Nawaambieni
CHF ndiyo mkombozi wa huduma za matibabu sasa…Mkuu wa wilaya ya Ruangwa
Agnes Hokororo (MB) akitoa rai kwa wananchi wake Wilayani humo wakati
wa uzinduzi wa kampeni za uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF ulioenda
sambamba na upimaji wa afya bure chini ya uratibu wa NHIF Lindi
uliofanyika leo hii kwenye viwanja vya CWT Ruangwa.Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Agness Hokoro hayupo pichani wakati wa uzinduzi huo .
Meneja
wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akiwaeleza wanahabari (hawapo
pichani) namna ya utekelezaji wa zoezi la uhamasishaji wa wananchi
kujiunga na CHF utakavyoendeshwa,sambamba na mafanikio yanayotarajiwa
kutokana na mkakati wa pamoja wa Mfuko na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa
ulivyokusudiwa.
Upimaji wa afya bure ukiendelea,madaktari wa mfuko na hospitali ya
wilaya wameendelea kutoa huduma za uwiano wa uzito wa mwili
(BMI),shinikizo la damu (BP) na sukari ambapo suala la lishe na
shinikizo la damu (BP)ni changamoto iliyoweza kubainika hivyo ushauri
ulitolewa,kushoto ni Dr. Rashida Omari wa hospitali ya wilaya akimpima
kiwango cha sukari mzee Abdalah Ngawenje.
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Agnes Hokoro (MB) akipima BMI kwenye viwanja vya
CWT,anayempima ni afisa wa mfuko ofisi ya mkoa wa Lindi Laurent Hoja
No comments:
Post a Comment