Tume huru ya uchaguzi katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imeahirisha kwa mara ya pili kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais ambapo mkuu wa tume ya uchaguzi amesema kuwa yatatangazwa leo Ijumaa.
Tayari asilimia 90 ya kura zimehesabiwa na rais Joseph Kabila  anaongoza kwa asilimia 49 huku mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi  akimfuata kwa asilimia 33, huku Polisi wa kupambana na fujo mjini  Kinshasa walipambana na wafuasi wa upinzani ambao wanadai uchaguzi  ilikuwa na udanganyifu.
Kulingana na kiongozi wa tume ya uchaguzi Daniel Ngoy  Mulunda, wana kibarua kigumu kuhakikisha kuwa matokeo yote  yamethibitishwa kabla ya kutangazwa ambapo Tume ya uchaguzi pamoja na  magavana wa mikoa wametoa wito kwa watu kutulia lakini mwandishi wa BBC  amesema bado kuna shaka kuhusu matokeo ya mwisho ya uchaguzi huo.
Kulitokea shambulio katika mojawapo wa vituo vya kuhesabu  kura katika eneo la Fizi mashariki mwa nchi ambapo Kituo cha radio  kinachofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Okapi, kilitangaza kuwa matokeo ya  mojawapo ya vituo thelathini katika mji wa pili kwa ukubwa Lubumbashi  yamepotea. Inadaiwa kuwa fujo za baada ya uchaguzi ndio zilizosababisha  kupotea kwa matokeo hayo.

No comments:
Post a Comment