TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, June 27, 2016
TASAF YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakiwa katika Mkutano wa kilele cha Maadhimisho
ya wiki ya Utumishi wa Umma uliojadili namna ya kuboresha utoaji wa
huduma kwa wananchi.
Baadhi
ya wafanyakazi wa TASAF wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko huo Bwana Ladislaus Mwamanga, ( hayupo pichani)
kujadili uboreshaji wa huduma za mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa
wananchi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga ( aliyeshika kipaza sauti)
akitoa ufafanuzi juu ya moja ya masuala yaliyoulizwa na wafanyakazi
(hawapo pichani) katika kikao cha kufunga wiki ya utumishi wa umma
yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo jijini Dar esa
salaam.
Mfuko huo wa Maendeleo ya Jamii unaotekeleza Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini , unatoa huduma kwa Zaidi ya Kaya Milioni Moja na Lakini
Moja nchini kote jukumu iliyopewa na serikali katika jitihada zake za
kupambana na Umaskini nchini..
Imearifiwa katika kikao hicho kuwa mafanikio makubwa yameanza
kujitokeza kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambapo wengi
wao wameanza kujiwekea misingi ya kupunguza umaskini kwa kuwa na uwezo
wa kusomesha watoto,kupata huduma za afya,kuwa na uhakika wa lishe na
kuongeza uchumi wao.
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini pia umeanza kusisimua hamasa ya
walengwa wa Mpango huo kuboresha maisha yao kwa kiwango cha kuanza
kuboresha makazi yao kwa kujinunulia mabati na kuezeka nyumba,kuanzisha
miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,mbuzi nahata
nguruwe.
ZOEZI LA UHAKIKI WA VYAMA VYA SIASA LAANZA LEO

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uhakiki wa vyama vya Siasa , Bw. Sisty Nyahoza (kulia) akihakiki daftari lenye orodha ya wanachama wa Chama cha National League for Democratic (NLD) wakati wa zoezi la kuhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho Oscar Emmanuel Makaidi na Katibu Mkuu wa NLD Tozzy Ephraim Matwanga.
Bw. Ibrahim Mkwawa, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa Upande wa Uperembe “Monitoring” (katikati) akikagua nyaraka mbalimbali za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakati wa uhakiki wa utekelezaji wa masharti ya usajili na matakwa ya Sheria ya Vyama vya Siasa lililoanza leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhasibu Bi. Severa Assey kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
WAZIRI NAPE NNAUYE AZINDUA STUDIO YA REDIO YA JAMII KATIKA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA OUT), JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikata utepe wakati wa Uzinduzi wa Redio ya Jamii ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana jambo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa toka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Zulmira Rodrigues wakati wa Uzinduzi wa ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiwa ndani ya Studio ya ‘’Community Media Network of Tanzania (COMNET)’’ akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa Habari mara baada ya kuizindua rasmi 27 Juni, 2016 Jijini Dar es Salaam.
MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI AKANUSHA TAARIFA YA WANYAMA KUCHINJWA MAISARA-ZANZIBAR
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahamoud amekanusha uvumi wa baadhi ya wananchi kuwa wanyama walioshindwa kugombolewa ndani ya muda uliowekwa, kuchinjwa na kuuzwa kwa beinafuu Maisara.
Mkuu huyo alisema taarifa hizo hazina ukweli ukweli ni kwamba wanyama hao wataendelea kutunzwa na Serikali kwa kipindi kinachokubalika na kwa wale ambao watakaoshindwa kuwakombowa wanyama wao watataifishwa na kuwa mali ya Serikali.
Ameyaeleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Afisini kwake Vuga Mjini Zanzibari wakati akitowa taarifa maalumu kwa wananchi wa Mkoa Mjini Magharibi kuhusu Uthibiti wa wanyama kwenye maeneo yasio ruhusiwa.
Hata hivyo amewataka wafugaji kutokubali kutowa fedha kwa wahusika na ukamataji wa wanyama bila ya kupitia taasisi husika (Manispaa), kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa Masheha, Polisi au Manisipaa iwapo kutajitokeza hali hio ili kuzuia vitendo vya rushwa.
Aidha ameeleza katika utekelezaji wa zoezihilo kumejitokeza changamoto zikiwemo malalamiko kwa baadhi ya waumini wa dini ambao wanyama wao wanawatumia kwa ajili ya shughuli za ibada wamekamatwa.
Vilevile kumejitokeza kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaohusisha zoezi hilo na mambo ya kisiasa kwa kuwashajihisha wananchi kuvunja sheria kwa kupingana na utekelezaji wa zoezi hilo.
Alisisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu na Serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi haitokuwa na muhali katika utekelezaji wa kazi zao na atakaekwenda kinyume na agizo hilo hatuwa za kisheria zitachukuliwa zidi yake.
Alifahamisha Utekelezaji wa sheria hizo umekuja kutokana na kukithiri kwa uvunjifu wa nidhamu kwa baadhi ya wafugaji katika maeneo mengi ya Mkoa wa Mjini Magharibi jambao ambalo linasababisha uchafunzi wa mazingira, ongezeko la ajali, kukuthiri kwa wizi, kuanza kwa migogoro baina ya wafugaji na wakulima, uharibifu wa miiundombinu pamoja na uhalifu wa kutumia mapanga.
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU KUKUTANA NA WADAU PAMOJA NA WANANCHI 28 JUNI, 2016
OfisiyaTaifayaTakwimu
Taarifa kwa UmmaKatika kuazimisha “WIKI YA UTUMISHI WA UMMA” yenye kauli mbiu “Uongozi wa Umma kwa ukuaji Jumuishi: kuelekea katika Afrika tunayoitaka”, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inawajulisha wananchi na wadau wote kuwa imetenga siku ya Jumanne tarehe 28 Juni, mwaka huu, kuwa siku maalumu ya kukutana na wananchi ili kutoa elimu na kusikiliza hoja na maoni kuhusu utoaji wa takwimu rasmi nchini.
Muda ni kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 9.00 Alasiri katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu.
KARIBUNI WOTE
ImetolewanaMkurugenzi Mkuu,
OfisiyaTaifayaTakwimu.
WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO MAALUM WA SADC
Mashine za tiketi za kieletroniki kuanza kutumika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine za tiketi zakieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mhandisi kutoka kampuni ya B.C.E.G ya China Bw. Xiong (kushoto) akifafanua jambo kwa Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(kulia) kuhusu mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa leo Juni 27,2016.
Mtaalamu wa Mashine za tiketi za kieletroniki kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel (kushoto) akimuelekeza jinsi ya kutumia moja ya mashine hizo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge alipotembelea kuangalia maendeleo ya uwekaji wa mashine hizo uwanjani hapo Leo Juni 27,2016.
Mtaalamu kutoka kampuni ya Selcom Bw. Adrew Emmanuel akirekebisha moja ya mashine za tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.
Baadhi ya wananchi wakijaribu kutumia mashine ya tiketi za kieletroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika kuingia katika Uwanja wa Taifa hivi karibuni.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Waganga wa tiba asili watakiwa kujisajili
Sunday, June 26, 2016
BREAKING NEWZZZ: Rais Magufuli afanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na afanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Bi. Zainab R. Telack kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Bi. Zainab R. Telack anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Anna Kilango Malecela ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Rais Magufuli pia amemteua Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma. Dkt. Binilith Satano Mahenge anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabit Mwambungu ambaye amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es salaam ambako atapangiwa majukumu mengine.
Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Charles F. Mlingwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Dkt. Charles F. Mlingwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Stanslaus Magesa Mulongo ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Wakuu wapya wa mikoa walioteuliwa wataapishwa tarehe 29 Juni, 2016 saa tatu kamili asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam na mara baada ya kuapishwa watakula kiapo cha maadili ya uongozi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Juni, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 139. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri ambapo kwa wale ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60 ameamua wastaafu. Mhe. Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine.
Katika uteuzi huo, Wakuu wa Wilaya waliopo sasa ambao wamebaki katika nafasi zao ni 39. Pia Rais Magufuli amewateua Wakurugenzi Watendaji wa halmashauri 22 kuwa Wakuu wa Wilaya kutokana na utendaji wao mzuri. Aidha, nafasi 78 za uteuzi wa Wakuu wa wilaya zimejazwa na watanzania wengine ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza wengi wao wakiwa ni vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali. Walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni kama ifuatavyo (Orodha imepangwa kulingana na mikoa)
ARUSHA
1.
Arusha - Mrisho
Mashaka Gambo
2.
Arumeru - Alexander
Pastory Mnyeti
3.
Ngorongoro - Rashid Mfaume
Taka
4.
Longido - Daniel
Geofrey Chongolo
5.
Monduli - Idd Hassan
Kimanta
6.
Karatu - Therezia Jonathan Mahongo
DAR ES SALAAM
1.
Kinondoni - Ally Hapi
2.
Ilala - Sophia
Mjema
3.
Temeke - Felix
Jackson Lyaviva
4.
Kigamboni - Hashim Shaibu
Mgandilwa
5.
Ubungo - Hamphrey
Polepole
Subscribe to:
Posts (Atom)






