TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, November 15, 2014

HABARI ZILIZOTAWALA SIKU YA TAREHE 13 HIZI HAPA JIKUMBUSHE.

VITUKO VYATAWALA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA , MLEVI AFANYA VURUGU KUBWA

Wasanii  wakielezea kifo cha mabovu , Juu ni Msanii Mabovu enzi za uhai  wake
Waombolezaji  wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa
Wasanii wakiwa  wamelipiga chata kaburi la mabovu mara baada ya mazishi yake
Baadhi ya  wasanii wa kundi la Weusi ambao  wamefika  Iringa kumzika msanii Mabovu leo
Makini akichangisha rambi rambi
Msanii JOh Makini akiwa na michango ya msiba wa mwenzao Mabovu leo
Mwakilishi  wa  wasanii wa kundi la Weusi Joh Makini kushoto  akimpa pore baba wa msanii Mabovu mzee Upete kulia baada ya kumaliza kuzika nyumbani kwake Mwangata wengine ni baadhi ya  wasanii  walioshiriki mazishi hayo leo
Mwakilishi wa kundi la weusi kwanza Joh Makini akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima leo
Picha na habari na kikosi cha matukiodaima.co.tz Vituko vyatawala msiba wa msanii Ahmed Zubery Upete a. k. a Geez Mabovu Iringa mlevi (pichani aliyekaa chini)atembeza kichapo kwa wafiwa kisa ataka aruhusiwe kuufukua mwili wa marehemu ili auage Mara ya mwisho asisitiza kuwa marehemu amekua nae na ana siri nzito ya kifo chake.
Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.
Chapombe huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye kufika eneo hilo.
Kutokana na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza  mara  baada ya mazishi hayo  mmoja  kati ya  wadau  wa  tasinia ya muziki nchini na promota mkubwa wa mziki nyanda za  juu  kusini Edwin Bashir ambae ni  mtangazaji  wa  kituo cha  Radio Ebony  Fm alisema  kuwa  mbali ya umoja ambao  wasanii  wameuonyesha katika msiba huo kwa  kuja kushiriki mazishi  ila bado angeshauri  wasanii kwa  wakati mwingine  kujenga ushirikiano wa  kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.
” Sisemi  kwa  ubaya  ila kiukweli  msanii  Geez Mabovu  ameumwa sana karibu mwaka mzima anasumbuliwa na ugonjwa  wake ila hakuna  msanii ambae amefika  kumjulia hali  ila  leo wengi  wamesafiri  kuja kumzika….. inapendeza  kusaidiana  wakati wa ugonjwa badala ya  kusubiri mwenzenu afe “
Bashir  alisema  kuwa msanii  huyo ni  miongoni mwa  wasanii  wa mwanzo zaidi  kuutangaza mkoa wa Iriga katika tasnia ya  muziki na kuwa hata kabla ya vituo vya radio  kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na kusikika katika  radio  mbali mbali za nje ya Iringa.
Alisema  kuwa msanii  huyo toka amemaliza  elimu  yake kamwe  hajapata kufanya  shughuli  nyingine  nje ya mziki na kuwa  wakati  wote  alikuwa akijishughulisha na muziki  zaidi .
Hata  hivyo  alisema chanzo cha Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia makazi yake  jijini Dar es Salaam ni  kuzidi  kuutangaza muziki  zaidi na mkoa wake wa Iringa malengo ambayo alipata  kufanikiwa kwa  kiasi  kikubwa .
” Utaona   jinsi ambavyo  msiba  wake  leo  ulivyowavuta  watu  wegi  wapenzi na wadau wa muziki  kutoka mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa ambao kimsingi  baadhi yao  imekuwa ni mara yao ya kwanza kufika Iringa ….pamoja na kufarijika kwa  umati wa  watu  waliofika kumzika  ila  moyo umeniuma sana hasa  ukizingatia kuwa   kifo  chake hakikuwa na  ghafla bali  amekufa kwa mateso makubwa kwa  kuugua  karibu mwaka  mzima  sasa hivyo kwa  umoja  huo ningetegemea wangefika enzi za uhai  wake kumuuguza mwenzao”
Kwa  upande wake mwakilishi  kwa  kundi   la Weusi Bw  Joh Makini alisema  kuwa  kifo cha Mabovu  kimeacha  pengo kubwa katika tasnia  ya  muziki hasa muziki wa hiphop Tanzania,
 Alisema  kuwa  Mabovu  amepata  kuishinae Kinondoni  Jijini Dar es Salaam  mtaa mmoja  ila  pia amepata  kushirikiana  kazi mbali mbali  za kimzuki .
Hivyo  alisema  kuwa  ushirikiano  huo  ndio  ambao umewasukuma  kufika mkoani Iringa  kushiriki mazishi  hayo baada ya  pengo kubwa ambalo  wamelipata .
 
Akizungumza  kwa niaba ya  wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema  kuwa  Iringa  imempoteza  msanii mkongwe na  kuwa kifo  chake  kitaenziwa na  wasanii wa mkoa wa Iringa  pia  ambao  wapo nje ya mkoa huo kwa kuangalia jambo la kufanya  katika kuwanyanyua  wasanii chipukizi wa mkoa huo.
Alisema  kuwa  wapo  wasanii maarufu  wengi  kutoka mkoa wa Iringa ambao  wana majina makubwa kama  Rehema Chalamila (RAY C} akina  MiKe T  na  wengine  wengi na kuwa  kama  njia ya  kumuenzi  Mabovu  watahakikisha wanaunganisha  nguvu kwa kushirikiana na vyombo  vya habari  kuona Iringa inampata mwakilishi mwingine wa Mabovu kutoka kwa  wasanii Chipukizi .
Msanii Mabovu  alifariki  dunia jana  majira ya saa 2 usiku  nyumbani kwa wazazi  wake eneo la Mwangata mjini Iringa ambako alikuwa akiugulia na amezikwa  leo katika makaburi ya Mlolo nje  kidogo na mji wa Iringa

Tigo kusaidia mpango wa kujenga na kutoa vifaa kwa maabara ya shule za sekondari wilayani Mtwara

unnamed
Mkuu wa wilaya ya Mtwara mjini Bw. Wilman Ndile (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala kwaajili ya ujenzi wa maabara katika wilaya ya Mtwara, kulia kwake niMeneja wa Tigo kanda ya kusini, Bw.Daniel Mainoya na kushoto kwake mkurugenzi wa kampuni ya Proactive Solution, Nestory Phoye.
 ………………………………………………………………………………
Tigo Tanzania leo imetangaza kwamba itasaidia kujenga na kuchangia vifaa katika maabara ya shule za sekondari ambazo zimekwisha jengwa wilayani Mtwara. Mamlaka ya wilaya yanaandaa harambee kubwa siku ya Ijumaa wiki hii kwa ajili kufanikisha jambo hili. Akizungumza wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Meneja wa Kanda ya Mtwara kutoka Tigo Daniel Mainoya alisema kwamba kampuni yake inaamini katika kuwapatia watoto mazingira bora yakusomea, ili kuweza kuwajengea uwezo wa kuwa wananchi wanaowajibika na kuzalisha ipasavyo. “Hii ni muhimu sana hasa hasa katika kujifunza masomo ya sayansi. Ni muhimu kwa watoto wetu kupewa vifaa vinavyotakiwa ili kuweza kupata uelewa si wa kinadharia tu bali wakiuzoefu wa namna ya kujifunza masomo ya sayansi kama Baiolojia, Kemia na Fizikia,” alisema Mainoya. Wilaya ya Mtwara, ni moja kati ya wilaya sita zilizoko katika halmashauri ya mkoa wa Mtwara, yenye jumla ya shule za sekondari 42 zinazoendeshwa chini ya serikali. Kati ya hizi asilimia 18 tu ya shule hizi ndo zenye maabara ya kujifunza Fizikia, Kemia na Baiolojia, kutokana na maelezo ya Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Wilman Kapenjama. Akielezea kwamba hali kuwa ni “mbaya,” Kapenjama aliwaambia waandishi wa habari kwamba kukosekana kwa maabara hizo ni kilema kikubwa kwa wanafunzi wanaoazimia kuja kufanya kazi katika tasnia ya sayansi kama madaktari, maenjenia na kadhalika. Kutokana na maelezo ya DC alama ya wastani ya ufaulu kwa wilaya ya Mtwara katika masomo ya sayansi kwenye shule za sekondari kwa sasa ni asilimia 35. “Ni kwa sababu hii tuntoa rai kwa wadau wote kutoka katika sekta binafsi na ya umma kuja kutuunga mkono katika kuchangisha fedha kujenga maabara mapya na kuwapatia vifaa kwa maabara chache ambazo tayari zilishajengwa ili kuweza kuwawezesha watoto wetu kufurahia masomo ya sayansi na wakati huo huo kuweza kutimiza ndoto zao ya kuwa wanasayansi bora duniani,” alisema Harambee hiyo inayojulikana kama Tigo Mtwara Benefit Gala, itafanyika Ijumaa hii na itajumuisha kampuni na watu binafsi, pia kutakuwa kuna mnada wa bidhaa na vitu mbali mbali kama michoro ya Kiafrika, Yakimakonde na mnada wa safari za kitalii nchini, yote haya ni kwa ajili yakuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa maabara 43 katika sekondari mbali mbali hapa wilayani, alisema Kapenjama.

PINDA AAGANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNIDO NCHINI

unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNIDO nchini  aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu unnamed1 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi Mkazi wa UNIDO  nchini aliyemaliza muda wake, Bw. Emmanuel Kalenzi ambaye alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu kuaga Novemba 13, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
==============================================================

TANZANIA KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA SEKTA YA NYUKI DODOMA

index
Mahmoud Ahmad Arusha
Tanzania  inatarajia kujenga kituo Kikubwa   cha sekta ya nyuki ambacho kitatoa mafunzo  juu  ya namna bora ya kufuga nyuki kisasa
 
Mtendaji Mkuu wa baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi Dakta  Anaclet Kashuliza  ameeleza hayo  wakati wa kongamano la kwanza  la ufugaji nyuki barani Afrika.
 
