TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 24, 2014

MAWAKALA WA REDIO JAMII WATAJA FAIDA ZA MRADI WA SIDA PANGANI

DSC_0043

Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akisisitiza jambo katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya.
Na mwandishi wetu, Pangani
Mawakala wa redio jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari .
Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika warsha inayowapa uwezo wa kuweka kumbukumbu za kazi zao na vyanzo vya habari kwa kutumia Tehama iliyofanyika Pangani, washiriki hao wamesema mafanikio hayo siyo tu katika taaluma bali pia yamewajenga na kuwaimarisha kimaisha.
Mmoja wa washiriki hao alisema, “kusema ukweli natoa shukrani zangu kwa SIDA na UNESCO kwa kutupatia mafunzo haya kwa sababu mimi binafsi nimeweza kununua kompyuta pakato (laptop) kwa ajili ya kuendeleza niliyoyapa kwa vitendo, na niko mbioni kununua simu za kisasa aina ya ‘tablet’,” alisema Sospether Rugemarila kutoka Fadeco FM redio.
DSC_0105Sehemu ya washiriki wakifutilia kwa umakini mafunzo hayo.
Katika kipindi cha miaka miwili cha mradi huo, mafunzo mbalimbali yametolewa kwa mawakala wa redio jamii kama vile matumizi ya mtandao katika kutafuta habari, mbinu mbalimbali za kupeleka taarifa na vipindi vya redio kupitia mtandao, matumizi ya simu aina ya ‘smartphone’ katika kuripoti taarifa maalum au majanga na matumizi ya mitandano ya kijamii kwa lengo la kuwasiliana, kushirikiana na kubadilishana mawazo, taarifa na vipindi vya redio.
“Sisi baada ya kupata mafunzo ya matumizi ya simu aina ya “smartphone” tulifungua akaunti ya pamoja ya Facebook kwa jina na UMMAREJA kama ulingo wetu wa kubadilishana mawazo, taarifa na masuala mbalimbali yanayohusu ustawi wetu kama mawakala,” alisema mwenyekiti wa umoja huo Msuli Mwaijengo kutoka Kyela FM redio.
DSC_0281Sospeter Rugemarila wa FADECO FM Redio, akizungumzia mafanikio aliyoyapata kutokana na mafunzo ya kuzipa uwezo Redio Jamii matumizi ya Teknolojia mpya katika kukuza upatikanaji na upashaji habari vijijini.
Sabina Nestory ni miongoni mwa mawakala ambao walikuwa na uwezo mdogo sana kabla ya mafunzo haya kuanza. Lakini ila anapohudhuria mafunzo mapya na kiwango chake pia kimekuwa kikiongezeka kiasi cha kumfanya aone umuhimu wa kununua simu aina ya ‘smartphone’ ambayo anasema itamrahirishia kutafuta na kutuma taarifa mbalimbali kwa niaba ya chama cha Umoja wa Wanawake katika Habari na Mawasiliano Sengerema (WAHAMASE) unaomiliki kituo cha Sengerema FM redio.
“Mimi nilipohudhuria mafunzo ya Tehama Ifakara nilikwenda moja kwa moja dukani kununua simu ya ‘smartphone’ ili nione inafanyaje kazi, ninayo, bado naisoma huku nikiendelea kuitumia kwa kuripoti matukio mbalimbali ya vijijini hususan ya maendeleo”.
DSC_0290Peter Marlesa wa Sengerema FM Redio, akielezea jinsi alivyofanikisha kutayarisha makala na vipindi mbalimbali zikiwemo habari za Mahakama na migogoro vijijini.
Mafunzo hayo yameweza kuwapandisha ngazi baadhi ya mawakala kuwa wafanyakazi vituoni baada ya kuonyesha umahiri na ujasiri katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku kama ilivyofanyika Mtegani FM redio, Makunduchi Zanzibar na Sengerema FM, Sengerema Mwanza. Peter Marlesa ni miongoni mwa waliobahatika kupanda ngazi kutokana na umahiri na ubunifu wake katika kuandaa vipindi mbalimbali kwa kujituma.
“Baadhi ya mambo niliyofaidika na mradi ni utayarishaji wa vipindi vya makala ya redio, jarida, vipindi vinavyohusu makundi maalum, habari za mahakamani na migogoro na taarifa za habari. Ni mara ya kwanza katika kituo chetu kuandika habari za mahakamani na maeneo tata vijijini.”
Kwa mara ya kwanza warsha hii ya kuwapa uwezo wa kuweka kumbukumbu imewakutanisha mawakala 25 kutoka redio tisa ambazo ziko kwenye mradi wa kuzipa uwezo redio jamii matumizi ya Tehama ulioanza mwaka 2012 ambao baada ya hitimisho watapitiwa vyeti vya ushiriki. Redio hizo ni Fadeco, Kahama, Kyela, Micheweni, Mtegani, Orkonerei, Pambazuko, Pangani na Sengerema.
DSC_0112Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa maelekezo jinsi ya kufanya mazoezi kwa vitendo.
DSC_0347Sabina Nestory wa Sengerema FM Redio, akionyesha Smart Phone yake aliyoinunua wakati wa mafunzo ili kufanikisha mafunzo ya matumizi ya simu na habari kwa vitendo.
DSC_0268Afisa Mipango Kitengo cha Mawasiliano, Habari na Tehama kutoka UNESCO, Bw. Al Amin Yusuph, akiewaelekeza jambo washiriki namna ya kuhifadhi habari kwa kutumia simu yenye uwezo mkubwa (Tablet).
DSC_0084Programme Assistant wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari kutoka UNESCO, Rosemary Lyamba, akitoa maelekezo kwa washiriki katika warsha ya siku tatu ya kutoa uwezo wa kuweka kumbukumbu ya vipindi na vyanzo vya habari kwa kutumia Teknolojia mpya iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
DSC_0178Picha juu na chini ni washiriki wa warsha hiyo wakifanya mafunzo kwa vitendo kwa kutumia Teknolojia mpya ya TABLET.
DSC_0064
DSC_0263Washiriki wakiwa kwenye kazi za vikundi.
DSC_0400Mshauri na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na mawakala wa Redio Jamii nchini.

