Kikosi cha Timu ya DACICO F.C.(Picha Zote kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania).
=================================
Wanafunzi
wapya wa Vyuo vya Uandishi wa Habari jana wamekaribishwa kwa sherehe na
shamrashamrav mbalimbali kutoka Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha
Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City Collge(DACICOSTUA) kwa
kushirikiana na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Mlimani Profesional
vyote vya jijini Dar es Salaam, ambao waliandaa michezo mbalimbali
ikiwemo kuvuta kamba, mashindano ya Urembo, kutunisha Misuli, kuimba,
kucheza, kujibu mada, kuogelea, netball, volleyball katika hafla
iliyofanyika makao makuu ya chuo cha Dacico kibamba chama.
Akizungumza
katika hafla hiyo mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala,
Dacico, Bw. Idrisa Mziray, alisema kuwa lengo la sherehe hizo ni
kuwakaribisha wanafunzi wanaoanza mafunzo kwenye Vyuo hivyo new Intake,
ambao baada ya kuwasili kila muhula ufanyiwa ukaribisho na serikali za
vyuo hivyo kwa lengo la kutakiana baraka na pia kufanya utambulisho wa
viongozi kwa wanafunzi wageni ili kuweza kuendana na utaratibu unaokuwa
umewekwa na bodi ya chuo kwa kuwashirikisha wanafunzi ambao ni viongozi
wa serikali yao.
Aidha
katika Hafla hiyo mapema wanafunzi wa chuo cha Dacico kilichuana na
Mlimani Profesional katika michezo mbalimbali lakini hata hivyo
wachezaji wengi wa Mlimani Profesional walifanikiwa kuibuka washindi
kwenye michezo ya Pooltabl, kuvuta Kamba kabla ya kubwagwa kwenye mchezo
wa Soka kwa kukubali kufungwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na mchezaji
Mathias Haule kwa shti kali mchezo ambao ulifanyika kwenye uwanja wa
Kibamba Chama.
baada
ya mchezo huo hafla hiyo ilikwenda moja kwa moja ukumbini na
kuwakutanisha
tena katika michezo ya pooltabe ambapo wachezaji wa Dacico walionekana
kukabwa koo kutokana na wachezaji wa mlimani profesional kuonyesha
kiwango kizuri katika kulenga na kutumbukiza mipira ukilinganisha na
wenzao wa Dacico pooltable lakini hata hivyo hadi mwisho wa mchezo timu
zote zilitoshana nguvu kwa kufungana michezo miwili miwili lakini Yohana
Dula wa Dacico akiibuka nyota wa mchezo huo kutokana na kushangiliwa
sana na mashabiki waliokuwa wamefurika kushuhudia michezo hiyo.
Kivutio
kikubwa katika hafla hiyo ilikuwa ni mashindano ya Urembo ambayo
yalishirikisha jinsia zote na hivyo kuonekana kuwa kivutio kikubwa kwa
wote waliokuwa wakifuatilia shamrashamra hizo na hivyo kufanya vifijo na
ndelemo kutawala muda wote ususani alipokuwa akikatiza mshindi Ikumbo
Gradman ambaye aliwabwaga wenzake kutokana na kuwa kivutio kikubwa
kwenye mashindano hayo akifuatiwa na Fatuma Said, wakati kwa upande wa
wanaume kivutio kikubwa ilikuwa ni kwa haji juma maarufu kama kaseja
kutokana na umahili wake wa kudaka mipira, wakati shindano la Miss Bantu
lilikosa msisimuko kutokana na washiriki Cecilia Kimaro, Saumu
Ramadhan, Rabia Salum, shamim Juma kushindwa kutokea Uwanjani.
Washindi
wengine katika Michezo hiyo ilikuwa ni pamoja na Kasilima na Grayson
Mgoi walitoshana nguvu baada ya wote kupata kura sawa kutoka kwa
mashabiki waliokuwa wamejaa ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City
College, katika mchezo wa kuimba na kucheza, Happy Mayala kuogelea kwa
upande wa Wanawake huku nafasi ya pili ikienda kwa Mariam Mwakatumbula
na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Vanessa hata hivyo fainal hiyo
ilishindwa kuwa na msisimko kutokana na kiza kuingia na hivyo washiriki
wengine waliokuwa wamejiandikisha kushiriki kushindwa kutokana na muda.
MWISHOOOOOOOOOO
|
No comments:
Post a Comment