Kituo hicho kinatarajiwa kujengwa MKoani Dodoma kwa msaada wa Kampuni moja kutoka Marekeni mbali na kituo hicho kuhusika na utoaji  mafunzo pia kitahusika na  uchakataji  wa asali
 
Dakta Kashuliza amesema kuwa kituo hicho  kitahusika na utunzani wa  kumbukumbu  ya vitu vya  asali  vya ufugaji nyuki hapa Tanzania na kinatarajia kuanza katika kipindi cha miezi minne ijaayo
 
Dakta Kashuliza  aidha amesema mbali na kujengwa kwa kituo hicho kikubwa barani afrika pia  Tanzania inatarajia kujenga viwanda vidogo vidogo, vya kati na viwanda vikubwa kwa ajili ya kusindika asali na nta
 
Viwanda hivyo  vitatumika kwa ajili ya watalii kutoka nje  watakaopata fursa ya kutembelea viwanda hivyo pamoja na kituo kikubwa  cha  Dodoma kujionea  juu ya hali ya raslimali asali ilivyo.
 
Wakati huo huo Serikali Mkoa wa  Singida imesema kuwa ipo tayari  kuyaondoa  makundi yote  ya watu waliovamia maeneo ya wahadzabe wakiwemo wakulima na wafugaji na hivyo kuwawezesha kumiliki maeneo hayo kama zilivyo jamii nyingine nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa mkoa wa Singida,Vicent  Parseko  Kone
 
Hatua hii inalenga kuwapa haki yao  ya msingi ya kumiliki ardhi jamii hiyo ya wahadzabe kama  jamii nyingine ya watanzania hapa nchini
 
Amewaambia washiriki wa kongamano la ufugaji nyuki barani afrika kuwa   asilimia 77 ya eneo linalokaliwa na jamii ya wahadzabe tayari limevamiwa na wafugaji pamoja na wakulima  jambo ambalo linatishia maisha ya jamii hiyo ya wahadzabe ambao  maisha yao yote hutegemea sekta ya nyuki 
 
Amesema katika mkakati huo wa kuwaondoa wavamizi wote pia  Serikali imefanikiwa kupeleka huduma mbambali za kijamii zikiwemo za maji, miundo mbinu ya barabara, elimu na afya.
 
Mkuu huyo wa Mkoa pia amesema Serikali Mkoani humo imefanikiwa kuyapima maeneo yote wanamoishi wahadzabe ili kuwawezesha kupata hati miliki
 
Pia amesema Serikali imesambaza mizinga  zaidi ya 150 katika jamii hiyo ili kuiwezesha kuendeleza zaidi ufugaji wa nyuki katika jamii hiyo pamoja na kuipatia  mtama kwa ajili ya kuwawesha kuendelezaa kilimo katika vijiji vyao
 
Mkoa huo hivi sasa una  watu wapatao 1,300 wa jamii ya  wahadzabe ambapo  300 wanaishi katika wilaya ya Mkalama katika Kijiji cha Munguli
 
Wakizungumza katika kongamano hilo mmoja wa jamii hiyo ya wahadzabe amesema jamii hiyo inayo haki ya kumiliki  ardhi kama jamii nyingine ya kitanzania
 
Aidha ameitaka serikali kukomesha vitendo  vya  baadhi ya jamii kuvamia maeneo yao kwa  kutumia nguvu  za kiuchumi walizonazo
 
Hivyo ameitaka   serikali kuhakikisha  jamii   ya wafugaji na wakulima kufuata taratibu pale wanapoingia katika  baadhi ya maeneo
 
Amekiri kuwa  kwa asilimia kubwa jamii ya wahadzabe walikuwa  hawajui haki haki zao pamoja na matumizi ya ardhi
Continue reading →
==============================================================

Ugungaji wa Semina ya wakuu wa Mikoa na Wilaya Bara na Visiwani

1Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakiwa katika ugungaji wa semina yao ya siku taku iliyozungumzia Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania bara iliyofungwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katika Ukumbi wa Sea Cliff  Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum) 2 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa Bara na Visiwani wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kuhusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania bara ufungaji huo ilifanyika  jana Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum) 3 Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji  katika  Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja,(Na Mpiga Picha Maalum) 4Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufungaji wa Semina ya siku tatu kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  iliyohusu Mahusiano na Mwingiliano katika siasa na Utendaji  katika  Ukumbi wa Sea Cliff Kama nje ya Mji wa Unguja jana,(Na Mpiga Picha Maalum) 6 Picha ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa Wakuu wa Mikoa,Wilaya,Makatibu Tawala wa Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Barabaada ya kufungwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikat, (Na Mpiga Picha Maalum) 8Picha ya pamoja iliyowahusisha washiriki wa Semina ya siku tatu ya kwa Maafisa Tawala Mikoa na Wilaya za Mikoa ya Zanzibar na Baadhi ya Tanzania Bara  baada ya kufungwa na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara  Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri katikati, (Na Mpiga Picha Maalum)
==========================================================

WANANCHI WAHIMIZWA KUJITOKEZA KUPIMA UGONJWA WA KISUKARI

index
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Serikali imetoa wito kwa kila mwananchi nchini kuhakikisha kwamba anapima afya yake  mara kwa  mara  kwa kuwa ugonjwa wa kisukari unaweza usionyeshe dalili yoyote mapema ili kuweza kukabiliana  na kupunguza athari za ugonjwa huo
Aidha Serikali imesisitiza kuwa endapo mtu atatambulika  kuwa ana ugonjwa huo, atumie huduma za afya kulingana na ushauri wa atakaopewa na wataalam wa afya.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Stephen Kebwe leo alipokuwa anatoa tamko kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa Novemba 14, mwaka huu duniani kote yenye kauli mbiu “Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi”.
Siku ya kisukari duniani ilianzishwa baada ya kuona ugonjwa wa kisukari unaongezeka sana duniani kote na Tanzania kama nchi nyingine duniani huadhimisha siku hii kwa kushirikiana na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari  Tanzania kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na madhara mbalimbali yatokanayo na ugonjwa huu, alisema Naimu Waziri.
“Ugonjwa wa Kisukari ni hali ambayo hutokea wakati sukari katika damu inapokuwa nyingi kupita kiwango cha kawaida kwa muda mrefu” aliongeza Dkt Kebwe.
Amebainisha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa kisukari ulimwenguni wanaishi katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania, na tafiti zinaonyseha kuwa mwaka 2007 kulikuwa na wagonjwa 246 milioni duniani,mwaka 2012 wagonjwa milioni 371, mwaka 2013 wagonjwa milioni 382ulimwenguni kote  na mwaka 2013 kulikuwa na wagonjwa milioni 19.8 barani Afrika.
 
Aidha nchini Tanzania kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2012 na kuhusisha wilaya 50 ulionyesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25 na kuendelea wana ugonjwa wa kisukari.
 Dk. Kebwe  aliongeza  kuwa takwimu za   watoto wenye kisukari mwaka huu ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wa kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki za  hapa nchini.
“Lakini wapo wengine hawajitokezi kwenye kliniki kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani potofu, gharama pamoja na umbali wa huduma za afya zilizopo” aliongeza Naibu Waziri huyo.
Aidha Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaendelea na utekelezaji wa Sera ya Afya(2007) inayolenga kutoa huduma kwa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani ya Nchi na wa kimataifa.
Tanzania inaungana na mataifa yote duniani kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2011 la kuhakikisha magonjwa yasio ya kuambukiza yanapungua kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.
================================================================

BODI YA FILAMU TANZANIA YAZITAKA KAMPUNI ZA FILAMU KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA FILAMU.

1
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiongea na wahusijka wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya nao mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
2q
3
4
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Kajala Masanja akiweka sahihi ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu yake pamoja na malipo ya faini mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu yake ya Mbwa Mwitu.
5
Meneja ambaye pia ni Mratibu wa Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke akiweka sahihi katika fomu maalum ya kukubali kufanya marekebisho katika filamu iliyokaguliwa na Bodi hiyo mbele ya Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania wakati aliitikia wito wa Ofisi ya Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuelezwa juu ya Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
6
Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kajala Entertainment wakati alipofanya naye mkutano leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwapa Sheria na Kanuni zilizokiukwa katika filamu ya Mbwa Mwitu.
(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO-DSM)
Na Benedict Liwenga, Maelezo-DSM.
BODI ya Filamu Tanzania imezitaka Kampuni za filamu nchini kufuata Sheria na Kanuni mbalimbali wakati wa kutengeneza filamu ili kuepusha ukiukwaji wa Sheria na Kununi.
Rai hiyo imetolewa leo na Katibu wa Bodi hiyo, Bi Joyce Fissoo wakati alipofanya mkutano na Kampuni ya Kajala Entertainment ambapo mnamo Septemba 22, mwaka huu ilikagua Filamu fupi ya kampuni hiyo iliyopewa jina la Mbwa Mwitu yenye dakika 12 na kubaini baadhi ya makosa.
Akiongea wakati wa mkutano na wadau wa kampuni hiyo, Bi Fissoo alisema kuwa Bodi iliielekeza Kajala Entertainment kuifanyia marekebisho filamu hiyo katika dakika ya 7 ambapo ilionekana wanawake wakidhalilishwa na kubakwa kinyama na pia katika dakika ya 11 ambapo ilionyesha wizi na uvamizi.
Alisema kuwa, wahusika walielekezwa kufanya marekebisho hayo kwa kuondoa vipande husika na baada ya kufanya marekebisho hayo waliwasilisha Bodi ya Filamu nakala ya filamu iliyokuwa imefanyiwa marekebisho yenye dakika 12 na kupewa kibali namba 4261 ya tarehe 24 Septemba, 2014.
Bi Fisso aliongeza kuwa, mnamo tarehe 25 Septemba, 2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, filamu hiyo fupi ilionyeshwa bila ya kuzingatia marekebisho yaliyokuwa yameelekezwa kwa mujibu wa Sheria kwa kuzingatia kifungu cha Sheria cha 19 (2) (a).
“Baada ya ukiukwaji wa Sheria katika kifungu cha 19 (2) (a) na kile cha 24 (i), (m) na (n) vya Kanuni za Sheria ya Filamu husika, wahusika waliitwa mara mbili kufika Bodi ya Filamu lakini hawakufanya hivyo, lakini baada ya kumbushio na kalipio wahusika baadaye walifika Ofisi za Bodi katika kikao cha tarehe 13 Novemba mwaka huu”, alisema Bi. Fissoo.
Alieleza kwamba, wahusika walikiri kuwa walipata ujumbe wa wito wao wa kuitwa na Bodi hiyo ambapo Mratibu wa masuala yote ya Kampuni ya Kajala Entertainment, Bi. Leah Mwendamseke aliieleza Bodi kuwa anaomba asamehewe kwa kuwa walikuwa na shughuli nyingine mbalimbali.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Kajala Massanja aliiomba radhi Bodi ya Filamu Tanzania huku akisema kuwa mara nyingi yeye huwa amekuwa akiwaachia wsaidizi wake kutekeleza majukumu ya kampuni yake ingawa yeye kama mmiliki wa kampuni hiyo anawajibika moja kwa moja.
Aidha, Bodi iliitaka Kajala Entertainment kueleza sababu ya kukiuka maelekezo ya Bodi ambayo yalikuwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake licha ya mtunzi na mwandishi wa musuada na muongozaji wa filamu hiyo, Bi. Leah Mwendamseke alijitetea kuwa alifanya utafiti na kukutanana vijana mbalimbali waliowahi kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Hata hivyo, Leah Mwendamseke alishindwa kuoanisha uhalisia wa matokeo ya utafiti wake na ujenzi wa visa vya hadithi ya filamu ambayo inaweza kupeleka ujumbe chanya kwa jamii, huku wahusika wakieleza kwamba lengo lao kubwa lilikuwa ni kuelimisha jamii kuhusu maovu yanayotokea na namna ya kuyaepuka ambapo mtunzi huyo aliahidi kurekebisha vipengelee husika katika filamu hiyo ili kuwa na filamu bora.
Kwa upande wake Mwakilishi toka Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Tanzania, Sylivester Mganga aliushauri uongozi wa Kajala Entertainment kufuata maelekezo na kuzijua Sheria mbalimbali zinazohusu mambo ya filamu kwa kuvishirikisha vyombo vya ulinzi na usalama kabla ya kujichukulia maamuzi ya kutengeneza filamu zenye kutishia amani ya nchi.
Bodi ya Filamu Tanzania imetoa onyo kali kwa wahusika kwa kutengeenza filamu zenye kuonyesha ama kukuza uhalifu na udhalilishaji bila kuainisha mkondo wa Sheria licha ya msamaha kutokana na kosa hilo ambapo Bodi hiyo imeitaka kampuni hiyo ilipe faini ya shilingi milioni moja kwa mujibu wa kifungu cha 47 (2) (a) cha Kanuni za Sheria ya Filamu ambayo wahusika waliridhia adhabu hiyo.
========================================================

WASIRA AKERWA NA MAKUNDI YA KUDUMU NDANI YA CHAMA

wasira ipp(1)
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,(Uhusiano na Uratibu ) , Stephen Wasira amesema kuwa yupo tayari kuvunja makundi ya kudumu yanayoongozwa na Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Felix Mrema pamoja na Batilda Burian aliyekuwa mgombe wa ubunge na kushindwa  kwa chama hicho kwenye chaguzi mbali mbali.
Aidha amesema kuwa Arusha inashindwa kwenye chaguzi mbalimbali kutokana na makundi yaliyopo ndani ya chama hicho na si kwasababu ya vyama vya upinzani kuwa na nguvu ya kuiangusha CCM.
Wasira aliyasema hayo jana Jijini hapa kwenye kikao cha Halmashauri ya Wilaya kilichofanyika jana ndani ya ukumbi wa CCM Mkoa na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa chama hicho chenye lengo la kupitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za wenyeviti wa mitaa.
Alisema makundi ya Batilda na Mrema ni lazima yamalizwe na kama mlezi yupo tayari kuyaita makundi hayo ili kumaliza tofauti zilizopo ndani ya chama na kutoa rai kwa wagombea wengine kuwa kama wameshindwa wakubali kushindwa na kumpa ushirikiano mgombe aliyepitishwa kwa wakati huo ila si vyema kuweka makundi ndani ya chama.
“Nakerwa sana na kushindwa kwetu kwenye chaguzi ambao sisi wenyewe ndio tunaofanya tushindwe na kwanini tunaendelea kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali sisi tukishinda au kushindwa tunapongezana  hili ni tatizo hata kama tumeshindwa tunapongezana  haiwezekani  lazima tufike mahali tuvunje makundi na kuchagua kiongozi/mgombea aliyemteule na si kuongozi asiyetakiwa na wananchi”.
Hata kamati za Siasa Mkoa wa Arusha nazo pia zimegawanyika  waandika maazimio na kamati nyinge zinakaa na kuyakataa hapana tunachane na makundi  na pia tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa  lazima tuchague kiongozi mteule na si kumchagua mjomba wala shangazi yako maana akishindwa tunashindwa wote kama chama na si wewe uliyetaka awepo.
Alihoji suala la wananchi wa Kijiji cha Nanja kilichopo Wilayani Monduli kuandamana hadi Ofisi za Mkoa kutoa malalamiko yao kuwa mgombea waliyemtaka si yule aliyepitishwa na kutoa tahadhari kwa wananachama na viongozi kuwa kwanini wanataka kuwa wabinafsi na kuhoji kwanini  mteule asipitishwe badala yake apitishwe mgombea asiyetakiwa na wananchi wa eneo husika/.
Aliongeza asijidanganye mtu Rais ajaye atatoka ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwani hata maandiko yanasema kuwa wagombea ni wengi lakini wateule ni wachache  .
Pia Wassira aliwasihi wanachama wa CCM pamoja na wananchi kwa ujumla kujitokeza kupiga kura ya maoni kwaajili ya katiba mpya pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kutimiza wajibu wao.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, onesmo ole Nangole awali akikaribisha Wassira ambaye ni mlezi wa chama hicho Mkoani hapa alisema kuwa kinachokiangusha CCM kwenye chaguzi mbalimbali Mkoani hapa ni makundi ndani ya chama na kuyataja makundi hayo kuwa yanaongozwa na Batilda pamoja na Mrema huku akimsihi Wassira kuwaita kwa pamoja na kuwafungia ndani ili waweze kujadili kiini cha makundi hayo na kuyavunja kabisa.
Nangole alihoji ni kwanini wanaangusha wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama na kutoa rai kwa wanaccm kuachana na majungu na kuacha watu kuamua nani wanayemtaka badala yake wasipeleke wateule mizigo kwenye chaguzi halafu mwisho wa siku chama kinashindwa kwenye chaguzi mbalimbali.uchaguzi unapofika tuweke nia ya kushindwa na kupongezena
===========================================================

Tigo, Original Komedi,na Wasanii kibao kutikisa jiji la Mwanza kwenye tamasha la Welcome Pack jumamosi hii.

1 Meneja wa Bidhaa wa Tigo Bw. Edwin Mgoa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza tamasha kubwa la Tigo welcome pack litakalofanyika uwanja wa ccm Kirumba jijini Mwanza Jumamosi ya wiki hii, tamasha hili litaweza kuwapa wananchi fursa ya kupata maelezo ya kina kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni ya Tigo.
5Kwaya Master Mwana FA akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo welcome pack jijini Mwanza jumamosi wiki hii.
6 Kikundi maarufu cha wachekeshaji cha Orijino Komedi kinatarajiwa kuwatumbuiza wananchi wa kanda ya ziwa katika tamasha maalum linaloandaliwa na Tigo jijini Mwanza Jumamosi ijayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Welcome Pack inayowapa wananchi fursa ya kupata maelezo ya kina kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo ya simu.
Meneja Bidhaa wa Tigo Bw.Edwin Mgoa alisema kwamba kampeni hiyo ya Welcome Pack inayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja na zaidi sasa imekwisha fanyika kwa mafanikio makubwa katika mikoa mingine ikiwemo Kagera, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Dodoma na Mbeya ambapo imewapa fursa maelefu ya wananchi kupata huduma za Tigo kwa karibu ikiwemo kifurushi cha Welcome Pack.
Kifurushi cha Welcome Pack, kwa mujibu wa Mgoa, kinampa mteja anaenunua laini mpya ya Tigo dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Tumeandaa matamasha haya kwa ajili ya kusherehekea huduma hii mpya mahususi kwa wateja wetu. Na kwa safari hii, Tigo imeamua kwenda kutikisa jiji la Mwanza na kikundi cha The Orijino Komedi na wasanii wengine wa Bongo fleva. Kwa hiyo tunapenda kuwasihi wateja wetu wote wa kanda hiyo ya ziwa kuchukua fursa hii kuja kujaribu hii huduma yetu mpya pamoja na kupata burudani isiyo na kifani kutoka kwa wasanii bora kabisa kutoka nchini Tanzania,” alisema Mgoa.
Mmoja wa wanakikundi kutoka Orijino Komedi, Lucas Mhavile almaarufu kama Joti alisema kwamba yeye binafsi pamoja na kikundi chake kizima wanafuraha kubwa sana kushiriki katika msafara wa tamasha la Tigo Welcome Pack na wapo tayari kwenda Mwanza kuwapatia zaidi ya burudani mashabiki wao.
“Napenda kutoa rai kwa watu wote wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa CCM Kiruma siku ya Jumamosi kuanzia saa 6 mchana. Tamasha la Tigo Welcome Pack si jambo la kukosa! Njoo upate burudani, ucheze na ufurahi. Lakini usisahau pia kujipatia kifurushi cha Welcome Pack kutoka Tigo na uanze kuwasiliana na marafiki na familia yako kupitia ofa kabambe kabisa kutoka Tigo,” alisema Joti.
Akifafanua kuhusu kifurushi cha Welcome Pack, Mgoa alisema kwamba kifurushi hicho kinakuja na dakika 20 za muda wa maongezi, MB 175 za intanet, kutuma ujumbe mfupi wa SMS bila kikomo, na kiasi cha shilingi 500 kama salio la Tigo Pesa kwa kila mteja atakaye nunua laini ya Tigo kwa kiasi cha shilingi 1000 tu.
“Hii itawawezesha wateja wetu kuwasiliana zaidi na kwa gharama nafuu ambayo haijawahi kutokea,” alisema Mgoa.
Kampeni ya Welcome Pack itakuwepo kwa muda wa miezi mitatu, ambapo misafara zaidi ya 70 ikiwemo basi la Tigo la Kidijitali lenye malengo la kuwaelimisha wateja kuhusu huduma za Tigo za kidijitali litatembelea miji 70 na vijiji zaidi ya 100 ndani ya mikoa 10 tofauti ikiwemo Mbeya, Iringa, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Kigoma na Mtwara.
Wasanii maarufu wa Bongo fleva watakaotoa burudani ni pamoja na Profesa J, Joh Makini, Shah, Mheshimiwa Temba na Chege, Madee na Izzo Business. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni nyote,” alimalizia kwa kusema Mgoa.

