|
Mwenyekiti wa Kamati ya kufatilia
malalamiko ya wananchi wa mji mpya relini Bw. Omari Msusa kushoto
akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu fidia wanayotakiwa kulipwa huku
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Dar es Salaam, Bi,Eugen Mwaiposa akimsikiliza
kwa makini (Picha na Mpiga Picha Wetu) |
|
Mbunge wa jimbo la Ukonga Dar es
salaam, Bi,Eugen Mwaiposa (kulia) akisikiliza malalamiko ya wananchi wea
eneo la Mji Mpya Relini jimboni kwake jana wakilalamika kutaka kulipwa
fidia ndogo ambazo hazilingani na thamani ya nyumba zao (Picha na Mpiga
Picha Wetu) |
|
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Mjipya Relini,Ilala Dar es Salaam Bw. Geofrey Chacha (aliyesimama)
akitoa malalamiko ya wananchi mbele ya mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bi.
Eugen Mwaiposa wa pili kushoto wanaolalamikia kuhusu tahmini ya fidia
ndogo inayopitishwa ili kupisha upanuzi wa bomba la gesi linalotoka
Mtwara. (Picha na Mpiga Picha Wetu) |
|
……………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
WANANCHI wa Mji mpya Relini wilaya ya Ilala waliopitiwa na
mradi ya bomba la gesi ya Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Ukonga,
Bi. Eugen Mwaiposa awasilishe bungeni hoja ya kukataa mradi huo kutokana
na kupunjwa fidia ya nyumba na mali zao wanayotakiwa kulipwa.
Wakizungumza na kutoa maazimio hayo katika mkutano wa
dharura walioitisha na kuhudhuriwa na mbunge wao, wananchi hao walisema
awali walikubali mradi huo kwa manufaa ya taifa lakini baada ya kuletewa
dodoso la kutathmini mali na nyumba zao wamegundua kuna ujanja
unatumika kuwanyima haki na kuwafanya kuwa masikini maisha yao yote.
Waliendelea kudai kuwa mpaka sasa hawajui serikali
imemkabidhi nani jukumu la kuthamini nyumba zao kwani kampuni nyingi za
ujanja ujanja zimejitokeza kutaka kuwathamini lakini kwa kiwango cha
chini ambacho hakiwezi kumpatia makazi mengine.
Bw. Josephat Haule alisema waathirika wenzao katika Kata za
Kivule, Pugu Kwalala na Mbande wao wamethaminiwa vizuri na wanatarajia
kupata fedha za kujenga nyumba nyingine kutokana na gharama kuwa juu
lakini wao nyumba iliyojengwa kwa sh. mil 57 anathaminiwa alipwe sh.
mil. 11 na nyumba zenye thamani ya sh. mil. 10 wanataka alipwe sh, mil
3.
Bw. Robert Pius alisema kutoka taarifa ya Serikali itolewe
ya kutangaza kupitisha bomba la gesi eneo hilo waathirika wote
walisimamisha uendelezaji wa makazi hayo na kusubiri kupewa haki zao
lakini ni mwaka wa pili sasa hakuna taarifa zenye ukweli zinazowafikia
hivyo kuwafanya waishi kama wanya aina ya digidigi porini,
Mbunge Mwaiposa akizungumza na wananchi hao aliahidi
kushirikiana nao kujua ukweli wa kampuni gani iliyopewa jukumu la
kuthamini nyumba na mali zao kwani anachofahamu ni kuwa Kampuni ya Kilwa
Energy iliyopewa jukumu hilo awali hakiwa na uwezo wa kifedha kuwalipa
wananchi kwa wakati.
Aliahidi kushirikiana na Kamati ya wananchi hao
kushughulikia madai yao kwenda Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
kwenda kumuona Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, kwenda
kumuona Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ikishindikana wanakwenda
kumlalamikia Rais Jakaya Kikwete.
Alisema wananchi wanateseka kwa vile kuhamisha makazi kutoka
sehemu moja kwenda nyingine kunarudisha maendeleo nyuma na kama
anavyofahamu Serikali ya Rais Kikwete ni sikivu na yenye kufanya kazi
kwa ufasaha hajui sababu za wananchi wake kushindwa kutimiziwa ahadi zao
katika kiwango kinachostahili.
“Wananchi wangu wanadhiki, wanashida ya fedha lakini si kwa
malipo kidogo kiasi hicho, tunapiga picha tuoneshe umma thamani ya
nyumba na kiasi wanachotakiwa kulipwa ili wakaendelee na maisha yao
sehemu nyingine” alisema Bi. Mwaiposa.
Bi. Mwaiposa alikiri kuona
nyumba zilizothaminiwa kwa fedha kidogo ambazo haziwezi kununua kiwanja
kingine ambavyo kwa sasa katika maeneo hayo vinauzwa kati ya sh. mil. 10
mpaka sh. mil. 15 kwa kiwanja cha nusu hekari.
No comments:
Post a Comment