Mbunge Mgimwa |
MBUNGE
wa jimbo la Mufindi Kaskazin Mahmoud Mgimwa amesema kuwa kuwa
kati ya wabunge wachapakazi yeye ni miongoni na kuwa yeye si mbunge
mzigo kwa jimbo hilo kwani amefanikiwa kutimiza ahadi zake kubwa
zote alizopata kuwaahidi wapiga kura wake.
Akizungumza
katika mahojiano maalum juu ya ahadi alizopata kuwaahidi wapiga
kura wake wakati wa wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010
,Mgimwa alisema kuwa mbali ya jitihada kubwa ambazo amezifanya kama
mbunge katika kutekeleza ahadi mbali mbali ila bado anampongeza
zaidi Rais Dr Jakaya Kikwete ambae alipata kuahidi kuweka lami
katika mji wa Mafinga na tayari lami hiyo imewekwa na kuzidi
kumwongezea heshima kubwa yeye kama mbunge na Chama cha mapinduzi (CCM)
Alisema
kuwa miongoni mwa ahadi ambazo alipata kuzitoa kwa wapiga kura
wake wakati wa kampeni ni pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu kwa
maana ya barabara ya Mafinga – Madibila ambayo tayari imefanyiwa
matengenezo na ipo katika orodha ya barabara zitakazowekwa
lami,pamoja na ahadi za elimu ,afya ,maji ambazo zote zimefanyiwa
kazi.
Hivyo
alisema iwapo asingefanikiwa kutekeleza ahadi zake ambazo aliwapa
wapiga kura wake asingekuwa na haja ya kuendelea kuutaka ubunge
wa jimbo hilo ila kwa kuwa sehemu kubwa ya ahadi amepata kutekeleza
ni wazi kuwa yeye si mbunge mzigo hivyo bado ana uwezo wa
kuendelea kuwaongoza wanananchi wa jimbo hilo.
Mbunge
Mgimwa alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wameendelea kuwa na
ushirikiano mzuri katika kujituma kufanya kazi na kuwa imani
ambayo wananchi hao wameendelea kuionyesha kwake imezidi kumpa
nguvu zaidi ya kuwatumikia na kuwaomba kuendelea kujituma zaidi.
No comments:
Post a Comment