WANAFUNZI BORA CBE WAPATA TUZO.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO

Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam kimetoa tuzo kwa wanafunzi bora 12 waliohitimu na kufanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka wa masomo 2014/2015 ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini mchango walioutoa katika maendeleo ya taaluma chuoni hapo.

Akikabidhi tuzo hizo katika hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar es salaam, aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mwenyekiti wa sasa wa wanafunzi  waliomaliza chuo cha CBE, Bw. Harry Kitilya amesema kuwa wahitimu hao wanayo nafasi kubwa ya kutumia elimu waliyoipata na kuwa mfano katika kuleta mabadiliko nchini.

Amesema chuo hicho tangu kuanzishwa kwake  mwaka 1965 kimekua mfano wa kuigwa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu  ili waweze kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Biashara nchini kwa kuongeza  nafasi za ajira kwa kujiajiri wenyewe  kupitia shughuli za ujasiriamali,uanzishaji wa makapuni na miradi mbalimbali.

Bw.Kitilya amewataka wahitimu hao kujiendeleza zaidi kielimu ili waweze kukabiliana na ushindani wa ajira uliopo hususan katika soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kuepuka vitendo vya rushwa na uzembe pindi wanapoingia katika ajira.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akizungumza na wahitimu wa mwaka 2014 wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo ulioshuhudiwa na wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma ni utaratibu wa chuo hicho kuenzi na kuthamini juhudi walizozionyesha katika taaluma.

 Amesema utoaji wa tuzo hizo umehusisha  fani za Uhasibu,Udhibiti wa Biashara, Usimamizi wa Masoko,Manunuzi na Ugavi na kuongeza kuwa utafanyika katika kampasi nyingine za chuo hicho zilizoko Zanzibar, Mbeya, Dodoma na Mwanza.

“Siku ya leo mbali na zoezi hili la utoaji wa tuzo, wahitimu wote wa sasa na wa zamani wanakutana kujadili namna ya uendelezaji wa chuo chetu, siku hii ni muhimu sana kwa kuwa inaongeza ushiriki wao katika kujadili masuala mbalimbali ya kukiendeleza chuo” Amesema Prof. Mjema.

Ameongeza kuwa lengo la kuwakutanisha wahitimua wa miaka iliyopita ni kujenga umoja imara na kupata mrejesho kutokana na huduma wanazozitoa kwa jamii, mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo.
 
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu wa mwaka 2014 na wale miaka iliyopita wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa hafla hiyo, wameiomba Serikali kendelea kupanua wigo wa Elimu ya Biashara kwa kuongeza matawi mengi zaidi kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi katika maeneo yao.

Wameiomba Serikali kupitia wizara ya Viwanda na Biashara kuwaendeleza na kuwawezesha wahitimu wanaoonyesha nia ya kujiajiri wenyewe na kuanzisha makampuni yao hapa nchini.

Aidha ,wametoa wito kwa walimu kutoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea duniani ili kuwawezesha kukidhi soko la ajira  huku wakitoa wito  kwa wahitimu wa vyuo kujenga utamaduni wa kujitolea ili waweze kupata uzoefu.

MWISHO.

Thursday, November 13, 2014

MTOTO ANYONGWA BILA HURUMA ENEO LA MAJOHE DAR ES SALAAM

 Mtoto Nuru kabla yakufikwa na umauti pichani alipo kuwa na miaka 3.Mtoto huyo anadaiwa kunyongwa  Alhamisi iliyopita na kuzikwa katika Makaburi ya Majohe kwa Muslim   (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA BILALI) Mmiliki wa Blog ya UJIJIRAHAA.
 Nguo ya Mmtoto huyo alio kua ameivaa kabla ya kunyongwa kinyama .
 Hii ni Mipira ya kuvaa mikononi iliyotumika kuubeba Mwili huo.
 Mama wa marehemu Nuru  Mohamedi , ambaye ni Sauda Ally.  akiwa amelala kutokana na kuishiwa nguvu mwilini kwa kufikwa na tukio hilo.  wakati  akiongea  na mwandishi wa habari.
 Mama wa marehemu Nuru  Mohamedi , ambaye ni Sauda Ally (wakwanza kushoto). akiongea kwa shida  na mwandishi wa habari, Nyumbani kwa Mama  huyo leo Dar es Salaa eneo la Majohe.




 Familia ya mtoto Nuru Mohamed (7) pichani  juu,  wakitoka nje baada ya kumuonyesha mpiga picha wa Gazeti la  sehemu iliyopo ndani ya pagala alipouawa mtoto huyo kwa kuwekewa matofari juu ya  mtu asiyejulikana Alhamisi jioni eneo la Majohe Kichangani, Ukonga, Dar es Salaam.
Pagala la Nyumba hilo lipo barabarani.

WAZIRI MUHONGO AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA MCC

8
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisistiza jambo katika kikao baina ya Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan (wa pili kushoto) na ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress(wa kwanza kushoto). Wengine wa kwanza ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava na watendaji wa Wizara,na wa taasisi za Wizara wakifuatilia kikao hicho.
9Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan ( wa kwanza kushoto ) akimweleza jambo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) anayesikiliza katikati ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress mara baada ya kikao hicho.
11Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo katikati) katika picha ya pamoja ofisini kwake na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan (kushoto) na Balozi wa Marekani nchini , Mark Childress (Kulia)..
……………………………………………………………………
Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Makamu wa Rais wa Mfuko wa Changamoto za Millenia (MCC) Kamran Khan na Ujumbe wake akiwemo Balozi wa Marekani nchini Mark Childress, katika kikao kilicholenga kujadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa MCC Awamu ya pili na masuala ya kuendeleza sekta ya nishati nchini. Kikao hicho kimezihusisha pia taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini ikiwemo, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) pamoja na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA). Katika kikao hicho, Profesa Sospeter Muhongo amezitaka taasisi hizo kutekeleza miradi hiyo kwa kasi zikizingatia suala la uwajibikaji, ubunifu, uwazi na kuongeza kuwa, miradi hiyo itatekelezwa bila kuwepo na mazingira ya rushwa , huku akisisitiza ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika uendelezaji wa miradi hiyo. Kwa upande wake Makamu wa Rais wa MCC, Kamran Khan ameahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kutekeleza miradi hiyo ambayo inalenga kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha. Kwa upande wake Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amesisitiza suala la kuzingatia muda katika utekelezaji wa miradi hiyo na kuongeza kuwa, hakuna sababu itakayokwamisha miradi hiyo.

Rangers vs Majimaji Karume kesho

Mwandishi Wetu
index
KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Karume kuvaa na timu ya MAjimaji ya Songea, katika mchezo wa

Ligi Daraja la kwanza.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa
wanatarajia kuona upinzani mkali kutoka katika timu hiyo ambayo  mpaka sasa ndiyo inaongoza
ligi, wakati wao wakishika nafasi ya pili.
Kigundula alisema kuwa kikosi chao tayari kipo kambini kikijiandaa na mchezo huo, huku
kocha wao Ally YUsuph ‘Tigana’ akijipanga kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani.
PIa Kigundula amewataka wapenzi kujitokeza kwa wingi kuipa ushirikiano timu yao ambayo
inapambana kuhakikisha inapanda daraja msimu ujao.
“Kikubwa tukipata ushirikiano kwa wapenzi ambao wamekuwawakijitokeza kutushangilia mwanzo
mwisho tunaomba mjitokeze kutushangilia tufanye vizuri”alisemaKIgundula
Rangers ina pointi 16, baada ya kucheza mechi 8 huku wanaoongozawakiwa Majimaji
wakitofautiana kwa pointi mbili, endapo Rangers itashinda itakuwa ikiongoza kwa tofauti ya pointimoja.
Ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare mechi nne , huku ikiwa inakimbizana na Majimaji ambayo nayo ina pointi 15.

NHC yavutia uwekezaji kongamano la uwekezaji JNICC

Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima akifungua kongamano la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) lililolenga kukuza na kuvutia uwekezaji kutoka kwa makampuni na
taasisi mbalimbali kubwa za kimataifa katika sekta za Uendelezaji
Miliki, Kilimo na Usafirishaji. (Picha Zote za Kitengo cha Mawasiliano
kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Meneja waUendelezaji Biashara wa NHC, William Genya akijadiliana jambo na washiriki wa kongamano hilo

Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitoa
mada kwenye kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo, lililolenga kukuza na
kuvutia uwekezaji kutoka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kubwa za
kimataifa katika sekta za Uendelezaji Miliki, Kilimo na Usafirishaji.
 
 
Mkurugenzi wa Ukusanyaji Mapato wa Ofisi ya Rais, Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Lawrence Mafuru ambao ndio wandaaji wa kongamano hilo akizungumza  kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo,
kongamano hilo limelenga kukuza na kuvutia uwekezaji kutoka kwa
makampuni na taasisi mbalimbali kubwa za kimataifa katika sekta za
Uendelezaji Miliki, Kilimo na Usafirishaji.
Baadhi
ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.
 Baadhi
ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.

