Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar
wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani na gari la wazi kwenye
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zamzibar yaliyofanyika leo
yakihudhuriwa na vongozi mbalimbali wa Tanzania na Baadhi kutoka nchi za Afrka Mashariki.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete
akiwapungia mamia ya wakazi wa Zanzibar wakati akiwasili kwenye Uwanja
wa Amani kwenye kilele cha sikukuu ya miaka ya 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na baadhi ya
viongozi waandamizi wa Jeshi kwenye uwanja wa Amani wakati wa
maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.
Maandamano
mbali mbali kutoka kwenye Mikoa na Taasisi za serikali na zisizo za
Serikali yalipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa
Zanzibar na viongozi wengine.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa
wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila
kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kikosi cha Kifaru kinaonyesha kifaru cha kivita.
Vijana wa Halaiki wakionyesha ushiriki wao kwenye miaka 50 ya Mapinduzi “Mapinduzi Daima”.
Kikosi cha Mapinduzi kilichopambana na kuleta Mapinduzi ya Zanzibar
kikipita mbele ya jukwaa kuu na kutoa heshima kwa Rais wa Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein,kwenye kikosi hicho amebaki mwana mama mmoja
anayefahamika kwa jina la Fatma Abdalla Mussa watatu kutoka kulia.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
Picha na Adam Mzee
No comments:
Post a Comment