TBL YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI MJI MDOGO WA TUNDUMA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya akiongea na wafanyakazi wakituo cha Afya Tunduma mara baada ya kukabidhiwa kisima hicho na TBL
Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo akitoa neno la shukrani kwa TBL

PEAK PERFORMANCE INTERNATIONAL YATOA MAFUNZO YA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Training 1

Mkuu wa mafunzo kutoka Peak Performance International Tanzania Bi Claudine Muthama akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya utoaji bora wa huduma kwa wateja kwa wafanyakazi wa Quality Furniture Limited jana jijini Daressalaam katika hotel ya Accomondia.
Taking notes 1Baadhi ya wafanyakazi wa Quality Furniture Limited wakinuu maneno kutoka kwa mkuu wa mafunzo wa Peak Performance International Tanzania Bi Claudine Muthama ( hayupo pichani) jana katika hotel ya Accomondia jijini Daressalaam.Group photo2Wafanyakazi wa Quality Furniture limited wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mafunzo juu ya utoaji bora wa huduma kwa wateja jana katika Hoteli ya Accomondia. Mafunzo hayo yalitolea na kampuni ya Peak Performance International Tanzania yenye uzoefu wa karibu miaka kumi ya utoaji mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi na watu binafsi
……………………………………………………………..
Peak-Performance-Logo_0
Dar es Salaam, Wafanyakazi wa Quality Furniture Limited jana walipatiwa mafunzo juu ya utoaji bora wa huduma kwa wateja na kampuni ya Peak Performance International Tanzania, PPIT.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika Accomondia  Hotel, mkuu wa mafunzo wa PPIT Bi Claudine Muthama alisema kuwa “ katika dunia ya sasa ya kibiashara ambapo ushindani ni suala la kila siku na wateja wana machaguo mengi ya bidhaa na huduma suala la huduma bora kwa wafanyakazi ni suala mtambuka.”
Aliendelea kusema maneno mazuri kwa mteja yanaweza kufanya huduma yako kusambaa kwa watu wengi zaidi maana watu wana tabia ya kusimuliana. Kwahiyo kama kampuni au mtu binafsi atakosea katika huduma kwa wateja watu hawatajikisikia kurudia biashara na wewe.
Zaidi ya hayo kazi ya huduma kwa wateja inahitaji mtu ambae ni msikivu, mwenye kusoma saikolojia ya mteja kwa haraka pia uvumilivu pale unapopata mteja mgumu kushika maelekezo.
Kwa upande wao wafanyakazi wa Quality Furniture walisifia mafunzo hayo wakisema yamewapa mwanga na kuongeza uelewa wao  katika huduma bora  kwa wateja ambao hawakuwa nayo hapo kabla.
“Mafunzo haya yalikuwa na lengo kubwa la kubadili mitazamo ya wafanyakazi. Tunaamini baada ya mafunzo haya leo kila mmoja wetu amepata nguvu mpya na anaenda kuhakikisha wateja wetu wanaendelea kupata huduma bora.” alisema bwana  Tonny Obura Meneja Mauzo na Masoko wa Quality Furniture.
Peak Performance International Tanzania,  PPIT ni kampuni inayoongoza Tanzania kwa kutoa mafunzo kwa makampuni na watu binafsi juu ya huduma bora kwa wateja, ufanisi kazini, umoja na mshikamano, kutambua uwezo ulioko ndani yako pamoja na mafunzo mengine mengi yenye lengo la kuboresha na kukuza ufanisi kazini na mafanikio kwa ujumla.