 Baadhi
ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, DkShaban Mwinjaka, Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison
Mwakyembe wakifuatilia mada katika kongamano la uwekezaji lililoandaliwa
na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo.

Naibu
Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima na Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison
Mwakyembe wakifuatilia mada katika kongamano la uwekezaji lililoandaliwa
na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Bi Julieth Kairuki akitoa mada kwenye
kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo, lililolenga kukuza na kuvutia uwekezaji
kutoka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kubwa za kimataifa katika
sekta za Uendelezaji Miliki, Kilimo na Usafirishaji.
Mtendaji
Mkuu wa Investment Capital Group (ICG), Shose Sinare na baadhi ya
washiriki wengine waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.
Mkurugenzi wa Ukusanyaji Mapato wa Ofisi ya Rais, Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Lawrence Mafuru na washiriki
wengine waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji lililoandaliwa
na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo.
 Baadhi
ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.
 
 
 
 Naibu Waziri wa Fedha, Adam Kighoma Malima akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kongamano hilo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na waandishi wa habari kwenye kongamano hilo.

Baadhi ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.

Baadhi ya washiriki waliokuwapo katika kongamano hilo la uwekezaji
lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na
kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere
(JNICC) leo.
Maafisa NHC  Clara Lumbanga, Fatima Rajabu na Bulla Boma wakifuatilia mada katika
kongamano hilo la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo Makubwa
Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo.
 
 Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akitoa
mada kwenye kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo, lililolenga kukuza na
kuvutia uwekezaji kutoka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kubwa za
kimataifa katika sekta za Uendelezaji Miliki, Kilimo na Usafirishaji.
 
Mkurugenzi
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe akifuatilia
kwa makini kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha Mikutano
cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo, lililolenga kukuza na
kuvutia uwekezaji kutoka kwa makampuni na taasisi mbalimbali kubwa za
kimataifa katika sekta za Uendelezaji Miliki, Kilimo na Usafirishaji.
 
 Maafisa
wa NHC  nje ya kongamano la uwekezaji lililoandaliwa na Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) na kufanyika katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere (JNICC) leo, lililolenga
kukuza na kuvutia uwekezaji kutoka kwa makampuni na taasisi mbalimbali
kubwa za kimataifa katika sekta za Uendelezaji Miliki, Kilimo na
Usafirishaji.
 Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiwa katika
majadiliano ya kina na baadhi ya washirikia walioonyesha nia ya
kuwekeza katika miradi ya NHC.
Afisa Uendelezaji Biashara NHC, Fatima Adadi Rajabu akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Investment Capital Group (ICG), Shose Sinare
 
Afisa Masoko wa NHC, Mariam Ndabagenga akijadiliana jambo na washiriki wa kongamano hilo 
Mkurugenzi Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe akijadiliana jambo mmoja wa washiriki wa kongamano hilo

Taasisi ya Starkey Hearing Foundation yakabidhi madarasa matatu shule ya msingi ya Loiborsoit

1Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.David na steven
2 3Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin akipima sikio kwa mmoja wa watoto waliohudhuria kliniki iliyokwenda sambamba na ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
4Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.
5Mwanzilishi wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation, Bill Austin pamoja na mkewe, Tani wakipokelewa na wanakikiji wa Loiborsoit kwenye ufunguzi rasmi wa majengo matatu ya shule ya Msingi ya Loiborsoit yaliyojengwa na mwanzilishi huyo kwa ajili ya jamii ya Kimasai katika sherehe zilizofanyika eneo hilo wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara jana.Kulia ni David Furnish mmoja wa wageni maarufu aliyehudhuria hafla hiyo.Yohana shinini
7Wanafunzi wa darasa la kwanza wa Shule ya Msingi Loborsoit iliyopo Simanjiro wakiwa darasani huku timu ya Taasisi ya Starkey Hearing Foundation wakiwa nyuma yao wakati wa kukabidhiwa majengo hayo katika sherehe iliyofanyika Wilayani Simanjirojana..
9 11a
unnamed1Wakiwa katika picha ya pamoja  unnamed2Wakurugenzi wa Kampuni ya Montage Nesto Mapunda na Teddy Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja  unnamed3Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Teddy Mapunda akishuka kwenye helkopeta iliyowachukua wakuu wa taasisi ya Starkey Hearing Foundation

MWILI WA MAREHEMU ROBERT LENGEJU WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUZIKWA KESHO KIPERA MOROGORO.

Hili ndilo sanuku lililouhifadhi mwili wa Mwandishi/Mchambuzi wa Jukwaa Maalumu la MWALE WA DEMOKRASIA katika Gazeti la Raia Tanzania (Gazeti dada
la Raia Mwema),
kila Alhamisi. Mwili wa shujaa huyo wa Demokrasia uliswaliwa katika Kanisa Katoliki M
Watu mbalimbali walihudhuria katika misa hiyo ya kumsindikiza Lengeju katika safari yake ya mwisho kabla ya maziko yatakayo fanyika kesho (Novemba 13,2014) Kijijini kwako Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro. Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog.
 Ndugu wa marehemu Robert Lengeju wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mdogo wao.
Heshima za mwisho ziliendelea kutolewa na ndugu jamaa na marafiki.
Godfrey Dililunga kutoka kampuni ya Raia Mwema wachapaji wa gazeti la Raia Mwema na Raia Tanzania akitoa heshima za mwandishi huyo wa Makala za Mwale wa Demokrasia katika gazeti lao.
Mhariri wa Raia Mwema, Ezekiel Kamwaga akitoa heshima kwa mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakipita kutoka heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mstaafu, Isdore Shirima nae alikuwepo kutoa heshima za mwisho kwa Lengeju.
Waombolezaji
wanakwaya wakiimba katika misa hiyo.
wanafamilia wakiwa Kanisani katika misa.
Wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika misa hiyo leo.
 Kaka wa Marehemu Charles Lengeju akiwa amebeba msalaba wa marehemu.
Gari lililobeba mwili wa marehemu Robert Lengeju likiwa tayari kwa safari ya Kipera Mkoani Morogoro.

KAMPUNI YA MABIBO BIA NA JESHI LA POLISI WAFANYA SEMINA SHIRIKISHI MKOANI MOROGORO

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Ramadhan Abdul Mambea (kulia), naye akichangia jambo kwenye semina hiyo.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Mabibo, Eustadius Mutabingwa (kulia), naye alichangia uzoefu wake katika semina hiyo.
 Mkurugenzi wa Maghala na Usalama wa Kampuni ya Mabibo Bia (MBL), Boniface Katanyebile naye alikuwa katika semina hiyo akifuatilia kila jambo lililokuwa likijadiliwa.
 Wadau wakiwa katika semina hiyo.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Mabibo (MBL), Respicius Didace akitoa historia fupi ya kampuni ya Mabibo na mambo mbalimbali ya kisheria kuhusu utii wa sheria bila shuruti.
 Ofisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi, SSP Gemin Mushy (kushoto) na Mshauri wa Kampuni ya Mabibo, Kamala Stephen wakifuatilia mada katika semina hiyo.
………………………………………………………………………..
 
Dotto Mwaibale
 
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ni kosa kisheria kwa mtu kukutwa akiuza bidhaa au vinywaji vilivyosamehewa kodi na serikali vinavyouzwa majeshini.
 
Hayo yalisemwa na  Ofisa Mwandamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkunga Tuwaha wakati akitoa mada kwenye semina shirikishi kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Bia ya Mabibo iliyofanyika Top Life Hoteli mjini Morogoro leo asubuhi iliyohusu kujadili mambo mbalimbali ya jeshi hilo na utii wa sheria bila shuruti.
 
“Vinywaji na bidhaa zingine zenye msamaha wa kodi hasa katika majeshi yetu ni vema zikatumika kwa ajili ya askari na familia zao na si mtu mwingine” alisema Tuwaha.
Semina hiyo ilishirikisha askari wa jeshi hilo ambao ni mameneja wa kantini kutoka  mikoa ya Njombe, Tanga, Dodoma, Morogoro, Tanga na Dar es Salaam na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo. (Imeandaliwa na mtandao wa 
www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)

WANASHERIA MWANZA WAIFAGILIA WINDHOEK WASEMA NI BORA KWA AFYA

Wanasheria wa jiji la Mwanza wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mwanasheria Mtalemwa (wa pili kushoto), akiwa na wanasheria wenzake  wakifurahia Windhoek.
Kikao na hafla vikiendelea.
…………………………………………………………………………….
 
Dotto Mwaibale
 
BAADHI ya Wanasheria wa jiji la Mwanza wamesema unywaji wa bia ya Windhoek utasaidia kujenga afya za wanywaji kwani imetengenezwa kwa ubora wa juu ukilinganisha na bia zingine.
 
Wanasheria hao waliyabainisha hayo jijini Mwanza katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Mabibo kwa ajili ya kujua changamoto mbalimbali kutokana na soko la bia za Windhoek na Windhoek Draught na kupata maoni ya wadau wa vinywaji hivyo  iliyofanyika jijini humo mwishoni mwa wiki.
 
Mmoja wa wanasheria hao,   alisema kwa muda mrefu na familia yake amekuwa akitumia Windhoek na ajawahi kupata shida yoyote  kwani inachangamsha akili tofauti na bia zingine.
 
Bia hii haiwezi kumfanya mtumiaji ajisikie vibaya hata akinywa kiasi kikubwa na ndio maana mimi na wenzangu tunatumia bia hizi za windhoek.
 
“Iwapo tutajenga tabia ya kunywa bia hii hakika utafanya kazi zetu kwa uhakika hata tukiwa makazini kwani haitoi harufu mdomo na kulewesha ni vizuri  tukaiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia ” alisema Mwanasheria huyo.
 
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, Fr James Rugemalira aliwaomba wanamwanza kuiunga mkono Kampuni ya Mabibo Bia kwa kununua vinywaji vyake kwani mpango wa kampuni hiyo ni kujenga kiwanda ambapo kitakuza uchumi wa mkoa wa Mwanza na kutoa ajira kwa vijana.
 
“Hatuwezi kukamilisha ndoto zetu za kujenga kiwanda bila ya nyinyi kutuunga na kupata mrejesho mzuri wa mauzo ya bidhaa zetu tuungeni mkono kwa kununua Windhoek Lager na Windhoek Draught zenye namba ya MB66 ubavuni ambazo ndizo halali katika soko la Tanzania na si vinginevyo” alisema Fr James. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Washiriki wa Kongamano la Ufugaji nyuki Afrika washauri kutumia mizinga ya udongo

unnamed
Mshiriki katika kongamano akiendelea kujifunza namna ya ufugaji nyuki kutoka Halmashauri ya Mpanda Mkoani Katavi wakati wa kongamano la Ufugaji nyuki la Afrika jijini Arusha ambapo banda la Halmashauri ya Mpanda lawa kivutio kwa washiriki hasa asali safi ya nyuki wadogo na wakubwa iliyotokea kupendwa na kuwavutia washiriki wengikwenye kongamano.
(Picha Na Kibada Kibada -Arusha.)
………………………………………………………………………………………………..
Kibada Kibada-Arusha.
Washiriki wa Kongamano  la Ufugaji nyuki Afrika linaloendelea kwenye ukumbi  wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha wameshauri kuona  uwezekano wa kutumia mizinga iliyotengenezwa kwa udongo  ambayo ni rafiki wa mazingira ili kuepeusha uharibifu wa mazingira unaoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya mizinga inayotengenezwa kwa kutumia miti.
  mama wengi nchini Zambia wanaofuga nyuki kwa kutumia mizinga iliyotengenezwa kwa udongo katika kuhifadhi mazingira.
Akichangia katika kongamano hilo Afisa nyuki kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa washiriki kwenye kongamano hilo MR Rupia alieleza uzoefu wake alioupata kutoka nchini Zambia alipotembelea kujifunza masuala ya ufungaji nyuki  ambapo akina mama wengi nchini Zambia wanaofuga nyuki wanatumia  mizinga iliyotengenezwa kwa udongo katika kuhifadhi mazingira na  robo tatu ya wananchi wa Zambia wanaojishughulisha na ufugaji nyuki ni akina mama na watumia ufugaji nyuki wa mizinga iliyotengenezwa kwa udogo ili kuokoa mazingira na katika hilo  wamefanikiwa kuhifadhi mazingira.
Rupia akaeleza kuwa wanaumekatika nchi ya Zambia  ni wachache sana wanaojishughulisha na ufugaji nyuki kwa kuwa teknolojia inayotumika imekuwa rafiki zaidi kwa wanawake katika uhifadhi wa mazingira ndiyo maana wanawake wengi wanajihusisha na ufugaji nyuki kwa kutumia mizinga iliyotengenezwa kwa udogo kwa kuwa inasaidia kutochangia  uharibifu wa mazingira.
Akashauri hapa nchini Tanzania elimu na  hamasa ianze  kutolewa kwa wafugaji nyuki ili kufuga nyuki kwa kutumia mizinga iliyotengenezwa kwa udogo kwani itasaidia sana katika uhifadhi wa mazingira kwa kuwa itakuwa inatumia udongo kuliko kukata miti na kutengeneza mizinga  ya miti.
A wali wawasilishaji wa mada katika kongamano hilo waliwasilisha  mada mbalimbali baadhi ya mada    iliyohusu kupanua wigo wa mazao ya nyuki Tanzania iliyowasilishwa na Linus Gedi kutoka Tanzania,kuelewa ufugaji nyuki katika misitu na kuzingatia mfumo endelevu wa matumizi ya ardhi iliyowasilishwa na Janeth Lowore kutoka Uingereza,Athari za mabadiliko ya tabia nchi katika ufugaji nyuki, kwa kuzingatia utafiti uliofanyika Mkoa wa Kigoma iliyowasilishwa na Seif Salum kutoka Tanzania,
Mada nyingine ni mabadiliko ya Tabia nchi na tofauti zinazojitokeza katika ufugaji nyuki katika wilaya ya Kiteto Mkoani Arusha  na hatua za kukabiliana na athari hizo,muhtasari wa Hali ya Misitu na udhibiti wa moto wa nyika nchini Tanzania iliyowasilishwa na Gerald Otieno kutoka Tanzania pamoja na ile iliyohusu Sababu za zinazochangia ushiriki hafifu wa wanawake na Vijana katika Tasinia ya ufugaji nyuki kwa kuzingatiastadi iliyofanyika mkoani kigoma iiliyowasilishwa na Dkt Angela Mwakatobe kutoka Tanzania ambayo ilionekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa washiriki.,
Kongamano hilo la wafuga nyuki la Afrika   lilifunguliwa na waziri Mkuu Mizengo Pinda  kwa kuwashauri wafugaji nyuki watumie nafasi hiyo  kupata uzoefu kutoka kwa wafugaji tofauti ndani na nje ya nchi hasa wa Bara la Afrika katika.Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni kufuga nyuki kuzingatia hifadhi ya mazingira na kukuza uchumi, lengo kuboresha sekta ya ufugaji nyuki Afrika na nchi zinazoendelea kwa ustawi wa wananchi hasa waishio Vijijini.

ZAIDI YA WANARIADHA ELFU KUMI NA TANO KUSHIRIKI UHURUMARATHON 2014

unnamed
Mratibu wa mbio za uhurumarathon 2014 Innocent Melleck katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya maandalizi yam bio hizo kwa mwaka huu ambapo zitafanyika 07/12/2014 na kuongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha elfu kumi na tano kukadiriwa kushiriki kwa mara ya kwanza.Kulia kwake ni Katibu mkuu wa shirikisho la riadha nchini Selemani Nyambui na kushoto ni mjumbe wa chama cha riadha mkowa wa Dar Es Salaam Tullo Chambo
………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
 
ZAIDI ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa kuthibitisha kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza jana jijini, Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuongoa mbio hizo.
 
Melleck pia jana alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Chama cha Raidha Tanzania (RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.
 
Mratibu huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zimeanza kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN, huku pia zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na Leaders.
 
“Tunawashukuru wadau wote walioshiriki katika kujiandaa kushiriki mbio hizo hasa klabu za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha kushiriki mbio hizo zenye kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,” alisema Melleck.
 
Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama kimeialika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na mataifa mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania.
 
Nyambui alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji vyao na wanaamini yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania.
 
Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama kimeshiriki kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na mafanikio.
 
Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote yanayoendelea kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa kufuata taratibu za kiufundi.
 
Melleck alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa wale wote wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu
 
Mbio za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc 1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi media,CxC  Africa,Kitwe General Traders,Samsung,Cokacola,Tindwa Mediacal Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na TSN SUPERMARKETS.

VACANCY ANNOUNCEMENT

imagesP
ost Title: Research Director
Background The Ministry of Health and Social Welfare and the Drug Control Commission (DCC) in collaboration with the Centers for Disease Control and Prevention, Muhimbiili National Hospital, Mwananyamala Municipal Hospital and Temeke Municipal Hospital is implementing a program aim
ed at increasing coverage of people who use drugs (PWUDs) into medically assisted treatment (MAT) of opioid dependence with an ultimate goal of minimizing HIV infection among PWUDs. The program intends to achieve this goal through execution of innovative Key Population Implementation Science (KPIS) on Optimized Methadone Delivery with Take away Doses of Methadone. The initiative will be implemented with the financial support from the USA President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) through the Centers for Disease Control and Prevention with technical assistance from a USA based PANGAEA Global AIDS Foundation.
The Ministry now invites applicants who are qualified, self motivated, dynamic, results oriented performer and committed individuals to fill the position of a Research Director. The incumbent will be part of the key population implementation science team of investigators.
Continue reading →

TAARIFA MBALIMBALI ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TFF

index17
KAMATI YA SHERIA YAPITISHA USAJILI SDL
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imepitisha usajili wa Ligi Daraja la Pili (SDL) huku ikikata majina mawili ya wachezaji katika klabu za Abajalo ya Dar es Salaam na Magereza ya Iringa.
 Klabu hizo mbili zilisajili wachezaji 31 badala ya 30 ambapo ni kinyume na Kanuni ya 61(2) ya Ligi Daraja la Pili inayoruhusu klabu kusajili wachezaji wasiozidi 30 na wasiopungua 18.
 Wachezaji ambao Kamati ya Sheria iliyokutana jana (Novemba 11 mwaka huu) imewaondoa ni wale waliokuwa wameorodheshwa namba 31 katika usajili wa klabu hizo. Wachezaji hao ni Andrew Mathew Kazembe (Abajalo) na Joshua Omari (Magereza).
 Michuano ya Ligi Daraja la Pili inayoshirikisha timu 24 katika makundi manne ya timu sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini itaanza kutimua vumbi Novemba 22 mwaka huu.
 Wachezaji waliopitishwa katika kila klabu na idadi yao kwenye mabano ni Abajalo (30), Arusha FC (18), Bulyanhulu (28), Kariakoo (30), Kiluvya United (23), Magereza (30), Mbao (27), Milambo (29), Mji Mkuu (29) na Mkamba Rangers (30).
 Wengine ni Mpanda United (29), Mshikamano (28), Mvuvumwa (18), Njombe Mji (25), Pamba (24), Rwamkoma JKT (25), Singida United (26), Town Small Boys (22), Transit Camp (28), Ujenzi Rukwa (30), Volcano (25) na Wenda (20).
 Klabu zote zinakumbushwa kulipia na kuchukua leseni za wachezaji wao kabla ya ligi kuanza, kwani kwa mujibu wa kanuni hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kucheza mechi ya ligi bila kuonyesha leseni yake. 
 WATANO WAUNDA JOPO KUHAKIKI UMRI COPA
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeunda jopo la watu watano kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki hatua ya ngazi ya Taifa ya michuano ya Copa Coca-Cola 2014.
 Michuano hiyo ya ngazi ya Taifa itafanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 13 hadi 20 mwaka huu. Uhakiki wa umri utafanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu wakati timu zote zinatakiwa kuwasili Shule ya Filbert Bayi mkoani Pwani kuanzia Desemba 10 mwaka huu.
 Jopo hilo la uhakiki linaongozwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Henry Tandau. Wengine katika jopo hilo ni Ally Mayay, Charles Boniface Mkwasa, Dk. Jonas Tiboroha na Richard Yomba.
 Timu 16 zitakazocheza michuano hiyo inayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 ni Arusha, Dodoma, Geita, Katavi, Kigoma, Kinondoni, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Simiyu na Tanga.
 Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinakumbushwa kutuma TFF fomu za usajili ambazo zinatakiwa kuambatanishwa vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji husika.

TANESCO YASHINDWA KUWAUNGANISHIA UMEME WANANCHI WILAYANI MERU KWA MUDA MREFU

index
Mahmoud Ahmad Meru
Wananchi wa kata ya Seela\Sing’isi wilayani Arumeru mkoani Arusha wamelilalamikia shirika la ugavi wa umeme(TANESCO)kushindwa kuwaunganishia huduma ya umeme kwa muda mrefu sasa licha ya kulilipa shirika hilo fedha za kuunganishiwa umeme hali inayowaleta usumbufu wa mara kwa mara kuifuatilia huduma hiyo.
Kadhia hiyo imeibuliwa na mtandau huu  wakti lilipokuwa wilayani Meru baada ya wananchi kuelezea Kero mbalimbali wanazokumbana nazo katika kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla huku wakiliomba shirika hilo kutekeleza maombi yao ya kupatiwa huduma hiyo.
Wakionyesha Nakala za Mikataba yao na barua za Malalamiko walizopeleka kwa Meneja wa wilaya na mkoa wa shirika hilo la ugavi huku majibu yakinifu wakishindwa kuyapata na lini watapata huduma hiyo.
Mmoja ya wananchi hao aliyezungumza na mwandishi wa habari hii Khamis Juma alisema kuwa wana muda sasa karibu miezi mitano hawajapata huduma walioomba huku akifuatilia maeneo mbalimbali kujua wamekwamia wapi bila ya kupata majibu na teyari alikwisha lipia fedha za mkataba wa kuunganishiwa umeme.
Juma alionyesha barua ya Mkataba huo yenye kumb;USA\SL2 ya tarehe 136\2014 na kulipiwa siku hiyo hiyo na hadi leo takribani miezi mitano hajaungiwa umeme huku akifuatilia na kupewa majibu ya njoo kesho kutoka kwa watendaji wa shirika hilo la ugavi.
Suala la kuunganishiwa umeme kwenye baadhi ya kata wilayani humo limekuwa likiangaliwa kwa watu wenye nacho ambao wamekuwa wakitoa chochote kwa watendaji hao hali inayowafanya wasio naocho kukosa huduma hiyo kwa wakati.
Gazeti hili lilipomtafuta Meneja wa wilaya na mkoa kwa njia ya simu zaoa za mkononi  hawakuweza kupokea hata walipotumiwa ujumbe wa sms na mwandishi kujitambulisha bado hakukuwa na majibu.
Kwa upande wake dc wa wilaya hiyo Nyerembe Munasa Alisema kuwa Atalifuatilia suala hilo ili wananchi hao waweze kupata huduma yao ya msingi kwa ni haki yao na shirika linatakiwa kuwapa kwa wakati.

Serikali kudhibiti ukimwi kifikia maambukizi sifuri

 5Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akimpongeza kijana Yohana Haule mwenye umri wa miaka 23 kwa kuchora nembo na kupata tuzo ya kimataifa ya AIDS.
3Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
2Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka akifungua Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
1Mwenyekiti wa wadau wa Maendeleo kwenye sekta ya ukimwi Dkt. Michelle Roland akiwasilisha mada wakati wa Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
6Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka aliyekaa katikati kwenye picha ya pamoja na Wadau mbalimbali walioshiriki Mkutano wa Serikali na wadau wa Ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi.
……………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Serikali imepanga mikakati na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau wa ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanapungua hadi kufikia sifuri ifikapo mwaka 2025.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti mtendaji kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Dkt. Mrisho amesema kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita kwani idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa.
Akitoa mfano Dkt. Mrisho amesema kuwa Mkoa wa Njombe, Shinyanga, Dar es Salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa ambayo inaonyesha kuwa na idadi kubwa ya waathirika wa ukimwi hivyo kuwataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magojwa ya zinaa.
Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Turuka amesema kuwa serikali imedhamiria kuanzisha mfuko utakaokua unashughulikia masuala ya ukimwi wakati wa bajeti ya mwaka 2015/2016 wenye lengo la kuondoa maambukizi mapya ya ukimwi nchini.
Aidha Dkt. Turuka ameitaka jamii kutowanyanyapaa waathirika wa ukimwi bali wawapende na kuwapa moyo ili waendelee kuwa na afya bora kwani serikali inawapigania na kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za kuongeza maisha ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huo.
Mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji wa programu za ukimwi ulianzishwa mwaka 2003 ukifuatiwa na ule wa mwaka 2006 na kuendelezwa kila baada ya miaka miwili ambapo mkutano wa mwaka huu ni wa sita na umebeba kauli mbiu inayosema “Kwa yale mafanikio ambayo tumeyapata mpaka sasa tunayaendeleza”.

SHIWATA YALIA KUMPOTEZA AMIGOLAS

Amigolas_1001
Na Mwandshi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)unaungana na watanzania kuomboleza kifo cha mwanamuziki maarufu Hamisi Kayumbu ‘Amigolas’ aliyefariki Jumapili na kuzikwa Jumatatu iliyopita katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa marehemu Amigolas atakumbukwa kwa mengi aliyoyafanya akiwa mwanachama wa mtandao huo alishiriki kutafuta eneo la makazi ya wasanii ya kijiji cha Mwanzega na shamba la wasanii lililopo Ngarambe wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani.
Alisema alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele pale  alipowahamamisha wanamuziki wenzake kujiunga SHIWATA kutoka bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’akiwemo Luiza Mbutu,marehemu Abuu Semhando na wengine.
Marehemu Amigolas alifariki kwa ugonjwa wa moyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (M.N.H) alipokuwa amelazwa kwa siku tano kabla mauti kumkuta Jumamosi saa tano usiku.
Mkurugenzi wa African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka aliyekuwa mwajiri wake kabla ya kuhamia bendi ya JKT Ruvu alisema marehemu alikuwa mwanamuzi aliyejituma na kufanya kazi kwa juhudi zote kutoka ajiunge na bendi hiyo mwaka 1997.
Hivi karibuni SHIWATA imepoteza wanachama wake maarufu waliofariki akiwemo Abuu Semhando,Amina Ngaluma na Muhidin Gurumo.
Marehemu Amigolas alizikwa na umati mkubwa wa waombolezaji kwenye makaburi ya Kisutu Jumatatu saa 10 jioni. Ameacha wajane wawili na watoto wanne. Mungu ilaze roho marehemu mahali pema peponi. Amen.

AFRICA’S REGIONAL NETWORK FOR YOUTH POLICIES EXPERTS LAUNCHED AT THE FIRST GLOBAL FORUM ON YOUTH POLICIES ON BAKU, AZERBAIJAN.

Invest in Youth Logo 
Africa made history during the closing session of the just concluded First Global Forum on Youth Policies, held in Baku, Azerbaijan by announcing the birth of African Network of Youth Policy Experts (AfriNYPE) to advance the cause of youth policies in the region.
The network was announced at the closing plenary session attended by over 700 invited delegates constituting of experts, researchers, professors, government representatives across the world, and the United Nations Secretary-General’s Envoy on Youth, Mr. Ahmad Alhendawi.
A member of the Steering Committee, Adeola Austin Oyinlade, Human rights lawyer and Youth rights/policy expert from Nigeria described the unveiling as ‘good news from Africa’.
According to Mr. Oyinlade who is also a resource person to the African Union (Youth Division) on the implementation of African Youth Charter, the network’s objectives include establishing a comprehensive research and studies unit, in order to collect reliable data and analyse the current situation of youth policies in order to advise key African Stakeholders on concrete and practical mechanisms, for a more inclusive development and implementation of these policies, while improving legal enabling environment of youth participation in decision making.
Ms. Karima Rhanem, a civil society and youth policy expert from Morocco told the gathering that prior to the global forum, young African delegates to the forum engaged in intensive dialogue, through social media and desk research review to do situation analysis of youth policies in the region, mappings and SWOT analysis, which subsequently produced a concrete strategic document that led to the emergence of AfriNYPE.
According to Ms. Rhanem, AfriNYPE is a collective initiative of experts on youth policies in Africa who shared understanding of the urgent need for concrete development and implementations of youth policies in an African context.
interview with MAG TV 
Seleman Kitenge interviewed with MAG TV.
Yvonne Akoth, a gender equality expert from Kenya and a panelist during the Forum mentioned the need for young African voices to be heard in public policy and youth policy development processes, in preparation for the Post2015 Development Goals.
This would be one of the objectives of AfriNYPE, ‘a network that would build the capacity of young people, by enabling them to understand the importance of policy implementation in addressing issues affecting their overall development’ said by Ms. Akoth.
On the strategy to achieve its objective, Abiola Hamid, a youth leader and Youth expert from Nigeria said the network will develop a common and workable understanding of youth policies with theoretical and practical key indicators. He added that the network intends to create a database and fact files as reference point for youth policy research in Africa, and carry out assessments and evaluations of African youth policies, implementations and impacts on the lives of African youths.
interview with UN RadioSeleman Kitenge interviewed with UN Radio in Baku Azerbaijan.
On what he wants to do differently, Mr. Seleman Kitenge, Communication Personnel and Under Secretary General For Media-GIMUN from Tanzania responded, “I want to see young people have enough understanding of all matters related to policy, as well as being able to have a platform to voice out their views and being part of the problem solving, not being seen as a problems’.
On membership of the Network, Michael Zinkanell from Austria who is working with youth empowerment projects in Uganda said “our members consist of youth policy experts, who are directly working with youth empowerment and/or youth policies, targeting the youth in Africa.
All members should commonly value a democratic, fair and gender-balanced approach on how to improve young African’s life through policy development and implementation, regardless of ethnicity, religion, sexuality, or political orientation’.
Adding further, LombeTembo, an economist and a member of the Youth Governance and Accountability Task Team under Restless Development UK from Zambia said the Network membership base is made up of ‘African youth activists, researchers, policy experts and members of civil society organisations who attended the just ended First Global Forum on Youth Policies’. According to Ms. Tembo, ‘we are looking to widen our membership base and will be reaching out to African youth and youth -led organisations within Africa, as well as African youths in the Diaspora’.
meeting with Envoy2Seleman Kitenge(second left) and his counterparts in a special meeting with the UN Secretary General’s Envoy on Youth Ahmad Elhandawi.
During the AfriNYPE steering committee meeting with the United Nations Secretary-General’s Envoy on Youth, Ahmad Alhendawi charged the young network to take it from ideas to actions.
While also speaking to the United Nations News Centre, Mr. Alhendawi said “we have seen young Africans come together to establish a network for researchers on youth policies. We have seen countries pledging support and commitment and resources to support the global initiative on youth policies. I’ve seen people debating issues around youth policies.”
Since the forum ended in Baku, delegates have returned to their various countries to renew their commitment, engagement and advocacy on youth policy matters. The First Global Forum on Youth Policies was hosted by the Government of Azerbaijan in Baku on 28-30th October, 2014 and was co-organised by the office of the UN Youth Envoy, Council of Europe, UNDP, and UNESCO with technical support of Youthpolicy.org
with minister of sportSeleman Kitenge with the Minister of Youth and Sport of Azerbaijan,H.E Azad Rahimov.

