Meneja
Mradi wa Kampuni ya TanzaniteOne Bw. Erenet Emmanuel Mtawali (mwenye
kofia nyekundu) akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kusafisha
na kuzalisha madini ya Tanzanite (haupo pichani) unavyofanya kazi.
………………………………………………………………………..
Ujumbe
wa Algeria umepata nafasi ya kutembelea machimbo ya Tanzanite Mererani
katika Kampuni ya TanzaniteOne ambapo walitembelea sehemu mbalimbali
ikiwemo za uzalishaji, usafishaji, na uchongaji madini ya Tanzanite.
Vilevile, wakiwa Mkoani Kilimanjaro walipata fursa ya kutembelea Kiwanda
cha kuzalisha mbolea ya kupandia cha Minjingu ambapo walijionea namna
mbolea hiyo inavyozalishwa kwa kutumia masalia ya ndege aina ya Flamingo
waliokuwepo eneo hilo miaka mingi iliyopita. Aidha, ujumbe huo ulipata
fursa ya kutembelea mbuga za wanyama katika bonde la ngorongoro ambapo
wamehitimisha ziara yao nchini ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na
nchi ya Tanzania katika sekta za gesi, mafuta,umeme na madini.
Kamishna
wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Sameja akiuongoza ujumbe
wa Algeria kuondoka katika uwanja wa ndege wa Arusha , mara baada ya
kumaliza ziara Mkoani humo.
Mtaalamu
wa madini katika machimbo ya Kampuni ya TanzaniteOne Mererani Bw.
Damian Mansala akiueleza ujumbe wa Algeria namna mitambo ya kupeleka
wachimbaji ardhini na namna mtambo huo unavyosafirisha mchanga wa madini
uliochimbwa na kuusambaza katika hatua mbalimbali za uzalishaji wa
madini ya Tanzanite. Mkurugenzi
Mkuu wa Migodi katika Wizara ya Nishati na Migodi ya Algeria Bw.
Bourroudj Mohamed Tawar (aliyenyoosha mkono) akiangalia mwamba
uliotokana na masalia ya ndege aina ya flamingo, yanayozalisha Mbolea ya
kupanda ya Minjingu. Mwenye koti jeupe ni Mkuu wa uzalishaji wa
kiwanda cha Minjingu Bw. Inyana Mwambete, katikati ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda hicho Bw. Tosky Hans na wa kwanza kulia ni Kamishna
wa Madini Wizara ya Nishati na Madini Bw. Ally Samaje.
No comments:
Post a Comment