RAIS KIKWETE AGAWA MADUME BORA YA NG’OMBE MSOMELA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Msomela wakatia  a lipokwenda kukabidhi madume bora ya ng’ombe kwa wafugaji jana.D92A6820Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madume bora ya ng’ombe na kasha kuwakabidhi baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Msomela wilayni Handeni D92A6872Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mmoja wa wafugaji mwenye asili ya kimasai bwana Shayo Lahoda aliyegawiwa dume bora la ng’ombe katika kijiji cha Msomela wilayani handeni leo(picha na Freddy Maro)

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA NA KAMPENI KATA YA MBWEWE LEO

Sunday, March 23, 2014

Barcelona wapeleka vilio kwa mashabiki wa Real Madrid katika Uwanja wa Santiago Bernabéu, Madrid nchini Hispania.

BARCELONA VS REAL MADRID, IONEL MESSI APACHIKA 3 - NA CHRISTIANO RONALDO 1.

Lionel Messi (kushoto) akishangilia bao lake la tatu na wachezaji wenzake Gerard Pique (katikati) na Alexis Sanchez.

Karim Benzema akishangilia na wachezaji wenzake wa Madrid Angel Di Maria na Marcelo baada ya kufunga bao la pili.
Iniesta baada ya kufunga bao la kwanza akipongezwa na Jordi Alba (kushoto) na Dani Alves (katikati). Pembeni ni Neymar na Messi.
Pepe juu akishangilia pamoja na wenzake wa Madrid baada ya bao la tatu lililofungwa na Ronaldo.
Mashabiki wa Real Madrid na mabango yao.
Inakuwaje! Pepe akimshika tai Fabregas wakati wa mtanange huo. Pembeni ni Neymar.
Sergio Ramos akionyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Neymar.
MSHAMBULIAJI mahiri wa Barcelona, Lionel Messi, usiku huu
 amepeleka vilio kwa mashabiki na wapenzi wa Real Madrid 
baada ya kufunga 'hat-trick' wakati timu yake ikishinda 
bao 4-3 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid.
Mechi hiyo kali ya La Liga imechezwa katika Uwanja wa 
Santiago Bernabéu, Madrid nchini Hispania.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao mawili kwa penalti dakika 
ya 65 na 84 wakati lingine akilifunga dakika ya 42 baada 
ya Andres Iniesta kufunga mapema dakika ya 7. 
Mabao ya Madrid yamewekwa kimiani na Karim Benzema 
aliyetupia
 mawili dakika ya 20 na 24 la tatu likifungwa na Mchezaji 
Bora wa Dunia mwaka 2013/14, Cristiano Ronaldo kwa mkwaju 
wa penalti dakika ya 55

MAMLAKA YA HALI YA HEWA ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MAMLAKA HIYO DUNIANI INAYOADHIMISHWA KILA MWAKA IFIKAPO MARCH 23

Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Hassan Khatib Ame akitoa ufafanuzi wa kitu kwa wanafunzi wa Skuli ya Kombeni walipotembelea Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa iliopo ndani ya Uwanja wa ndege wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyo adhimishwa leo.DSC_0697Afisa Usalama wa Anga Bw. Rashid Omar Mselem akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani kuhusiana na usalama wa Anga na Hali ya Hewa pindi inapokuwa mbaya, katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani.
………………………………..
Na Miza Kona   – Maelezo Zanzibar              
Wanafunzi wa vyuo na sekondari wameitaka jamii kuwa na mwamko wa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa pamoja na kutembelea vituo hivyo ili kuweza kujua na kupata taarifa za mwenendo wa hali ya hewa Nchini.
Kauli hiyo wameitoa leo huko katika ofisi za Mamlaka hiyo ziliopo Uwanja wa Ndege Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani, wamesema jamii imekuwa haina mwamko mzuri katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa nchini.
Wamesema kuwa kila siku jamii inatakiwa kujua na kufuatilia taarifa hizo ili kuweza kufahamu hali ya hewa ilivyo ili kuepukana na majanga na matatizo yanaweza kutokea ambapo mamlaka hiyo hutoa taarifa.
Aidha wanafunzi hao wamewataka wanafuzi wenzao kutembelea katika vituo vya Mamlaka hiyo kwenda kusoma kwa vitendo na kuona shughuli hizo zinavyotolewa.
Wanafunzi hao wametembelea sehemu mbali mbali na kuona jinsi shuguli za kituo hicho zinavyofanyika ikiwepo sehemu ya usalama wa Anga, kipima joto, kipima mvua, kipima upepo, pamoja  utabiri wa hali ya hewa.
Wakitoa maelezo kwa wanafunzi maafisa mbali mbali wa Mamlaka hiyo wamesema kuwa huduma nyingi zinazoendeshwa nchini huwa zinashirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa taarifa za hali ya hewa ili kuendesha kazi zake.
Wamefahamisha Mamlaka ya Hali ya Hewa hushirkiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege jinsi ya kuingia kutoka kwa ndege nchini na namna ya kuwasiliana katika uendeshaji shughuli wa zake.
Aidha wamefahamisha kuwa Mamlaka hutoa taarifa zake kwa kutumia vipimo mbali mbali viliopo nchini vikiwemo kipima ju, kipima upepo pamoja na kipima mvua na kutoa taarifa jamii jinsi ya hali ya hewa ilivo na itakavyokuwa nchini.    
Nae  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mohammed Khamis Ngwali , amesema vijana wanatakiwa kubadilika na kuchukua tahadhari za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye mazingira bora.
Hata hivyo  Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana katika kujihisha na  masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa na hatua za kuchukua katika kipindi cha hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Amesema hatua hii muhimu ikichukuliwa na vijana italeta ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho kwa kujenga jamii iliyo imara baadae pamoja na kuokoa dunia  kwenye majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini.
 Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 23 Machi, kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUTUMIA KALAMU VIZURI KATIKA KIPINDI CHA KUELEKEA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA

Mhadhiri katika Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Dkt. Ayoub Rioba akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) na kueleza kuhusu umuhimu wa Vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika uandaaji wa katiba mpya, Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mwalimu Bashiru Ally akiongea na Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) na kuwaasa kutumia nyenzo zote ikiwamo Rasimu ya Katiba, Hotuba ya Mh. Rais Jakaya Kikwete hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika upatikanaji wa katiba mpya. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari  ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Kingunge Ngombale Mwiru akiongea na waandishi wa habari Hawapo Pichani) na kuwaasa wananchi kuwa na umoja hasa katika kipindi hiki cha upatikanaji wa katiba mpya kwa maendeleo ya Taifa na Wananchi kwa Ujumla. kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari                      ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamaradi Kawawa akieleza jambo kwa Waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) Kwenye Semina Iliyoandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO) kuhusu wajibu wa waandishi wa habari katika kuripoti habari za bunge maalum, Leo Mjini Dodoma.
(Picha na Hassan Silayo)
Posted By Blogger to THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG