Pichani
washiriki wa mafunzo ya namna ya kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia
na unyanyasaji wa watoto wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Kamishna wa
Polisi (DCP) Adolfina Chialo, wakati wa kufuata mafunzo ya kutambua
makosa ya ukatili wa kijinsia na watoto, yaliyofanyika mkoani Morogoro,
mafunzo hayo yaliwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa
ya Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji mkoa wa Morogoro.( Picha na
Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi )
…………………………………………………………………………
Na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi
Mkuu wa Dawati la Jinsia na
Watoto Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amewataka
wananchi kote nchini, kutofumbia macho vitendo vya ukatili na
unyanyasaji ambavyo vimekuwa vikitokea katika jamii yetu huku vikiathiri
idadi kubwa ya wanawake na watoto.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati
akifunga semina ya mafunzo kwa askari Polisi ya namana ya kutambua
viashiria vya makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto,
mafunzo yaliyofanyika kwa muda wa siku tano katika mkoa wa Morogoro,
huku yakiwakutanisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya
Dodoma, Pwani pamoja na wenyeji wa mafunzo hayo mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo, Kamishna Chialo,
alisema kuwa, lengo la mafunzo haya kwa askari na maofisa wa Jeshi la
Polisi, ni kuwajengea uwezo katika kutoa huduma bora katika kazi za
dawati la jinsia na watoto, ikiwa pamoja na kufahamu mbinu mbalimbali za
kutambua makosa ya ukatili wa kijinsia huku wakitambua kuwa suala la
utoaji wa huduma bora kwa mteja si hiari bali ni lazima.
Naye kwa upande wake mwakilishi
wa Kituo cha Sheria ( legal Sector) waliofadhili mafunzo hayo, Bi.
Wanyenda, alisema kuwa, Jeshi la Polisi linamchango mkubwa katika
kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia na hivyo kutokana na
mafunzo haya yatawasaidia askari katika kupambana na matukio ya ukatili
wa kijinsia ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitendeka katika jamii.
Bi. Wanyenda, aliongeza kuwa, ni
vyema askari waliopatiwa mafunzo haya wakaitumia fursa hii waliyoipata
kuweza kutoa elimu kwa askari ambao hawakuweza kushiriki katika mafunzo
haya kwa lengo la kuwajengea uwezo na namna ya kutambua viashiria vya
makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji.
Akisoma risala mbele ya mgeni
rasmi kwa niaba ya washiriki wenzake, Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Letea
Mofuga, alisema kuwa, mafunzo waliyopatiwa yamewasaidia kutambua na
kubaini viashiria pamoja na dalili za mtu aliyefanyiwa ukatili na hivyo
kuahidi kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo waliojifunza.
No comments:
Post a Comment