama wa marehemu Mwatano Juma alipoteza
fahamu baada ya kushuhudia tukio hilo na baada ya kuzinduka hakuweza
kuongea chochote kutokana na mshangao alioupata juu ya tukio hilo.
Kamanda
mwandamizi msaidizi wa polisi Mkoani hapa, ASCP Frasser Kashai adai
hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo. Marehemu Juma Nkuru Muha
(18), alifariki katika Hospitali ya Maweni akisumbuliwa na ugonjwa wa
mapafu.
No comments:
Post a Comment