Madiwani wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo
la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kushoto) kukata utepe wakati wa hafla
ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa
katika Shule za msingi katika Kata 13 za jimbo hilo. Hafla hiyo
imefanyika leo Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi
madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika shule
zilizopo katika Kata 13 za Jimbo hilo. Madawati hayo yaliyonunuliwa kwa
fedha za Mfuko wa Jimbo yalikabidhiwa kwa madiwani wa Kata hizo katika
hafla iliyofanyika Chuo cha Ufundi Chang’ombe, Dar es Salaam
Naibu Meya wa wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga akitoa shukurani kwa Mbunge Mtemvu kutoa madawati hayo.
Naibu
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Zena Mgaya akimpongeza
Mtemvu kwa juhudi za kuinua kiwango cha elimu wilayani Temeke.
Ofisa
Elimu wa Shule za Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba akieleze
furaha ya kupata madawati hao 500 yatakayopunguza tatizo la madawati
wilayani Temeke.
Mtemvu akiangalia wakati mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiandika jina lake.
Mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa
shukurani kwa Mtemvu kwa niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati
hayo
Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yalitotengenezwa VETA Chang’ombe
No comments:
Post a Comment