Na Magreth Kinabo – Maelezo
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka Watanzania kuongeza juhudi za kuzuia maambukizi ya Virusi
Vya
Ukimwi(VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ili katika Tanzania
iweze kuwa na kizazi kisichokuwa na VVU na ugonjwa wa Ukimwi.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) wakati akifungua mkutano wa
kitaifa wa wadau wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
Aidha
mama Kikwete aliwataka Watanzania kuchangia sh. 100 katika kupambana na
tatizo kwa mchango utawapa nguvu wadau wengine kuwaunga mkono.
Aliwataka wadau wamaendeleo kuendele kuunga mkno katika juhudi za kuondokana na tatizo hilo.
“
Lazima juhudi za makusudi zifanyike bila kuchoka kwa maeneo yote
Serikali, NGO’s, taasisi za dini mashirika ya kiraia na watu binafsi .
Hii itasaidia kunusuru kizazi chetu na kuwa na nguvu kazi iliyobora,
kizazi kisichokuwa na maambukizi na VVU na Ukimwi,” alisema Mama Kikwete
huku akisisitiza Tanzania bila Ukimwi inawezekana.
Aliongeza
kuwa mikakati imara na endelevu ni lazima iwepo kama vile kutoa huduma
za kuzuia maambukizi ya VVU na Ukimwi kwa kushirikisha jamii na kutoa
tiba kikamilifu zinaweza kupunguza maambukizi hayo.
Alisema
asilimia 98 ya wakina mama wajawazito wanahudhuria kiliniki angalau
mara moja na asilimia 43 mara nne wakati wa ujauzito kati ya hao,
asilimia 81 wanapimwa VVU.
Aliwataka
wakina mama wajazito kuhudhuria kiliniki wakati wa ujauzito kuanzia
siku ya kwanza hadi watakapoajifungua ili idadi ya wanahudhuria
kiliniki iweze kufikia asilimia 100.
Naye
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema hivi sasa
Tanzania imefanikiwa kupunguza maambukizi hayo kwa asilimia 15 mwaka
2012 kutoka asilimia 19 mwaka 2011 na lengo ni kufikia asilimia 5
ifikapo mwaka 2015.
Alisema
asilimia 90 ya wakina mama wajawazito wamepimwa VVU kati yao asilimia
64 wamegundulika wanaishi na VVU , pia asilimia 55 ya watoto wanapatiwa
dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.(ARV’s).
Kaimu
Mkurugenzi wa Kinga kutoka wizara hiyo , Dk .Neema Rusibamayilla
alisema alisema awamu ya pili ya kupambana na tatizo hilo itaanza
Januari mwaka huu katika mikoa mingine 16.
Mratibu
wa huduma hiyo kutoka Malawi, Dk. Michael Eliya alisema ni muhimu
kuweza katika utoaji wa huduma, kuboresha miundombinu ,ikiwemo
rasilimali fedha na watu katika kufanikisha malengo hayo.
======================================================
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. PEREIRA SILIMA AELEZEA MAFANIKIO YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YALIYOFIKIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA NNE, JIJINI DAR
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(katikati) akitoa taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es as Salaam(kulia) ni Kamishna wa Utawala wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve(Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari na Maelezo, Bw. Assah Mwambeni.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwa pamoja na Viongozi Wengine Wakuu wa Idara zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima akitoa taarifa rasmi ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne(wa pili kulia) ni Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylivester Ambokile(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, Pius Nyambacha.
Baadhi ya Wakurugenzi mbalimbali wa Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia kwa makini taarifa ya Mafanikio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne iliyotolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Prereira Silima kwa Waandishi wa Habari leo Januari 21, 2014 katika Ukumbi wa Mikutano, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Jijini Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment