MALINZI KUTEMBELEA KITUO CHA ALLIANCE
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafanya
ziara ya siku moja kutembelea kituo cha mpira wa miguu wa vijana cha
Alliance cha jijini Mwanza.
Lengo
la ziara hiyo ni kuangalia jinsi Alliance inayoendesha shughuli zake
ili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liweze kushirikiana na
kituo hicho kwa karibu.
Rais
Malinzi katika ziara hiyo atakayoifanya keshokutwa (Januari 15 mwaka
huu) atafuatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu kwa Vijana,
Ayoub Nyenzi na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ramadhan Nassib.
Alliance
inatarajia kufanya mashindano yatakayoshirikisha vituo vyote vya
kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana (academy) wiki ya tatu ya Februari
mwaka huu jijini Mwanza.
Mashindano
hayo yatashirikisha timu za umri wa miaka 13, 15 na 17 ambapo Alliance
itagharamia malazi, chakula na usafiri wakati timu hizo zikiwa jijini
Mwanza.
RAMBIRAMBI MSIBA WA MCHEZAJI BONIFACE NJOHOLE
Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Boniface Njohole
kilichotokea jana (Januari 12 mwaka huu) mkoani Morogoro.
Njohole
ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ufundi na Mashindano ya Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) hadi umauti unamkuta anatarajia
kuzikwa kesho (Januari 14 mwaka huu) kijijini kwao Mngeta wilayani
Ifakara.
Msiba
huu ni mkubwa kwa jamii ya mpira wa miguu kwani alitoa mchango akiwa
mchezaji, kocha na kiongozi kwa nyakati tofauti, hivyo mchango wake
tutaukumbuka daima.
TFF
tunatoa pole kwa familia ya marehemu Njohole, klabu ya Reli na MRFA na
kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba huo mzito. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya
marehemu kama rambirambi zake.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina
YAHYA KUFUNGA SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Hamad Yahya atakuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa
semina ya waamuzi na makamisha.
Semina
hiyo ya siku mbili itafungwa kesho (Januari 14 mwaka huu) saa 4 asubuhi
kwenye ukumbi wa mikutano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi
zaidi ya 100 na makamishna 50 wanashiriki katika semina hiyo.
Makamishna hao ni baadhi ya wale wanaosimamia mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Kwa upande wa waamuzi ni wale wa daraja la kwanza (class one) ambao ndiyo wanaochezesha mechi za VPL na FDL.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kuandaa semina nyingine
baadaye mwaka huu kwa makamishna wapya wanaotaka kusimamia mechi za VPL
na zile za FDL.
VITAMBUSHO KWA WAANDISHI WA MPIRA WA MIGUU
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa vitambulisho vipya kwa
waandishi wa habari za mpira wa miguu kwa ajili ya kuripoti mechi
mbalimbali inayoziandaa na kuzisimamia.
Kila
chombo cha habari kupitia Mhariri wake au Mhariri wa Michezo kinatakiwa
kuwasilisha majina ya waandishi wake kwa barua maalumu ya ofisi pamoja
na picha (soft copy) kwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Orodha ya majina ya waandishi wakiwemo wapiga picha wanaoombewa vitambulisho hivyo iwekwe kwa umuhimu.
No comments:
Post a Comment