KINUKAMORI WAOMBA DOLA 30,000 KUTENGENEZA AJIRA KWA WATU 300

DSC_0218Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi (wa pili kushoto) akimkaribisha Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez alipowasili kwenye Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP huku akiwa amembatana na Mratibu wa Kitaifa miradi ya COMPACT mkoani Kilimanjaro, Victoria Nderumaki (wa tatu kulia) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto).
Na mwandishi wetu, Moshi
Taasisi isiyo ya kiserikali inayo shughulika na uhifadhi wa mazingira eneo la Kinukamori, Marangu mkoani Kilimanjaro Executive Wilderness Program (EWP) inatafuta dola za marekani 30,000 kwa ajili ya kuendesha program tatu zenye kutengeneza ajira, ujasirimali, utunzaji wa mazingira na mvuto kwa watalii wanaokwenda kupanda mlima Kilimanjaro.
Kauli hiyo wameitoa kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez wakati alipofanya ziara mkoani Kilimanjaro kuangalia miradi inayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
Uongozi wa EWP and Kinukamori Enterprises katika taarifa yao kwa Mratibu huyo, iliyosomwa na Mshauri wao wa fedha Grace Shayo wamesema pamoja na nia yao ya kuhakikisha maporomoko ya Kinukamori yanaendelea, kwanza kama taasisi na pili kama mradi wa kuhifadhi mazingira ya Mlima Kilimanjaro ambao ni sehemu ya urithi wa dunia, wakishirikiana na KINAPA wamefikiria miradi kadhaa ambayo ikienda kwa pamoja itaendeleza eneo hilo.
Wamesema fedha hizo zitatumika kutoa elimu ya ujasirimali kwa vijana 300 wanaoishi katika jamii ya Marangu ambao hutoa huduma mbalimbali kwa wenyeji na pia wageni wakiwemo watalii.
Kundi hilo linalotakiwa kupewa mafunzo ni pamoja na wapagazi 50, waendesha pikipiki 100, wachuuzi 100 na walima mboga 50.
DSC_0221Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisalimiana na Mratibu miradi ya UNDP Kitaifa, Nehemia Mususuri aliyembata na Bw. Alvaro Rodriguez. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises, Bw. Alpha Phares Moshi.
Pia fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuanzisha na kutoa huduma ya chakula kwa wanaopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kupunguza uchafu katika mlima huo na wakati huo huo kuongeza ajira kwa vijana.
Aidha fedha hizo zitatumika kuanzisha kituo cha mazoezi kwa ajili ya wageni wanaotaka kupanda mlima Kilimanjaro kujizoesha na hali ya eneo hilo kabla ya kupanda mlima.
Grace alisema shughuli zote hizo zimelenga vijana kuwa na maeneo ya kudumu yenye ajira endelevu.
Pamoja na kutoa ombi la kusaidiwa kupata fedha hizo, wameshukuru pia kwa misaada iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kupitia COMPACT.Wamesema kama si misaada hiyo eneo hilo ambalo lina historia ya kuharibiwa kwa mazingira yake lisingekuwa linavutia na kutoa ajira kama ilivyo sasa.
Eneo hilo limeboreka mazingira baada ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ya EWP kazi iliyofanywa na Bw. Alpha Phares Moshi ambaye kwa sasa ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa EWP na Mkurugenzi wa Kinukamori Enterprises ambapo kwa kushirikiana na KINAPA na COMPACT vijana walipewa elimu iliyowezesha kutengenezwa kwa mradi wa kuhifadhi mazingira ya mto Una wenye maporomoko ya Kinukamori.
DSC_0231Bw. Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye mradi huo.
Vijana hao ambao ndio wanaoishi katika mteremko wa mlima Kilimanjaro walianza shughuli hizo mwaka 1997 na kuanza kufikiria kuyatengeneza maporomoko ya Kinukamori kama chanzo cha kivutio katika juhudi za kuhifadhi mto Una.
Walisema kwa kuzingatia madhumuni ya kuanzishwa kwa mradi huo vijana na wanawake walianza kurejesha hali ya mazingira kwa kuyaweka bora na kudhibiti uharibifu wa ikolojia.
Kutokana na juhudi hizo miti zaidi ya 5000 mingi ikiwa ya asili ilipandwa kandoni mwa mto na sasa miti hiyo inatumika kutoa mafunzo na kurejesha hali ya upatikanaji wa maji ya kutosha kwa ajili ya wananchi wa Marangu.
Aidha wanyama na ndege waliokuwa wametoweka kutokana na uharibifu wa mazingira uliokuwepo kwanza wameshaanza kurejea eneo hilo.
Pamoja na mafanikio hayo EWP wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ukubwa wa eneo la shughuli zao ambalo ni ndogo na sasa wanataka kusaidiwa kufika hadi maeneo ya chemchem ya Soko iliyopo Kahe.
DSC_0262Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akisoma taarifa ya taasisi yao kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez.
Aidha wamesema wanakabiliwa na tatizo la fedha na hasa kushawishi vijana kujikita zaidi katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na utalii wa kitamaduni.
Naye Mwakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na kuwapongeza EWP kwa kufanikisha kurejesha mazingira katika hali ya kawaida katika eneo hilo amesema kwamba wataendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba shughuli za hapo zinahifadhi mazingira na kutoa ajira kwa vijana.
Alisema duniani nzima kwa sasa inakabiliwa na tatizo la ajira kwa vijana ambao kutokana na kukosekana kwa ajira wanatopea katika ulevi na hivyo kuhatarisha nguvu kazi hiyo muhimu.
Alisema hata Tanzania pamoja na kuanza kufikiria kuwa na uchumi wa gesi, hatua hiyo itachukua muda lakini kuna haja ya vijana wanaomaliza shule wakawajibika katika miradi mbalimbali ya uhifadhi na maendeleo ya kiuchumi.
DSC_0271Mshauri wa fedha wa EWP na Kinukamori Enterprises, Grace Shayo akikabidhi taarifa ya taasisi hiyo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez aliyetembelea mradi wao na kujionea maendeleo yao.
Mwakilishi huyo pamoja na kutotoa ahadi katika ombi la taasisi hiyo amesema kwamba wataangalia nini cha kufanya kwani alifika eneo hilo kujifunza na kuona maendeleo kwani ana miezi miwili tu toka ameingia nchini kuwakilisha mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Alisema amefurahishwa na maendeleo yaliyopo na hasa kwa kuzingatia kwamba kulikuwa na tatizo la raslimali kufanya shughuli hiyo.
Alisema anatambua changamoto zilizopo cha ongezeko la watu, tatizo la ajira kwa vijana na mabadiliko ya tabia nchi na kwamba wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo kuona kwamba changamoto hizo zinakabiliwa na kufutwa.
DSC_0228Bango linaloonyesha tarehe ya kuzinduliwa kwa mradio huo wa COMPACT unaofadhiliwa na UNDP.
DSC_0455Baadhi ya sheria zilizowekwa kwenye maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
DSC_0238Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu akiwa amefuatana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez kutembelea mazingira ya taasisi hiyo pamoja na vivutio vya kitalii vilivyomo kwenye Maporomoko ya maji ya Kinukamori yaliyopo Marangu mkoani Kilimanjaro.
DSC_0276Pichani juu na chini ni mtoa maelezo kwa watalii (Guide) wa EWP na Kinukamori Enterprises, Pascal Cosma akitoa maelezo ya sehemu ya utamaduni wa Kabila la Kichaga kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la maendeleo UNDP, Alvaro Rodriguez aliyembatana na ujumbe wake kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na UNDP.
DSC_0280
DSC_0285
DSC_0283 
Sanamu la aliyekuwa Chifu wa kabila la Wachaga Chifu Thomas Marealle lilipo kwenye taasisi hiyo.
DSC_0293
Pichani juu na chini ni mtoa maelezo kwa watalii (Guide) wa EWP na Kinukamori Enterprises, Pascal Cosma akiendelea kutoa maelezo ya tamaduni mbalimbali za kabila la wachaga ikiwemo na sanamu mbalimbali zilizowekwa kwenye taasisi hiyo.
DSC_0295