Kamishna
wa Polisi jamii nchini, CP Mussa Alli Mussa, akitoa neno mbele ya
askari na maofisa katika kikao cha utendaji kazi kilichofanyika jana
jijini Dar es salaam(picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi )
…………………………………………………………………..
Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Na Demetrius Njimbwi na Alexander Mpeka, Jeshi la Polisi
Kamishna wa Polisi Jamii Nchini,
(CP) Mussa Alli Mussa, amewataka maofisa wa Polisi pamoja na askari kote
nchini, kuhakikisha wanafanya kazi zao katika misingi ya uwazi na
usasa, dhana itakayosaidia uenezi wa Polisi jamii/ulinzi shirikishi
katika kupambana na matukio ya uhalifu na wahalifu.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati
alipokutana na baadhi ya watendaji wa Jeshi la Polisi katika wilaya ya
kipolisi ya Ilala, katika kikao cha pamoja kuhusiana na utendaji wa
Polisi katika dhana ya Polisi jamii na namna ambavyo Jeshi hilo
linavyoweza kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa pamoja na kushirikiana
na wananchi na jinsi wanavyoshirikishwa.
Kamishna Mussa, aliongeza kuwa,
tangu kuanzishwa kwa Polisi jamii/ulinzi shirikishi, mafanikio makubwa
yameweza kufikiwa kwani mpaka sasa makundi kadhaa ya uhalifu yameweza
kugundulika na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuangamizwa ikiwa pamoja na
wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria, alisema.
Hata hivyo, Kamishna Mussa,
aliwataka wananchi kuwathamini na kuwapa ushirikiano maofisa wa
Polisi/Polisi Kata pamoja na vikundi vya Ulinzi Shirikishi hatua ambayo
itasaidia kukabiliana na matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali na
kuifanya jamii kuishi kwa amani pasipo kuwepo kwa matukio hatarishi.
Kwa upande wake, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Lazaro Mambosasa, alisema kuwa, Jeshi l
Polisi limejipanga katika kukabiliana na aina zote za uhalifu na kwamba
alitamuonea ama kumdhurumu mtu yeyote katika kusimamia na kulinda
usalama wa raia na mali zao.
Mambosasa, ameongeza kuwa, kila
askari katika nafasi yake anawajibu wa kuhakikisha kuwa, jamii
inaondokana na uhalifu pamoja na matishiona huku akiwataka maofisa na
askari kuwa na utayari katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa
kuzingatia dhana ya Polisi Jamii/Ulinzi shirikishi, alisema.
No comments:
Post a Comment